Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ameamua kujiuzulu nafasi yake

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ameamua kujiuzulu nafasi yake

Kufa kufaana => Wajanja, madalali wa michezo na wapika majungu na Fitna ni mda wao kuokota pesa za wale maadui wa manji huku wengine wakienda kwa manji kujidai kumpelekea taarifa za uchunguzi wao wanavuta pesa, Mfumo huu wa kuwa na Wanachama wajinga wajinga wenye njaa wapenda Fitna ni Mfumo wa kipumbavu sana, haukuzi soka bali soka la Tanzania litazidi kudidimia kwani endapo Manji ataondoka akaja mwingine bado hao wanachama njaa watamuyumbisha tu, ni wakati wa kuangalia Upya juu mifumo mibovu inayoiongoza soka la Tanzania, kule Ulaya wanachama hawana uwezo wa kuyumbisha Timu kwa majungu na njaa zao hata vilabu vikuwa Africa kusini na kwingineko barani afirika hakuna ujinga kama huu uliopo Yanga.
Huu ujinga uliopo Yanga unataka kutueleza haupo Simba?

Zile dola laki tatu za Okwi zipo wapi?
 
Bado mnaendelea na akili za kumtegemea mtu mmoja mmoja? Na huyo wa bilioni 65 akijitoa ghafla katikati ya msimu, mtaanza kutafuta mwingine? Kwa hizi timu za wanachama, ni lazima wanachama wawe sehemu kubwa ya kuridhisha ya uendeshaji wa timu
Wanachama ni shiiiiida!! Wengi hawana kazi mdo wote wapo pale club ya Yanga kazi yao ni kuomba omba kama matonya, wengi wanaishi kwa majungu na Fitna, hawana Uchungu na Timu bali wapo kwa masilahi ya matumbo yao, Mfumo huu wa kuwa na wanachama wa aina hii unepitwa na wakati maana imekuwa sumu kwa Soka la Tanzania.
 
Ni kweli mkuu huo Ujinga upo hata Simba ingawa wajinga wa Simba kidogo wanajitambua kuliko wajinga wengi waliopo yanga.
Inawezekana wewe ukawa ndio mjinga zaidi, Simba na Yanga hakuna wa kumnyooshea mwingine kidole, Azzam ndio timu pekee mpaka sasa inayoeleweka na siyo hizi porojo zako.
 
JERRY MURO ALIKUWA ANAWANYOOSHA KWA KWELI NAMKUMBUKA KWA MAJIBU YAKE YA KUWAZIBA MIDOMOO.
KWELI MSEMAJI WA TIMUU NDOO KILA KITUU
 
Inawezekana wewe ukawa ndio mjinga zaidi, Simba na Yanga hakuna wa kumnyooshea mwingine kidole, Azzam ndio timu pekee mpaka sasa inayoeleweka na siyo hizi porojo zako.
Wewe utakuwa mkuu wa wajinga huko Azam pia kuna wapenzi wa simba na Yanga jikite kushauri jinsi ya kuondokana na wajinga wenzako kwenye soka la maji taka.
 
Weka wazi HAPA jina lako Kamili Na namba ya Kadi YAKO ili tujiridhishe VIZURI.
Yaani wazee tumefanya fugisu hadi manji ameikimbia timu halafu niweke jina na namba yangu hadharani? Wewe kijana umetumwa na manji au nini unataka?
 
Yanga ilipiga hatua sasa inarudi nyuma kisa wajanja wametumia fursa kula pesa za maadui wa manji na kupenyeza Sumu.
 
Yaani wazee tumefanya fugisu hadi manji ameikimbia timu halafu niweke jina na namba yangu hadharani? Wewe kijana umetumwa na manji au nini unataka?

Mimi pia Ni Mzee Na Sisi Wazee ndio tunajua thamani ya Kuwa mwanachama tumechangia mengi Kwenye timu zetu huwezi kuchukua timu alafu ukasema tu 75% itakuwa Yangu alafu 25% Yenu. HUO ungekuwa ujinga sawasawa Na ule wa sultan Mangungo aliposaini mkataba wa Carl Peters bila HATA kuusoma. Wenzao wa Simba MADA Yao ilipendekezwa kwanza hadharani wakaijadili Kwa Kina Kwa mwezi mzima kabla hawajaenda mkutanoni. YEYE Manji analeta MADA ngumu Kama hiyo Kwa kushtukiza mkutanoni? Ni DHARAU ya kiwango gani hiyo? Halafu anachukua timu wakati YEYE ndiye Mwenyekiti mbona DEWJI hakutaka uenyekiti Simba??? Nakupongeza Mzee mwenzangu Kwa kuukataa UJUHA wa kiwango Cha juu kilichokuwepo duniani kabla mungu hajashusha mitume Na Manabii.
 
Nimeumia sana sanaaa Manji kujiuzulu... sana..na Yanga mtakufa kibudu... nahasira, na mmeniudhi...!! nahama Yanga.. huu sasa ni ubwege kupitiliza.. Manji ameisadia kwa hali na mali Yanga.. kutoka moyoni mwake... ametubeba kwa kila msaada.. alafu uongozi wa Yanga umeacha ujinga na majungu yaendelee, wakati wote huo Yanga inafanya vizuri hao watu wa majungu, uchawi na wapuuzi walikuwa wapi..?

I feel very disappointed... nimeumia sana... Sitaki tena nisikie sijui nn wala nn.. Yanga mtajiju..!! Machizi nn Uongozi wa Yanga... toka kuleee... mkafie mbali....

Ngoja kwanza mkuu.. Huu mchezo hauhitaji hasira....
 
hahahhahahahaha,,, yanga bana.......safari ya matumaini imeisha ghafla.....Mengi tena!!!!! hawa jamaa wawili wana vita yao... na bado haijaisha,,,,huyu alikuja yanga kumuonyesha uwezo yule.....yule katengeneza chokochoko kumkomoa huyu....hii tamthilia ni ndefu sana....vizazi na vizazi........
 
Delina- David Mosha, Mengi, Riz1 nk wasingekubali Manji achukue timu, lemutuz anajua zaidi
 
Back
Top Bottom