Uchaguzi 2020 Mwenyekiti wangu CCM Taifa, Rais Dkt. Magufuli tafadhali achana na Kauli kama hii katika 'Kampeni' zako kwani zinakuharibia na zinachanganya

Si alisema mwenyewe kule Bunda kuwa hajapeleka miradi ya maendeleo Bunda kwa sababu walichagua mpinzani.

Alipokuwa Kilwa law Bwege alisema kuwa hakupeleka pesa za kujenga stand kwa sababu wamechagua upinzani.

Akaenda kule Momba Mbozi alipoambiwa Kero ya maji akawaambia wakamuombe mbunge wao kwa sababu walichagua upinzani.

Jana Kaliua aliwaambia isingekuwa Kapuya asinngepeleka pesa za kujenga barabara sijui Kaliua anayelipa kodi ni Kapuya tu ?

Magufuli ni mbaguzi
 
Sasa Kwa Nini Basi anasema maendeleo hayana Chama? Wakati matamshi yake yanakinzana?Bora TANU yetu ya zamani
 
😂😂😂😂🤣🤣🤣😂🤣🤣🤣
 
tatizo wabunge wa upinzani wanapitia maendeleo anayoyafanya halafu wanamtukana. Yani unajenga hospitali jimbo la upinzani halafu mpinzani anaekutukana kila siku anakuja kusema " miaka mitano iliopita nimefanikiwa kujenga hospitali naomba mnichague tena "
 
Rais wangu si anasema yeye ni mcha Mungu na anataka kukaa pamoja na malaika. Mungu anasema mpende adui yako. Sasa hayo ya chuki siyo ya mcha Mungu. Wapende wananchi wako wote. Kwa nini kubagua watu. Hata kule ambako hawakukuchagua huko nako kuna wanaccm. Sasa unawatesa hata watoto wako kwa chuki binafsi. Tunaposoma maandiko Mfalme Nebukaderesa alinyanganywa ufalme na Mungu wa mbinguni. “ Most High is sovereign over all kingdoms on earth and gives them to anyone he wishes"
 

Una uhakika wa 100% kabisa kuwa hiki ulichokiandika hapa Kimekidhi Wewe Kuonekana ni miongoni mwa 'Great Thinkers' wa JamiiForums Mkuu?
 
Wana CCM Wenzangu leo niwaambieni tu ukweli kuwa Kauli za 'Kibabe' na zenye 'Ubinafsi' kama hizi 'zinamuharibia' mno Mgombea Wetu Dkt. JPM.
Shida mgombea wenu anaona kufanya kampeni ni kama kukamilisha ratiba tu, kwahiyo haoni kama kauli kama hizo zinaweza kumpunguzia kula kwenye uchaguzi huu, ndio maana ameamua kulopokalopoka kama siyo mngomea vile

Kwenye uchaguzi huu mgombea wenu amejipanga zaidi kwenye kuiba kula kuliko kwenye kutafuta kula kwa wananchi, mgombea ambaye amejipanga kuiba kula kama Magufuli, husitegemee hata siku moja akafanya kampeni za maana.
 
Nadhani kichwa chako kina kasoro kubwa kama sio dalili za kuanza kuokota makopo kama mlivyotabiriwa na katibu mkuu Bashiru Ally.Ni wabunge wapi wa CCM ambao hawachaguliwi wakati bunge lililopita wao ndio walikuwa majority.Au hawachaguliwi kivipi wakati uchaguzi haujafanyika.Nadhani kuna dalili za kuchanganyikiwa hapa wakati kampeni ndiyo kwanza mbichi.
 
Wewe ndio kichwa chako kina matatizo tena unafikiria kwa makalio umeweka uccm wako mbele badala ya kuangalia uhalisia soma uelewe kama huelewi tafuta tuition ulipie
 
navyoona mimi CCM wajitahidi kumkumbusha mgombea wao maana wanachama wasijepiga kura za hasira
 
Hii kauli imetolewa zaidi ya nara tano sasa, Chadema hawajacapitalize kwenye huu udhaifu. Amekuwa anatoa kauli zinazopingana. Chadema mnatakiwa kuongea kwa sauti kuhusu hili. Ndio njia pekee ya kumwaibisha!
Kumbe lengo lenu ni kumuaibisha badala ya kuuza sera.Nyie bado sana kuweza kuunda serikali Endeleeni kuwa wapinzani.Ndiyo maana Mbowe kaingia mituni kuepuka aibu.
 
Mkuu GENTANYCINE kwangu kauli hiyo haina unafiki kabisa kwani inawakilisha ukweli (japo hatutaki kusikia na kukubali ukweli) kwamba kipindi chote cha utawala wake viongozi wa upinzani, wawakilishi wa wananchi, hawakumpa ushirikiano. Kibaya zaidi wanabeza juhudi zake alizozifanya kuwaletea maendeleo wapiga kura hata kwenye majimbo ya upinzani.

Mwenye kusikia na asikie. Jimbo litakalomnyima kura mgombea wa CCM maendeleo ya vitu watayasikia kwenye vyombo vya habari tu. Kama ni CHADEMA watawaletea maendeleo ya watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…