Ndugu Mahanju, ni kweli unayoyasema; Lakini, nawaomba Watanzania tutangulize uzalendo kwanza. Uzalendo ambao ndani mwake mna kujitoa (mhanga) kwa hali na mali kwa ajili ya Nchi; kuna kujikana nafsi na kutengeneza kwa ajili ya watoto wetu, watoto wa watoto wetu, watoto wa watoto wa watoto wetu, na kuendelea.
Hebu jiulize, lipi bora, kujinyima (kwa muda) ili kile tunachokusanya tukitumie kujenga kwanza miundombinu mbalimbali (SGR, Stiglers HEP, Barabara nzuri, hospitali na vifaa tiba, eropleni, mifumo ya maji, mashule na vyuo, n.k.); Au, tukitumie kuongeza mishahara ya watumishi, na kadhalika?
Ni wazi huwezi fanya mambo yote kwa wakati mmoja. Hakutokuwa na efficiency. Lazima uwe na priority and options.
"Roma haikujengwa kwa siku moja"; hali kadhalika Ulaya magharibi au Asia. Watu walijifunga vibwebwe na leo hii vitukuu wa vitukuu ndio wanafaidi jasho la babu zao
Kwa hiyo, JPM yuko sawa. Watumishi wa Serikali na Watanzania kwa jumla, tunapaswa kujifunga mkanda na kuridhika na hiki kidogo tunachopata sasa. Ni dhiki ya muda tu kwani tukiisha kamilisha kutengeneza miundombinu hii, Pesa inayokusanywa kutoka vyanzo mbalimbali itatumika sasa kuboresha maisha ya watu. Tena kwa ulaiini kabisa. Serikali itakuwa na uwezo wa hata kufanya KCCCM kuwa zaidi ya 2,000/= kwa mwezi!
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu mbariki JPM.