Uchaguzi 2020 Mwenyekiti wangu Dkt. Magufuli kuna kitu ambacho haukukifanya kitakuangusha tu kwenye Uchaguzi huu

Ila wanajeshi, usalama, wabunge, wao ndio hawapaswi kufunga mikanda?
 
Hapo utakuta umeongea free WiFi,,,upo kitaa mtoto WA kiume umepaka na poda,,hujui kuhusu Jasho labda unalopata Kwa goli la mkono,, kiuno cha Dada ako ndo kinakupa jeuri za Ku comment ujuha!.. Hebu sema hizo mishe zako halali ambazo hazijayumba awamu hii
 
Watanzania tuna mrudisha Rais Magufuli kwa asilimia 99 io moja ilo baki watagawa Tundulisu na Membe
 
Watu wamethubutu, pita Quality Center sasa hivi frem zipo tupu maduka yamefungwa.
Hao walizoea kuingiza containers from abroad na kuzitoa bila ushuru. Zama hizo zimepitwa na wakati, ni wale tu ambao walikua wanalipa kodi ya serikali tangu enzi zile ndio wanaendelea na businesses. Kwa nini huzungumzii Baharesa na wengineo?
 
Matusi hayatakusaida, yanazidi kukupoteza. Bi mdogo msubiri lisu
 
Ngoja waje
 
Hizo 2,000,000/= alizinya wapi?
 

Ukada wa aina hii ni zaidi ya upumbavu na ulofa uliousema Mkapa.

Hao kuku unamuuzia nani watu hawana pesa. Mimi ni Daktari nimejiari,imeshatokea mara tatu kuna jamaa wametoka kijijini huko na wagonjwa wao wakabeba kuku ili wauze wapate pesa kwa ajili ya matibabu. Wamezinguka na kuku wao tena wa kienyeji hawajapata mtu wa kumuuzia mwisho wa siku wakaja kuomba niwatibu wagonjwa wanipe kuku ukabidi niwasaidie tu.
 

Lakini hakuna siku amewahi kusema tunapita kwenye dhiki kila siku anasema tuko vizuri na kuna mmoja amechangia kuwa wale waliozoea ujanja ujanja ndo wanaona maisha magumu. Kwanini tunadanganywa badala ya kuambizana ukweli hakuna jambo baya kama kutudanganya kuwa maisha ni mazuri na uchumi unakuwa vizuri wakati watu wako hoi si wafanya biashara si wafanyakazi si wakulima. Kwa kauli hizo za kejeli na hii hali waliyonao wananchi hakuna tofauti na utawala wa makaburu wa afrika ya kusini ambao walikuwa wanajenga miundo mbinu lakini wananchi wakiwa na maisha magumu hawana uhuru ndiyo maana wakaanzisha mapambano, hakuna kitu kinaweza kuchukuwa nafasi ya uhuru wa watu katika nchi yao kuwepo mazingira mazuri ya kujipatia maendeleo siyo hii hali iliyopo sasa. Tunahitaji mabadiliko hakuna namna.
 
Acha porojo wewe unaenufaika na awamu hii huku wenzako wakiangamia..
 

Kwani kikwete na Mkapa walikuwa wamefunga bomba la ajira Mbona wakati wao miradi ya maendeleo ilifanywa na hali ya maisha ilikuwa nzuri tuache kudanganya hii awamu imeshindwa kabisa ni bora kupisha wengine. Sasa hivi hata ukiwa na bishara hakuna wanunuzi, watu sasa hivi wanaona kula mayai ni luxury kula kuku pia matokeo yake ufugaji umekuwa hauna faida ni hasara tu. Haya maisha gani. Wote wanaosifia wako kwenye system ya utawala wafanya biashara na wakulima wanaelewa hali halisi ilivyo mbaya kimaisha.
 
Atapigiwa kura na flyover, stiglers na zahanati zisizo na dawa. Maisha ya wananchi si lolote wala chochote kwake, vitu kwake ndio cha kwanza kuliko watu.
 

Sera mbovu za Uchumi ndiyo zimetufikisha hapa tulipo haiwezekani watu walikuwa wana makampuni yanafanya vizuri tu hadi yamefilisika halafu mtu anasema anataka ushahidi wa namna uchumi ulivoharibiwa. Kila kitu kimeharibika korosho wote tunaona kilichofanyika huo siyo uharibifu ushahidi gani unataka.
 
Unamaanisha wananchi waishi maisha hayahaya kwa miaka 15 ijayo ambapo SGR itakuwa imekamilika ?
Unamaanisha wafanyakazi wasiongezewe mishahara kwa miaka 15 ijayo?

Unamaanisha uhuru wa kisiasa uaiwepo kwa miaka 15 ijayo kisa tunajenga SGR?

Hiyo si sababu , mkuu wetu alifeli kwenye approach tu kama hizo ni sababu makini alipaswa aahidi hivyo kwenye kampeni zake kuliko kuahidi kinyume huku unatenda kinyume baada ya kuingia madarakani
Kwa wakati wote huo sekta ya kilimo inayowagusa wengi iwe mahututi kisa tunajenga SGR ati tunafunga mkanda duhhh
Hapana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…