Mwenyezi Mungu, nifanye lipi ili ujibu ombi langu, niwe vipi ili unitue mzigo huu? Mbona ni kama umenifumbia macho hunioni

Joined
Nov 3, 2022
Posts
74
Reaction score
146
Mimi sio bora kuliko wengine ila napambana kwa namna ilio haki, kwa namna ilio ya juhudi huku namtanguliza alioiumba dunia hii.

Kila nachogusa ni kama kiko allergic na mikono yangu, hakiwi ridhiki, hakikaii, watoto watakula nini, nimtamtunza vp huyu mrembo ambae Mungu alinijalia.

Mimi ni mpumbavu kuliko wote? Mimi ni mdhambi kuzidi wadhambi wengine?

Je, natwanga maji kwenye kuni? Je nasukuma ukuta? Maana baba jitihada yangu kukufikia hailingani na muelekeo nilio nao.

Mama anataabika, mimi nitaabika, mdogo wangu anataabika,

Nimemuona mama yangu akikuliliia miaka nenda miaka rudi ila bado amekuwa rafiki wa tabu na mateso,.

Je, baba yangu ni laana umeiruhusu katika nzao yake, je ni basi tu hatupo katika mipango ya baraka zako?

Nashuhudia tu makuu ya hii dunia, hata walio na dhambi wakifurahia kiasi, ila mimi nimekuwa cas study ya tabu

Mbona saul alikuwa muuaji ila ulimpa ukuu wa milele, mimi ni wa aina gani hadi niwe mtumwa wa dhiki kiasi hiki

Baba, nimekufanyia makubwa, nimekulilia, hata kama nilikosea ila ilikuwa ni kwa jina lako.

Kwanini utake kuruhusu nifanye maamuzi utafikiri mlugha mlugha ambae hajawi kukutumainia?
 
Mimi sio bora kuliko wengine ila napambana kwa namna ilio haki, kwa namna ilio ya juhudi huku namtanguliza alioiumba dunia hii.

Kila nachogusa ni kama kiko allergic na mikono yangu, hakiwi ridhiki, hakikaii, watoto watakula nini, nimtamtunza vp huyu mrembo ambae Mungu alinijalia.

Mimi ni mpumbavu kuliko wote? Mimi ni mdhambi kuzidi wadhambi wengine?

Je natwanga maji kwenye kuni? Je nasukuma ukuta? Maana baba jitihada yangu kukufikia hailingani na muelekeo nilio nao.

Mama anataabika, mimi nitaabika, mdogo wangu anataabika,

Nimemuona mama yangu akikuliliia miaka nenda miaka rudi ila bado amekuwa rafiki wa tabu na mateso,.

Je baba yangu ni laana umeiruhusu katika nzao yake, je ni basi tu hatupo katika mipango ya baraka zako?

Nashuhudia tu makuu ya hii dunia, hata walio na dhambi wakifurahia kiasi, ila mimi nimekuwa cas study ya tabu

Mbona saul alikuwa muuaji ila ulimpa ukuu wa milele, mimi ni wa aina gani hadi niwe mtumwa wa dhiki kiasi hiki

Baba, nimekufanyia makubwa, nimekulilia, hata kama nilikosea ila ilikuwa ni kwa jina lako.

Kwanini utake kuruhusu nifanye maamuzi utafikiri mlugha mlugha ambae hajawi kukutumainia???
kua na Imani kwa Mungu, walau hata kama punje ya mbegu ya haradali, nae atakubariki na kukujibu maombi na mahitaji yako.

Aimen 🐒
 
Mleta mada punguza matarajio makubwa au ya aina fulani, punguza matazamio ya aina fulani, kuna sisi wenzako huku mfumo wa maisha yetu tukiucompare na wako wewe una weza kua na heri mara nyingi lakini hatuvunjiki moyo au kukata tamaa, maana nilipo mimi kwa sasa hivi sina hakika ya kesho nitakula nini lakini niko na amani maana kuna ambaye yeye hawezi kujilinganisha na mimi nimempita mara nyingi lakini nae ana amani na tumaini pia yupo na furaha, naongea hivi kwa ushuhuda kabisa.
Lisilo kuua linakuimarisha.
 
Nimeipenda hii boss

Maneno mazuri kabisa
 
Ndugu zangu maombi ya usiku wa manane au tisa yana matokeo bora sana,inaonyesha ni kiasi gani unataka msaada wa Mungu

Wakati wenzio wamelala wewe unamtakasa Mungu na kuomba rehema zake,yeyote mwenye changamoto za maisha na madhila mbali mbali awe anaamka usiku mzito walau hata mara tatu kwa wiki kheri kubwa itapatikana
 
Ndugu nimefanya kwa siku 30

Na siku nyingine pia
😢😢😢
 
Usikate tamaa, Endelea kumtumainia Mungu, Kadri Giza linavyozidi kuwa nene, Ndivyo Pambazuko linakaribia. Kumbuka Mungu hachelewi wala hawahi kujibu maombi yetu, Bali hujibu kwa wakati na majira yanayofaa! Huenda anazo sababu zake ambazo sisi hatuzioni wala hatuwezi kuzielewa, Huenda tukaomba gari ila akakawia kujibu ombi akikuepusha na ajali mbaya ambayo ingekupata na hilo gari! Endelea kumuamini Mungu, Yupo, anajua, na atakujibu!
Isaya 41:10 “usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu”.
 
Mleta mada punguza matarajio makubwa au ya aina fulani, punguza matazamio ya aina fulani, kuna sisi wenzako huku mfumo wa maisha yetu tukiucompare na wako wewe una weza kua na heri mara nyingi lakini hatuvunjiki moyo au kukata tamaa, maana nilipo mimi kwa sasa hivi sina hakika ya kesho nitakula nini lakini niko na amani maana kuna ambaye yeye hawezi kujilinganisha na mimi nimempita mara nyingi lakini nae ana amani na tumaini pia yupo na furaha, naongea hivi kwa ushuhuda kabisa.
Lisilo kuua linakuimarisha.
Nikweli,..kinachowauwa wengi ni matarajio makubwa kupita kiasi,...
 
Mungu katuumba ili tumpende, tumuheshimu, tumuabudu, kumtukuza na kumtumikia ili tupate kufika kwake mbinguni. Katika kusali kuna kusifu, kushukuru, kuomba na kuombea wengine! Mungu asikilizi malalamiko au kero; maana kukuweka hapo ulipo na kwa namna ulivyo ana sababu. Shukuru japo tu hata kwa kukupa uhai na utaona malango ya neema yanafunguka!
 
Mimi sio bora kuliko wengine ila napambana kwa namna ilio haki, kwa namna ilio ya juhudi huku namtanguliza alioiumba dunia hii.

Kila nachogusa ni kama kiko allergic na mikono yangu, hakiwi ridhiki, hakikaii, watoto watakula nini, nimtamtunza vp huyu mrembo ambae Mungu alinijalia.

Mimi ni mpumbavu kuliko wote? Mimi ni mdhambi kuzidi wadhambi wengine?

Je natwanga maji kwenye kuni? Je nasukuma ukuta? Maana baba jitihada yangu kukufikia hailingani na muelekeo nilio nao.

Mama anataabika, mimi nitaabika, mdogo wangu anataabika,

Nimemuona mama yangu akikuliliia miaka nenda miaka rudi ila bado amekuwa rafiki wa tabu na mateso,.

Je baba yangu ni laana umeiruhusu katika nzao yake, je ni basi tu hatupo katika mipango ya baraka zako?

Nashuhudia tu makuu ya hii dunia, hata walio na dhambi wakifurahia kiasi, ila mimi nimekuwa cas study ya tabu

Mbona saul alikuwa muuaji ila ulimpa ukuu wa milele, mimi ni wa aina gani hadi niwe mtumwa wa dhiki kiasi hiki

Baba, nimekufanyia makubwa, nimekulilia, hata kama nilikosea ila ilikuwa ni kwa jina lako.

Kwanini utake kuruhusu nifanye maamuzi utafikiri mlugha mlugha ambae hajawi kukutumainia???
Jinsi ulivyolalamika!
Kuna jamaa anaitwa Mauzinde ni shoga lililokubuhu Zanzibar linakula maisha sana na limeenda Canada!
Mungu wetu ni Mungu wa utaratibu. Eñdelea kumwabudu, toa sàdaka, anasikia ila ukikata tamaa lazima utamkaribisha shetani na baraka zote alizokuandalia ndo itakuwa bye bye.
 
Ndugu nimefanya kwa siku 30

Na siku nyingine pia
😢😢😢
Endelea kufanya na funga pia kikubwa uamini kwamba Mungu atakujibu wakati unaofaa,Mungu hawahi wala hachelewi

Kibaya ni kukata tamaa na rehema za Mungu,katu usiseme mbona Sijibiwi maombi yangu,hapo umevunja moja ya nguzo kubwa ya maombi,unatakiwa kuamini kwamba maombi yako yanasikiwa na yanajibiwa

Sisi waislamu kuna aya Allah anamwambia Mtume Wakuulizapo waja wangu kuhusu mimi,waambie nipo karibu yao naitikia maombi yao,wawe na subira,waniitikie na waniamini

Kumuitikia ni pamoja na sisi kutii maagizo yake kwetu,tuache maovu na kufanya mema,subira ni kitu kigumu lakini chenye malipo makubwa sana,Mola wetu anasema yupo pamoja na wenye subira

Kumuamini Mola wetu ndio jambo la msingi sana,unapoomba usiweke mashaka kwamba sijui nitajibiwa au laa,hapo unafeli big time,kama ulikuwa na mtazamo huu ubadili sasa anza kwa imani thabiti na inshallah utajibiwa

Muangalie Ayubu aliumwa kwa miaka 18 lakini hakukata tamaa na rehema za Mwenyezi Mungu

Yunusi alimezwa na Samaki lkn aliomba msamaha na kuomba msaada wa Mola wake na kuokolewa

Ibrahim hakupata mtoto kwa mda mrefu lakini aliomba na hakukata tamaa mwisho ulikuwa mwema

Hizo habar zote za manabii hatukuelezwa bure bali ni mafunzo na mfano wa kuwa na imani thabiti juu ya mwenyezi Mungu,tuige mifano yao

Kikubwa omba toba sana kabla ya maombi,mara nyingi dhambi zetu sisi wanadamu huwa ni kama ngao au ukuta wa kupata rehema za Allah,haimaaniishi wewe una dhambi kubwa laa,ila hii kwa ujumla wake,kwahiyo anza kuomba msamaha kwa dhambi zako kisha omba maombi yako

Kubwa nasisitiza kuwa na imani thabiti juu ya kwamba Mola wako atajibu maombi yako

Pole sana kwa changamoto zako lakini hayo nayo yatapita

Asante
 
Back
Top Bottom