HORSE POWER
JF-Expert Member
- Feb 22, 2015
- 2,238
- 1,577
Habari WanaJF.
Karibuni tupambane kwa hoja. Wote wenye hoja wake hapa tupeane elimu na maarifa. Mimi nitatumia Quran na mazingira yanayotuzunguka.
JE MUNGU YUPO?
Kwangu mimi jibu ni NDIO. Nina sababu mbili za kukubali uwepo wake. Lwanza mimi mwenyewe na mazingira yaliyonizunguka na pili ni miujiza ya kitabu cha Quran. Kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya Quran na mazingira tunayoishi.
Mwenyezi Mungu anasema:
Quran 45:3; "Bila shaka katika mbingu na ardhi ziko alama kubwa za kuonyesha kuwa yuko Mwenyezi Mungu kwa ajili ya wanaoamini".
Quran 45:4; "Na katika umbo lenu na katika viumbe alivyovitawanya, zimo alama vile vile kwa watu wenye yakini."
Quran 45:5; "Na katika kupishana (kufuatana) usiku na mchana, na riziki anayoteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mawinguni (mvua) na akaifufua kwayo ardhi baada ya kufa kwake, na katika mabadiliko ya upepo, zimo alama pia kwa watu wenye akili."
Kumbe hapa tunathibitishiwa na Mwenyezi Mungu kwamba alama za uwepo wake zimetuzunguka. Huyu mwanadamu kwanza aanze kujichunguza yeye mwenyewe kwa umakini; jinsi umbile lake lilivyopangwa kwa ufundi mkubwa, na achunguze utendaji kazi wa mwili wake aone maajabu ya mifumo mingi inavyofanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu bila ya kusigana.
Je, haya masuala yamekuja yenyewe tu? Hakuna aliyeyapanga masuala haya kwa utaalamu na kuyasimamia yakafuata mpango wake?
Itaendelea!