Mwenyezi Mungu: Sifa, Uwezo na Alama za uwepo wake

Hivi kwanini kuna watu wanaamini kuna mungu na kuna watu wanaamini kuwa hakuna mungu? tangu enzi hizo kumekuwa na mvutano huu si jambo la jana wala juzi kuwepo kwa mvutano huu. Haiwezekani pande zote mbili zikawa sawa lazima kuwe na upande ambao ndiyo uko sahihi na mwengine hauko sahihi,lakini mbona hadi leo mvutano huu hauishi kwa kujulikana ni upi upande sahihi?

Mkuu wapo wanaoamini kuwa kuna Mungu ila hakuna WANAOAMINI kuwa Mungu hayupo.
Kutokuwepo kwa Mungu ndo hali halisi sio imani.
Rejea maana ya neno imani
Cc aretasludovick
 
Last edited by a moderator:

Imani ni kutokuwa na uhakika/kutarajia mambo usiyokuwa na uhakika nayo. Ni kama upumbavu fulani lakini unatenda kazi ndani ya mtu kutokana na mind ilivyo.
 
Last edited by a moderator:
Mungu mwenye uwezo wote, utakatifu wote, ujuzi wote na upendo wote asingeumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana.

Utakatifu wake tu usingeruhusu awe na uhusiano wowote na ulimwengu ambao mabaya yanawezekana.

Ukweli kwamba tunaishi katika ulimwengu ambao mabaya yanawezekana unatuonyesha kwamba huyo mungu hayupo, ni wa kufikirika tu.

Ni kama kusema kuna pembetatu ambayo ni duara katika Euclidean geometry, huku ukijua wazi kwamba pembetatu haiwezi kuwa duara na duara halowezi kuwa pembetatu.

Mkuu Kiranga kwanza heshima kwako.Wewe unamjadili MUNGU katika upande mmoja tu wa utakatifu,bila ya kubainisha kwamba hata ubaya pia chanzo chake ni MUNGU.Katika bustani ya Eden kulikuwa na miti miwili.Mmoja wa MEMA NA MABAYA na alieupanda ni MUNGU.Kwa hiyo MUNGU ni chanzo cha mambo yote.Ukisema ni mtakatifu na ubaya usiwepo kumbuka kwamba yeye hajafungwa na wakati wala mfumo.Yuko flexible.Mabaya yametoka kwake na mema yametoka kwake kwa hiyo ubaya Unawezakana mbele zake na wema Unawezakana mbele zake.
 
Wewe ndio unatoa mpya sasa.

Hebu tupe na maana ya ile miti mkuu
 
Last edited by a moderator:
Wewe ndio unatoa mpya sasa.

Hebu tupe na maana ya ile miti mkuu

Mti wa kwanza ulikuwa ni mti wa UZIMA.Huo matunda yake yalikuwa ruksa kula.Hakukuwa na kifo magonjwa njaa wala kazi wala uchungu wa uzazi wala taabu yoyote.Haya ndo maisha uliotakiwa uishi aretasludovic.Na mti wa pili ulikuwa wa MEMA NA MABAYA.Huu walikatazwa asilani wasile matunda yake,ila walikula ndo imepelekea kuwa na taabu kubwa ambayo hii leo imekufanya wewe mkuu uamini MUNGU hayupo.Kabla ya kula haya matunda,wakati binadamu akila yale matunda ya mti wa UZIMA MUNGU alikuwa akikaa mle Kwenye bustani na wanadamu.Alikuwa baba wa familia.Hivyo shida za kiuchumi,kiafya na kimahusiano(ndoa) zisingekuwepo.
 
Maandiko ya biblia yanasema kuwa kabla ya kula tunda walikuwa hawajui jema na baya.
Vipi, wewe unaliongeleaje hili mkuu?
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana na wewe.Haya matunda mimi nimeona kwamba yalibeba mfumo wa maisha ya mwanadamu.

Sasa mkuu ilikuwaje Mungu akawaachia maagizo viumbe visivyojua jema na baya?

Hivi unaweza kumuachia mbuzi maagizo kweli? Mkuu naomba unipe jibu la kueleweka bila kumumunya mumunya.
 
Kwanza siwezi muachia mbuzi maagizo labda kama kutakuwa na uwezo wa mimi kuwasiliana nae au awe na akili.Ila mtoto wangu naweza.MUNGU aliwapa maagizo maana aliwapa ufahamu mzuri na aliwasiliana nao kwa maongezi na mafundisho.Aliwaonya maana walikuwa kama watoto wasiojua mazingira yao.Hivyo kwa kuwa MUNGU aliyajua mazingira kushinda wao ndo alikuwa akiwaelekeza taratibu.Maana yeye ndo alieandaa mazingira yote waliokuwa na waliotakiwa wayatawale.
 
Kumbuka Adamu alikuja duniani kichwa kikiwa empty kama cha mtoto mchanga.Na MUNGU ndo alikuwa akimfeed vitu.Kwa hio utoto wake baba mlezi wake alikuwa MUNGU.
 
Kwanza siwezi muachia mbuzi maagizo labda kama kutakuwa na uwezo wa mimi kuwasiliana nae au awe na akili.Ila mtoto wangu naweza.MUNGU aliwapa maagizo maana aliwapa ufahamu mzuri na aliwasiliana nao kwa maongezi na mafundisho.Aliwaonya maana walikuwa kama watoto wasiojua mazingira yao.Hivyo kwa kuwa MUNGU aliyajua mazingira kushinda wao ndo alikuwa akiwaelekeza taratibu.Maana yeye ndo alieandaa mazingira yote waliokuwa na waliotakiwa wayatawale.

Hapana! Hili sio jibu. Unajua maana ya kitu kisichojua jema na baya?
 
Mungu hahukumu kwa kitu kisichokuwa na uwezo wa kujua jema au baya,binaadam kapewa uwezo wa kujua jema na baya na ndio maana ataenda kuulizwa kwa aliyoyafanya hapa duniani,je wewe huna uwezo wa kutambua jema na baya?kwa vyovyote uwezo unao wa kutambua jema na baya na ndio maana huwezi kulala kitandanda kimoja na nduguyo wa kike.
 
Mungu hahuku kwa kitu kisichokuwa na uwezo wa kujua jema au baya,binaadam kapewa uwezo wa kujua jema na baya na ndio maana ataenda kuulizwa kwa aliyoyafanya hapa duniani,je wewe huna uwezo wa kutambua jema na baya?kwa vyovyote uwezo unao wa kutambua jema na baya na ndio maana huwezi kulala kitandanda kimoja na nduguyo wa kike.

Rudia kusoma comments za nyuma uache kukurupuka
 
Mungu hahukumu kwa kitu kisichokuwa na uwezo wa kujua jema au baya,binaadam kapewa uwezo wa kujua jema na baya na ndio maana ataenda kuulizwa kwa aliyoyafanya hapa duniani,je wewe huna uwezo wa kutambua jema na baya?kwa vyovyote uwezo unao wa kutambua jema na baya na ndio maana huwezi kulala kitandanda kimoja na nduguyo wa kike.

ahsante sana nakiri nimekuelewa sana tangu uliposema kuhusu Mungu kuumba mabaya na mzuri na jins unavyojibu hapa! natamani muanzisha uzi angejibu hivi,kama unaweza kumpata muanzisha uzi kuna kitu kimenichanganya au kama utakiweza hata wewe nijibu tu maana ni kama kimenitoa ktk imani nacho ni kuhusu Mungu kusema kuna watu atawapa mioyo migumu ya kutomjua yeye,hiki kimenivuruga maana kweli wapo watu ni hivyo makosa yao ni nin wakati wanazaliwa hawajui lolote,yeye Mungu ndie muweza wa vyote hivyo kwa imani yangu kama ameamua kuufanya moyo wangu uwe mgumu basi hata nifanyeje sitaweza,kama kuna andiko la ufafanuz wa hili naomba tafadhali
 
Ndugu yangu Lamalu,ahsante kwa swali zuri.Nakujibu kama ifuatavyo:
Kwanza tambua mwanadamu ni kiumbe aliye katika mtihani.Kufaulu au kutofaulu mtihani hiyo ni suala la mwanadamu mwenyewe kwa sababu amepambanuliwa njia zote mbili;HAKI na BATILI.Matokeo ya kila njia ameshaambiwa kwa hiyo ana hiari.
Mwenyezi Mungu hailazimishi nafsi ya mtu kufanya mema au mabaya,suala la kuwa na moyo mgumu kuliko jiwe sababu ni mtu mwenyewe.Hebu angalia;mwanadamu huyu kapewa AKILI ya kutambua jema na baya,kaletewa na mitume na manabii ili wamfikishie ujumbe na kumuonya na vitabu vya dini kaletewa.Yote kwa pamoja vimeletwa kumsaidia mwanadamu kuitambua njia sahihi.Lakini kuna watu humu duniani,hata umuelezeje,hata umuonyeje,tumia kila mbinu kumfikishia ujumbe wa Mungu BADO ATAPINGA.Tena anazidisha kasi ya maasi kwa kiburi na inda,mtu wa namna hii ndio Mwenyezi Mungu anasema wana mioyo migumu kuliko jiwe.Watu wa namna hii wameamua wenyewe kupotea kwa sababu Mwenyezi Mungu anamuongoza aliye tayari kuongozwa.
 
Hujajibu swali! Hapa umezunguka na kukubali kwamba watu wa aina hiyo wapo.
Lakini unalizunguka swali la muuliza swali na kujifanya kwamba wao ndio wameamua wawe hivyo ilihali maandiko yanasema mungu ndio kawafanya wawe hivyo.
 
Hakuna andiko linalosema kwamba Mungu amewafanya watu fulani kuwa ni mioyo migumu kama jiwe.Ni suala tu kutoielewa aya.Kinachozungumzwa hapo ni kwamba moyo wa mwanadamu huwa mgumu kadiri anavyokithirisha maasi.Na chanzo kikubwa hapa ni nafsi.Na hapa nazungumzia inayoamrisha maovu.Nafsi hii humuongoza mwanadamu kufanya maasi dnidi ya Mungu,na mwanadamu kadiri anavyofanya maasi moyo hujenga kutu na kuwa mgumu.Moyo wa namna hii huwa sugu katika maasia.Hawa ndio Mwenyezi Mungu anasema wana mioyo migumu kuliko jiwe.Wamekithirisha maasi kwa kufuata matamanio ya nafsi zao;hata uwaonye,uwanasihi,uwahimize habari ya Mungu HAWATOBADILIKA maana nyoyo zao zimekua sugu maana ndio njia waliochagua.
Ieleweke kwamba mwanadamu yuko huru kuchagua;aidha aende kwenye HAKI au BATILI.Mwenyezi Mungu kaleta miongozo tu kwa huyu mwanadamu;kwa hiyo ana hiari aidha afuate miongozo hiyo ya mola wake ya kumpeleka kwenye kufaulu au afuate matamanio ya nafsi yake yanayopambwa na ibilisi na kumpeleka kwenye kufeli na hasara kubwa.
 
Back
Top Bottom