Shing Yui
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 15,168
- 38,049
Hakuna andiko linalosema kwamba Mungu amewafanya watu fulani kuwa ni mioyo migumu kama jiwe.Ni suala tu kutoielewa aya.Kinachozungumzwa hapo ni kwamba moyo wa mwanadamu huwa mgumu kadiri anavyokithirisha maasi.Na chanzo kikubwa hapa ni nafsi.Na hapa nazungumzia inayoamrisha maovu.Nafsi hii humuongoza mwanadamu kufanya maasi dnidi ya Mungu,na mwanadamu kadiri anavyofanya maasi moyo hujenga kutu na kuwa mgumu.Moyo wa namna hii huwa sugu katika maasia.Hawa ndio Mwenyezi Mungu anasema wana mioyo migumu kuliko jiwe.Wamekithirisha maasi kwa kufuata matamanio ya nafsi zao;hata uwaonye,uwanasihi,uwahimize habari ya Mungu HAWATOBADILIKA maana nyoyo zao zimekua sugu maana ndio njia waliochagua.
Ieleweke kwamba mwanadamu yuko huru kuchagua;aidha aende kwenye HAKI au BATILI.Mwenyezi Mungu kaleta miongozo tu kwa huyu mwanadamu;kwa hiyo ana hiari aidha afuate miongozo hiyo ya mola wake ya kumpeleka kwenye kufaulu au afuate matamanio ya nafsi yake yanayopambwa na ibilisi na kumpeleka kwenye kufeli na hasara kubwa.
Kwenye quran lipo na kwenye biblia hebu kasome kutoka 7 mstari wa 3.