Jimena
JF-Expert Member
- Jun 10, 2015
- 25,935
- 96,056
kabla sijakujibu wewe unaelewa nini maana ya dini?
Kwani hapa tunaongelea dini au Mungu?
Dini ni neno la kiarabu linalomaanisha njia
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kabla sijakujibu wewe unaelewa nini maana ya dini?
Kwamna hoja ni ngeni au si ngeni si jambo la msingu, na sijaona umuhimubwa kusema hoja si ngeni.
Cha muhimu ni hoja kupata jibu.
Unalo jibu la hoja?
Watu waliposhindwa kujibu "Poincare's Conjecture" hawakulitatua kwa kusema "swali hili lina zaidi ya miaka 200 halijajibiwa". Si geni. Walitafuta jibu mpaka wakalipata.
Swali hiki nimelisoma mara ya kwanza miaka takriban 20 iliyopita, katika kitabu cha "Philosophy of Religion: An Anthology". Na limejadikiwa kwa mamia kama si maelfu ya miaka, bila jibu la kuridhisha kutoka kwa wale wanaosema mungu huyu yupo.
Swali la msingi kabisa ni hili.
Kwa nini mu gu mwenye iwezo wote, ujuzi wote na yoendo wote hajaumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani wakati ambapo alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Hujalijibu.
Nukuu zako ni hafifu na hazijibu swali.
Kwani zinatoa uwezekano wa mungu kushindwa kuumba ulimwengu usio na mabaya.
Hazijibu swali, zinarudi kwenye msi gu wa mimi kuyliza swali.
Eti mungu yupo
Afu mtu ana qoute Qur'an
Nani kasema Qur'an ndio kitabu cha kutoa facts.
Wewe uliye qoute unahitaji usome Darwin's book entitled The Origin of Species
Ndugu yangu,Charles Darwin ni binadamu.Ni mwanasayansi na anayeheshimika.Sasa ikiwa aliweza kufanya tafiti nyingi za kisayansi,unadhani huo uwezo alionao kaupata wapi?
Mimi nawaachia wa nukuu Quran, maana ndicho kutabu wanachokuamunu.
Katika Quran, imeandukwa kwamba kuna watu mungu atawafanya mioyo yao iwe migumu kumuelewa. Hata wafanyeje hawatapata rehema ya kumjua. Ndivyo alivyotaka mwenyewe.
Sasa nawauliza. Inakuwaje mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote akawa na roho mbaya hivyo?
Hao watu wamemkosea nini mpaka awapangue hivyo?
Na kama yeye mwenyewe ndiye aliyewapangia kutomjua hata wafanye nini, siku ya kiama atawahukumu? Kwa kosa gani?
Mpaka sasa sijapewa jibu.
Ndio maana nasema usome usome The Origin of Species
Utaelewa uwezo wote aliupata wapi.
Au wewe unafikiri alipewa na mungu?
Swali zuri sana ndugu yangu.Naomba nikujibu kama ifuatavyo,iwe ni faida pia kwa wale wenye swali kama lako.
Quran 76:1; "Hakika ulimpitia binadamu wakati mrefu katika dahari,hakuwa kitu kinachotajwa.(Binadamu ndiye kiumbe wa mwisho kuletwa ulimwenguni).
Quran 76:2; "Kwa hakika tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyochanganyika;(ya mwanaume na mwanamke),ili tumfanyie mtihani (kwa amri zetu na makatazo yetu);kwa hiyo tukamfanya ni mwenye kusikia na mwenye kuona."
Quran 76:3; "Hakika sisi tumemuongoa,(tumembainishia njia zote mbili;kuwa hii ndio ya kheri na hii ndio ya Shari).Basi (mwenyewe tena) atakuwa mwenye Shukrani au awe mwenye kukufuru. (kukanusha)."
Hapo jibu liko wazi kwamba huyu mwanadamu ana hiari ya kuchagua;aidha kushukuru au kukufuru kwani kawekewa wazi kila kitu.Na kapambanuliwa njia ya uongofu na upotevu;kwa hiyo ni juu yake kuchagua kwani huo ni mtihani.Na Mwenyezi Mungu kaumba maovu kama mtihani kwa wanadamu.
Wewe ni mwanasayansi,nijibu kwa mujibu wa sayansi.
Ni jambo jema na linalopendeza kwamba hapa JF kuna wasomi wengi na wazuri,na hasa masuala ya sayansi.Mimi nimeishia darasa la saba.Bila shaka nitapata elimu.
Nina maswali matatu kwenu mnaokanusha uwepo wa Mungu kwa hoja za kisayansi:
1.Ni wapi/nini/nani asili au chanzo cha sayansi?
2.Hao wanasayansi wametumia uwezo mkubwa wa akili katika tafiti zao.Je,ni wapi asili ya huo uwezo wao wa kiakili?
3.Ni kwanini basi kwa uwezo wao huo wameshindwa kubuni mkakati wa kisayansi ili wasife au kuurudisha uhai?
Kitu chochote cha kisayansi lazima kiweze kutafitiwa na kupata uhakika wa mambo yanavyokwenda. Sayansi ni juhudi tu ya mwanadamu kujiongezea maarifa ili aweze kuishi katika dunia hii. Hadi sasa ufahamu wa mwanadamu na uelewa wake kuhusu mazingira yake ameweza kuupata kwa muda mrefu na kadri anavyopata changamoto katika maisha yake. Vitu vyote anavyogundua mwanadamu kupitia utafiti wake kwakweli siyo kwamba havipo bali vipo tangu dunia ilipoumbwa. Ila juhudi za kuzivumbua hizo tunu ndio zinachukua muda mrefu kupitia wanadamu kujifunza na kuchunguza dunia na ulimwengu kwa ujumla. Hadi sasa mwanadamu kupitia ugunduzi wake ambao tunauita sayansi ameweza kufahamu dunia na ulimwengu kwa kiasi kidogo sana. Haitafika siku binadamu akayaelewa mambo yote yanayomzunguka. Hata kama atasoma vitabu vyote vitakatifu. Hata tunaowaita manabii na mitume wa mungu mwenyewe hawakuyafahamu mambo yote japo waliweza kufanya mambo mengi ambayo kwa watu wengine yalionekana kama maajabu au miujiza. Hata ufahamu wetu kuhusu mungu hatujaweza kuupata wote na hivyo hakuna hata mtu au mtume au nabii atakayesema anazifahamu siri zote za uungu. Kwahiyo, katika kuchangia mada hii ninachoweza kusema ni kuwa sayansi haitakoma kwani binadamu hajafaham mambo yote na wala sayansi ya ugunduzi kwa maana ya kujifunza mambo mapya haitakoma na wala binafamu hana uwezo wa utambuzi wa mambo yote ya dunia hii. Inatosha tu kuamini kuwa kuna mambo hatuyajui na wala hatutayajua yote hata kama tutalala macho. Kama hatuamini tujiulize kwann tunalala usingizi bila kujijua? Ni dakika ipi na nukta ipi mtu anaweza kusema alilala!!! Na ndio maana maandiko matakatifu yanatufunfisha kuwa mungu ni MWENYEZI (God is almighty) NI MUWEZA WA YOTE, ALIKUWEPO, YUPO ATAENDELEA KUWEPO NA HAFANANISHWI NA CHCHOTE. Ndiyo maana yote hayo tunayapokea kwa IMANI. Kama unaamini unaishia kusema AMINA. Hata kwa anayebisha hawezi kuwa na majibu, kwani mwenye majibu ya yote ni MUNGU MWENYEWE. Siku ikitokea binadamu awaye yote akawa na majibu ya yote hayo basi HUYO ATAKUWA NI MUNGU MWENYEWE. Ulimwengu hauna mwisho, na mambo yake yote hayana mwisho. Uwezo wetu wa kufikiri una mwisho na ndio tofauti yetu kati yetu na Mungu. Kwa akili zetu hatuwezi kuyajua yote kwasababu sisi sote ni WANA WA ADAM.
Allah ni malikia wa malikia!
Kumbe huyo Allah ni wa kike?
Hebu nielezee vyema mkuu huu umalkia wake ulianza lini au aliupataje pataje, je kuna mfalme pia hapo pembeni yake?
Aisee! Hata mimi naanza kushangaa.
Allah ni malikia wa malikia!
Ni jambo jema na linalopendeza kwamba hapa JF kuna wasomi wengi na wazuri,na hasa masuala ya sayansi.Mimi nimeishia darasa la saba.Bila shaka nitapata elimu.
Nina maswali matatu kwenu mnaokanusha uwepo wa Mungu kwa hoja za kisayansi:
1.Ni wapi/nini/nani asili au chanzo cha sayansi?
2.Hao wanasayansi wametumia uwezo mkubwa wa akili katika tafiti zao.Je,ni wapi asili ya huo uwezo wao wa kiakili?
3.Ni kwanini basi kwa uwezo wao huo wameshindwa kubuni mkakati wa kisayansi ili wasife au kuurudisha uhai?