Mwenyezi Mungu: Sifa, Uwezo na Alama za uwepo wake

Mwenyezi Mungu: Sifa, Uwezo na Alama za uwepo wake

Hakuna andiko linalosema kwamba Mungu amewafanya watu fulani kuwa ni mioyo migumu kama jiwe.Ni suala tu kutoielewa aya.Kinachozungumzwa hapo ni kwamba moyo wa mwanadamu huwa mgumu kadiri anavyokithirisha maasi.Na chanzo kikubwa hapa ni nafsi.Na hapa nazungumzia inayoamrisha maovu.Nafsi hii humuongoza mwanadamu kufanya maasi dnidi ya Mungu,na mwanadamu kadiri anavyofanya maasi moyo hujenga kutu na kuwa mgumu.Moyo wa namna hii huwa sugu katika maasia.Hawa ndio Mwenyezi Mungu anasema wana mioyo migumu kuliko jiwe.Wamekithirisha maasi kwa kufuata matamanio ya nafsi zao;hata uwaonye,uwanasihi,uwahimize habari ya Mungu HAWATOBADILIKA maana nyoyo zao zimekua sugu maana ndio njia waliochagua.
Ieleweke kwamba mwanadamu yuko huru kuchagua;aidha aende kwenye HAKI au BATILI.Mwenyezi Mungu kaleta miongozo tu kwa huyu mwanadamu;kwa hiyo ana hiari aidha afuate miongozo hiyo ya mola wake ya kumpeleka kwenye kufaulu au afuate matamanio ya nafsi yake yanayopambwa na ibilisi na kumpeleka kwenye kufeli na hasara kubwa.

Kwenye quran lipo na kwenye biblia hebu kasome kutoka 7 mstari wa 3.
 
Mungu hahukumu kwa kitu kisichokuwa na uwezo wa kujua jema au baya,binaadam kapewa uwezo wa kujua jema na baya na ndio maana ataenda kuulizwa kwa aliyoyafanya hapa duniani,je wewe huna uwezo wa kutambua jema na baya?kwa vyovyote uwezo unao wa kutambua jema na baya na ndio maana huwezi kulala kitandanda kimoja na nduguyo wa kike.

nani alimzawadia mwanadamu uwezo wa kujua mema na mabaya?

ni shetani au Mungu?
 
nani alimzawadia mwanadamu uwezo wa kujua mema na mabaya?

ni shetani au Mungu?

Ni Mwenyezi Mungu ndiye aliyempa mwanadamu akili ya kupambanua jema na baya.Na kwa mapenzi makubwa ya Mungu kwetu AMETUWEKEA WAZI kwamba baya lipi na jema ni lipi.
 
Mti wa kwanza ulikuwa ni mti wa UZIMA.Huo matunda yake yalikuwa ruksa kula.Hakukuwa na kifo magonjwa njaa wala kazi wala uchungu wa uzazi wala taabu yoyote.Haya ndo maisha uliotakiwa uishi aretasludovic.Na mti wa pili ulikuwa wa MEMA NA MABAYA.Huu walikatazwa asilani wasile matunda yake,ila walikula ndo imepelekea kuwa na taabu kubwa ambayo hii leo imekufanya wewe mkuu uamini MUNGU hayupo.Kabla ya kula haya matunda,wakati binadamu akila yale matunda ya mti wa UZIMA MUNGU alikuwa akikaa mle Kwenye bustani na wanadamu.Alikuwa baba wa familia.Hivyo shida za kiuchumi,kiafya na kimahusiano(ndoa) zisingekuwepo.

Sasa kwanini alipanda mti ambao anajua fika ukasababisha matatizo? Huo mti wa kujua mema na mabaya ulikuwa na ulazima gani kuwepo?

Na kama watu walikuwa bado hawajajua mema na mabaya, yeye aliwapaje onyo kuwa wasile tunda kutoka kwenye mti huo?
Na kama mwanzoni walikula tunda la uzima kwanini walikufa? Au tunda hilo lilikuwa halifanyi kazi vizuri?
 
Last edited by a moderator:
Wapi hapo huyo Mungu ametuweka wazi? Ikiwa hata yeye mwenyewe ameshindwa kujiweka wazi?

Ameshindwa kujiweka wazi kivipi? Mwenyezi Mungu amejipambanua kwa ALAMA au DALILI nyingi mno.Wewe mwenyewe ni alama ya kwanza kabisa ya uwepo wa Mungu.We uliataka kumuona physically?
 
Ameshindwa kujiweka wazi kivipi? Mwenyezi Mungu amejipambanua kwa ALAMA au DALILI nyingi mno.Wewe mwenyewe ni alama ya kwanza kabisa ya uwepo wa Mungu.We uliataka kumuona physically?

Sasa HORSE POWER we unataka kuleta hadithi za abunuwasi tu, huyo Mungu amejipambanua wapi? Acha ngonjera mkuu unapojibu hoja ni lazima uambatanishe na vithibitisho.
 
Last edited by a moderator:
Sasa kwanini alipanda mti ambao anajua fika ukasababisha matatizo? Huo mti wa kujua mema na mabaya ulikuwa na ulazima gani kuwepo?

Na kama watu walikuwa bado hawajajua mema na mabaya, yeye aliwapaje onyo kuwa wasile tunda kutoka kwenye mti huo?
Na kama mwanzoni walikula tunda la uzima kwanini walikufa? Au tunda hilo lilikuwa halifanyi kazi vizuri?

Hili swali la MUNGU ALIWAACHIAJE MAAGIZO/ONYO VIUMBE AMBAO HAWAJUI JEMA NA BAYA, ndio naulizaga sana lakini wanalikimbia mkuu
 
Ameshindwa kujiweka wazi kivipi? Mwenyezi Mungu amejipambanua kwa ALAMA au DALILI nyingi mno.Wewe mwenyewe ni alama ya kwanza kabisa ya uwepo wa Mungu.We uliataka kumuona physically?

Sisi tunahoji uwepo wa Mungu na sifa zake wewe unasema kuwa sisi ni alama ya Mungu?
 
Ni Mwenyezi Mungu ndiye aliyempa mwanadamu akili ya kupambanua jema na baya.Na kwa mapenzi makubwa ya Mungu kwetu AMETUWEKEA WAZI kwamba baya lipi na jema ni lipi.

kasome tena biblia halafu ndiyo uje hapa kubishana na sisi!!

aliyekuzawadia ujuzi wa mema na mabaya kulingana na biblia ni Ibilisi,na baadae Mungu mwenyewe aka confirm kuwa ibilisi ni mkweli(ref:genesis 3:22)

kitu cha ziada ambacho Mungu alikifanya baada ya Adam's deception ni kumzuia kuwa immortal sinner.
(case closed)

anyway,wewe bado ni mwanafunzi sana katika dini,nakushauri ukajifunze kwanza halafu rudi hapa,sisi utatukuta tu.

NB:if you don't believe in bible,i will use quran to verify my statement above.
 
Back
Top Bottom