Mwenyezi Mungu, twaomba uyafungue macho ya rais wetu

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
790
Reaction score
1,316
Kwa wasomaji wa historia ya uprotestant watakuwa wanakumbuka dua maarufu; "Lord, open the King of England's eyes" ya William Tyndale, aliyoiomba akiwa anachomwa moto October 1536 kwa kosa la kutafsiri Biblia kwa lugha ya kingereza. Kwa faida ya wasiofahamu, mpaka karne ya 16, dini pekee katika eneo lote la Ulaya ilikuwa ni Ukatoliki, na misa zilikuwa zikiendeshwa kwa lugha ya kilatini (Latin mass), jambo ambalo wanamageuzi wengi wa kiroho hawakuwa wakikubaliana nalo. Kutafsiri Biblia katika lugha ya kiingereza wakati huo ilikuwa ni fundisho potovu (heresy) na adhabu ya mtu heretic ilikuwa nikuchomwa moto hadharani mpaka ufe. Kwa hiyo dua hii ya William Tyndale ilikuwa ikiomba rehema kwa Mwenyezi Mungu, kuyafungua macho ya Mfalme Henry VIII, dhidi ya madhila haya yaliyokuwa yakitekelezwa kwa mkono wake dhidi ya wanamageuzi.

Nimelejea kisa hiki kwasababu kinaweza kuwa na mfanano fulani wa muktadha baina ya hali iliyopelekea dua hii kutolewa na kile alichokiongea Askofu Gwajima, May 24, 2025 kuhusu utekaji, utesaji na uuaji kwa upande mmoja na hoja za makundi mbalimbali yanayoendelea kumjibu hotuba yake hiyo kwa upande mwingine. Kuhusu kuwa aliyoyasema Askofu yana merits au hayana merits, hilo ni jambo ambalo nakuombea dua Mwenyezi Mungu afungue macho yako uone mwenyewe uhalisia wake ulivyo. Isipokuwa uniruhusu kufafanua kuwa, wakati akina Tyndale na wafia dini wengine wa Oxford; akiwepo askofu Hugh Latimer, Nicholas Ridley na Thomas Cranmer aliyekuwa Archbishop wa Canterbury; wakichomwa moto wakiwa hai, lilikuwepo kundi kubwa lenye nguvu, ambalo kutokana na kunufaika kwake, lilikuwa likiwachochea wafalme wa Ulaya kutekeleza unyama huu. Wasiwasi ni kuwa, Je, kinachoendelea katika mjadala huu sasa, hakiakisi historia hii hata kama motives zaweza kuwa tofauti?

Mh Rais, mm ni mwana CCM, ingawa sijashika nyazifa kubwa za juu, kipo kisa naweza kukushirikisha. Mwaka 2013/2014, mm nikiwa mwenyekiti wa CCM shirikisho mkoa wa Kilimanjaro, kuna waziri wa viwanda na biashara(sasa ni marehemu), tukiwa Nyumbani kwa Mchumi wa mkoa, na baadhi ya viongozi chama wakiwepo, alimsema vibaya sana rais Kikwete kwa mambo ambayo hakuwahi kusikika akiyapinga mbele ya kamera za vyombo vya habari. Ingawa haikuchukua muda ailitenguliwa, ila kuna kitu cha kujifunza. Sisemi hivi kumaanisha wasaidizi wako wapo hivi, ila kujaribu kukueleza sisi wana CCM tulivyo. Sio kila anayemjibu Gwajima kwenye hili, tena kwa kauli zinazoleta ukakasi, anasema hivi kukutetea, wengine wanajikosha tu wapate ugali wao, ila pembeni wanaweza kuwa wanakung'ong'a.

Mh. Rais, mie sina mashaka na ushindi wako katika uchaguzi mkuu ujao. Mpaka sasa sijaona chama chochote cha siasa kinachoweza kuwa tishio kwako. Changamoto kubwa kwako wewe uliyonayo ni LEGACY. Baada ya urais wako 2030 utakumbukwaje? Huu ndio ushindi mkubwa, ambao kwa dua zangu, namwomba Mwenyezi Mungu akuwezeshe kuuona. Ukiwa rais, utasikia mengi, wapo wanaojifanya wanakusaidia kumbe, wanatengeneza ukaribu na wewe ili kujisaidia wao. Ni Mwenyezi Mungu tu ndiye anayeweza kukuongoza kuona upendo au ghiriba za watu wanaokuzunga na kung'amua dhahiri zao. Matamanio yetu wengine ni kuona urais wako unakuwa uthibitisho usio na shaka kuwa wanawake ni viongozi bora.

Najua ww ni muislamu, lakini naamini waislamu na wakristo sote tunakubaliana kuhusu nabii au mfalme Suleiman. Ikikupendeza waweza soma 1Wafalme 3:1-15.
 
Kwa wasomaji wa historia ya uprotestant watakuwa wanakumbuka dua maarufu; "Lord, open the King of England's eyes" ya William Tyndale, aliyoiomba akiwa anachomwa moto October 1536 kwa kosa la kutafsiri Biblia kwa lugha ya kingereza. Kwa faida ya wasiofahamu, mpaka karne ya 16, dini pekee katika eneo lote la Ulaya ilikuwa ni Ukatoliki, na misa zilikuwa zikiendeshwa kwa lugha ya kilatini (Latini mass), jambo ambalo wanamageuzi wengi wa kiroho hawakuwa wakikubaliana nalo. Kutafsiri Biblia katika lugha ya kiingereza wakati huo ilikuwa ni fundisho potovu (heresy) na adhabu ya mtu heretic ilikuwa nikuchomwa moto hadharani mpaka ufe. Kwa hiyo dua hii ya William Tyndale ilikuwa ikiomba rehema kwa Mwenyezi Mungu, kuyafungua macho ya Mfalme Henry VIII, dhidi ya madhila haya yaliyokuwa yakitekelezwa kwa mkono wake dhidi ya wanamageuzi.

Nimelejea kisa hiki kwasababu kunaweza kuwa na mfanano fulani wa muktadha na hali iliyopelekea dua hii kutolewa na kile alichokiongea Askofu Gwajima, May 24, 2025 kuhusu utekaji, utesaji na uuaji kwa upande mmoja na hoja za makundi mbalimbali yanayoendelea kumjibu hotuba yake hiyo kwa upande mwingine. Kuhusu kuwa aliyoyasema Askofu yana merits au hayana merits, hilo ni jambo ambalo nakuombea dua Mwenyezi Mungu afungue macho yako uone mwenyewe uhalisia wake ulivyo. Isipokuwa uniruhusu kufafanua kuwa, wakati akina Tyndale na wafia dini wengine wa Oxford; akiwepo askofu Hugh Latimer, Nicholas Ridley na Thomas Cranmer aliyekuwa Archbishop wa Canterbury; wakichomwa moto wakiwa hai, lilikuwepo kundi kubwa lenye nguvu, ambalo kutokana na kunufaika kwake, lilikuwa likiwachochea wafalme wa Ulaya kutekeleza unyama huu. Wasiwasi ni kuwa, Je, kinachoendelea katika mjadala huu sasa, hakiakisi historia hii hata kama motives zaweza kuwa tofauti?

Andiko hili limejaa hekima tele, natamani mlengwa alione na afunguke macho atoke kizani alipo hivi sasa.

Mimi ni mmoja wapo kati ya waliompenda sana, na kiukweli natamani aache alama isiyo na ukakasi kama kiongozi mwanamke.
 
umekuja vizuri mwanzon ila hapo kiunoni ukanichefua,in short hafai na hana sifa tusibwabwaje maneno.

R.I.P Miamba ya diplomasia mmetuachia kizazi cha hovyo kuwahi kushuhudiwa kwenye international relation arena.
 
Andiko hili limejaa hekima tele, natamani mlengwa alione na afunguke macho atoke kizani alipo hivi sasa.

Mimi ni mmoja wapo kati ya waliompenda sana, na kiukweli natamani aache alama isiyo na ukakasi kama kiongozi mwanamke.
Mtu kasota na kuanzia cheti,kaunga unga mara paaa, prezidaa kanogewa😂😂
 
Ukishakubali kua kiongozi lazima kabisa ukubali kuskia Yale ambayo huwezi kuyapenda Mother kazungukwa na watu wanafiki watupu ndo wanafanya mambo mengine ambayo hawajatumwa wanajifanya wanamsandia kumbe wanamchafua
 
Kwa wasomaji wa historia ya uprotestant watakuwa wanakumbuka dua maarufu; "Lord, open the King of England's eyes" ya William Tyndale, aliyoiomba akiwa anachomwa moto October 1536 kwa kosa la kutafsiri Biblia kwa lugha ya kingereza. Kwa faida ya wasiofahamu, mpaka karne ya 16, dini pekee katika eneo lote la Ulaya ilikuwa ni Ukatoliki, na misa zilikuwa zikiendeshwa kwa lugha ya kilatini (Latini mass), jambo ambalo wanamageuzi wengi wa kiroho hawakuwa wakikubaliana nalo. Kutafsiri Biblia katika lugha ya kiingereza wakati huo ilikuwa ni fundisho potovu (heresy) na adhabu ya mtu heretic ilikuwa nikuchomwa moto hadharani mpaka ufe. Kwa hiyo dua hii ya William Tyndale ilikuwa ikiomba rehema kwa Mwenyezi Mungu, kuyafungua macho ya Mfalme Henry VIII, dhidi ya madhila haya yaliyokuwa yakitekelezwa kwa mkono wake dhidi ya wanamageuzi.

Nimelejea kisa hiki kwasababu kunaweza kuwa na mfanano fulani wa muktadha na hali iliyopelekea dua hii kutolewa na kile alichokiongea Askofu Gwajima, May 24, 2025 kuhusu utekaji, utesaji na uuaji kwa upande mmoja na hoja za makundi mbalimbali yanayoendelea kumjibu hotuba yake hiyo kwa upande mwingine. Kuhusu kuwa aliyoyasema Askofu yana merits au hayana merits, hilo ni jambo ambalo nakuombea dua Mwenyezi Mungu afungue macho yako uone mwenyewe uhalisia wake ulivyo. Isipokuwa uniruhusu kufafanua kuwa, wakati akina Tyndale na wafia dini wengine wa Oxford; akiwepo askofu Hugh Latimer, Nicholas Ridley na Thomas Cranmer aliyekuwa Archbishop wa Canterbury; wakichomwa moto wakiwa hai, lilikuwepo kundi kubwa lenye nguvu, ambalo kutokana na kunufaika kwake, lilikuwa likiwachochea wafalme wa Ulaya kutekeleza unyama huu. Wasiwasi ni kuwa, Je, kinachoendelea katika mjadala huu sasa, hakiakisi historia hii hata kama motives zaweza kuwa tofauti?

Mh Rais, mm ni mwana CCM, ingawa sijashika nyazifa kubwa za juu, kipo kisa naweza kukushirikisha. Mwaka 2013/2014, mm nikiwa mwenyekiti wa CCM shirikisho mkoa wa Kilimanjaro, kuna waziri wa viwanda na biashara(sasa ni marehemu), tukiwa Nyumbani kwa Mchumi wa mkoa, na baadhi ya viongozi chama wakiwepo, alimsema vibaya sana rais Kikwete kwa mambo ambayo hakuwahi kusikika akiyapinga mbele ya kamera za vyombo vya habari. Ingawa haikuchukua muda ailitenguliwa, ila kuna kitu cha kujifunza. Sisemi hivi kumaanisha wasaidizi wako wapo hivi, ila kujaribu kukueleza sisi wana CCM tulivyo. Sio kila anayemjibu Gwajima kwenye hili, tena kwa kauli zinazoleta ukakasi, anasema hivi kukutetea, wengine wanajikosha tu wapate ugali wao, ila pembeni wanaweza kuwa wanakung'ong'a.

Mh. Rais, mie sina mashaka na ushindi wako katika uchaguzi mkuu ujao. Mpaka sasa sijaona chama chochote cha siasa kinachoweza kuwa tishio kwako. Changamoto kubwa kwako wewe uliyonayo ni LEGACY. Baada ya urais wako 2030 utakumbukwaje? Huu ndio ushindi mkubwa, ambao kwa dua zangu, namwomba Mwenyezi Mungu akuwezeshe kuuona. Ukiwa rais, utasikia mengi, wapo wanaojifanya wanakusaidia kumbe, wanatengeneza ukaribu na wewe ili kujisaidia wao. Ni Mwenyezi Mungu tu ndiye anayeweza kukuongoza kuona upendo au ghiriba za watu wanaokuzunga na kung'amua dhahiri zao. Matamanio yetu wengine ni kuona urais wako unakuwa uthibitisho usio na shaka kuwa wanawake ni viongozi bora.

Najua ww ni muislamu, lakini naamini waislamu na wakristo sote tunakubaliana kuhusu nabii au mfalme Suleiman. Ikikupendeza waweza soma 1Wafalme 3:1-15.
Kwa hiyo unataka afanyeje?
 
Mama amezungukwa na watu wenye nia ovu…binafsi namuombea…wanaomshauri wanataka kumuangamiza…Mungu atamlinda….NB : hoja za Mh Gwajima zipate majibu.
 
Back
Top Bottom