Mwenyezi Mungu, twaomba uyafungue macho ya rais wetu

Imenilazimu nicheke kwa uchungu baada ya kusoma mada hii.

Ni kama "usimulizi" wa hadithi ni mzuri, unao mpangilio mzuri; hasa huko kunakohusu habari za kidini.

Mambo yanakuja kubadilika haraka sana inapofikia kwenye maswala ya kisiasa; na hasa baada ya kujitambulisha anakohusika mwandishi wa mada yenyewe.
Anaandika:
Mh. Rais, mie sina mashaka na ushindi wako katika uchaguzi mkuu ujao. Mpaka sasa sijaona chama chochote cha siasa kinachoweza kuwa tishio kwako
Wewe unajitambulisha ni mwanaCCM, tena mwenye elimu ya kiwango hicho unachokionyesha mbele ya jina lako; tueleze "kutokuwa kwako na mashaka..." kunatokana na nini hasa?
Wewe katika maoni yako huoni mihangaiko mikubwa sana iliyopo sasa humu nchini, inayohusisha siasa. Huoni hawa watu wanaopotea, wengine kutekwa na baadhi kupoteza maisha; huna chochote kinachokufanya ujiulize haya yanatokana na nini?
Wewe, Daktari Francis, hustushwi kabisa na hali ya kisiasa inayo ashiria uvunjifu wa amani nchini; kwa sababu tu CCM na viongozi wenu hamtaki, tena kwa maksudi kabisa hata kueleza hamtaki, kwa nini pasiwepo na marekebisho ya mfumo wa uchaguzi kuwezesha uchaguzi huo uwe HURU, na wa HAKI , ili waTanzania waweze kuwachagua viongozi wanaowataka wenyewe? Kama Samia, Mwenyekiti wako anakuamini wewe juu ya "uhakika" ulio nao wewe, kuwa hakuna mshindani wake, tatizo la kufanya marekebisho hayo rahisi inatoka wapi?
Na hawa akina Mtungi, mnaowatumia kuwavuruga CHAMA mnachokiogopa zaidi, ili wamsafishie njia huyu mtu uliye naye imani sana, ni wa kazi gani hawa?
Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA, yupo gerezani kwa mashtaka ya kufikirika, kesi inazungushwa kila mara; hata watu kujitokeza tu kusikiliza kesi inakuwa ni vita; nyinyi watu wa CCM, teana wasomi kama wewe, tena mjuvi mzuri wa historia za kidini, akili zenu zinagota vipi inapofika kwenye chama na viongozi wenu?

Nisiandike zaidi, lakini wewe, pamoja na hao wenzako unaowananga kwenye hiyo mada yako, wote ni wanafiki tu. Sijui unafiki huu unatokana na nini hasa? Wewe mwenyewe umetaja 'uhitaji wa ulaji', ukiwashutumu hao wengine. Mbona na wewe ni kama umo kwenye juhudi zile zile za kutafuta ulaji?
Samia hawezi kushinda uchaguzi wowote ule ulio haki, bila ya matumizi makubwa ya pesa, matumizi ya nguvu na vitisho, na kutumia vyombo vya dola kuvuruga uchaguzi. Huo ndio ukweli wenyewe.

Nakushukuru kwa historia hiyo ya waprotestant. Inanikumbusha matatizo yetu hapa na lugha yetu ya Kiswakili. Kuna watu huwezi kuwashawishi chochote kuwa kuwa na elimu nzuri hakuhitaji kujuwa Kiingereza kingi. Kumbe Waingereza wenyewe tatizo hilo liliwakumba na lugha yao hiyo, ambayo sasa sisi tunaimba kama kasuku, kwa ni muhimu sana ili tuonekane tunajuwa tullicho jifunza mashuleni.

Sikuhakiki chochote. Soma kama ilivyo.
 
Dawa ni Mabadiliko siyo Kubembeleza! Sikio la Kufa huwa halisikii dawa,hata ungeshauri kiasi gani.
Kwa CCM, hili la "kutobembeleza" sasa haliepukiki. Utatumia bembeleza ya namna gani hawa watu wabadili nyoyo zao?
 
Kitendo cha kukubali kua na machawa badala yakuwakemea nakuwakataa ndio imezalisha haya tunayoyaona nivigumu sana kukubali ila ndio ukweli
 
Kwa CCM, hili la "kutobembeleza" sasa haliepukiki. Utatumia bembeleza ya namna gani hawa watu wabadili nyoyo zao?
Ni kumwomba Mungu atusaidie kuung'oa huu utawala kama alivyofanya kwa Farao wa Misri na Nebukadreza wa Babeli!
Hayo ndiyo maombi mazuri!
 
Najua ww ni muislamu, lakini naamini waislamu na wakristo sote tunakubaliana kuhusu nabii au mfalme Suleiman. Ikikupendeza waweza soma 1Wafalme 3:1-15.
Umezunguka saaaana sana, sema straight forward kuwa Mambo hayako kama yanavyoelezwa na CHAWA. Rais asikubali kudanganywa na CHAWA
 
Ahsante kwa mchango mzuri, mawazo tofauti tofauti ni muhimu kwa ustawi wa nchi yetu.

Nataka niweke msimamo wangu wazi, kama ambavyo nimekuwa nikiandika mara zote, sikubaliani na vitendo vyovyote vya uvunjifu wa haki za binadamu! Kuvunja haki za binadamu siyo sera ya CCM, na mwana CCM yoyote anayevishabikia, bila kujali nafasi yake kwenye chama na serikali, ni wazi amepotoka.

Kuhusu CCM kuwa na uwezo wa kushinda uchaguzi sidhani kama ni jambo linalohitaji tathmini ya hesabu ngumu za actuarial, hilo lipo wazi na namba zinaongea. CCM haihitaji kucheza rafu kupambana na CHADEMA, na kwakweli lingekuwa ndani ya uwezo wangu, ningewahakikishia wapinzani haki yao ya kufanya siasa ili kupunguza manukuniko kila uchaguzi unapomalika
 
Ni kumwomba Mungu atusaidie kuung'oa huu utawala kama alivyofanya kwa Farao wa Misri na Nebukadreza wa Babeli!
Hayo ndiyo maombi mazuri!
Ni kumwomba Mungu atusaidie kuung'oa huu utawala kama alivyofanya kwa Farao wa Misri na Nebukadreza wa Babeli!
Hayo ndiyo maombi mazuri!
CCM; na hasa Genge la Samia wanapenda sana mawazo ya aina hii. Samia angejuwa mahali ulipo, angekujazia kibubu ili ueneze kwa kasi fikra za namna hii kwa waTanzania wote.
 
Naheshimu sana fikra za aina hii. Laiti kama zingechangia hata kwa chembe ndogo tu kuepusha hayo yanayofanyika ndani ya chama hicho, kwa jina la chama. Hii ni 'tragedy', inayo umiza wengi, hata wasiokuwemo ndani ya chama hicho; kujuwa kwamba chama kinanajisiwa na kundi la watu wachache, lakini walio wengi wasiopendezwa na hali hiyo, nao wanaonekana kuwa mateka, kama waTanzania wengine wote tulioko nje ya chama hicho.

Mkuu Dr. Francis', labda ingesaidia kidogo kwa wewe unayeipenda CCM inayotumiwa na waovu wachache ndani ya chama, ni kipi hasa kinacho kufanya uendelee kukipenda chama hicho katika hali yake mbovu kama ilivyo sasa?
Mbaya zaidi, kwa nini nyinyi watu mnaoipenda CCM nzuri, inakuwaje hamna lolote la kupinga matendo maovu huko huko ndani ya chama chenu. Mnaogopa kupoteza maslahi?
Hapa sioni huo u-Dactari ukiutumia kujibu hoja iliyopo mezani.
Kama "CCM haihitaji kucheza rafu kupambana na CHADEMA", woga huu mkubwa walio nao viongozi wako ni wa nini?
Hawa viongozi wenu wameamua tu kuvuruga nchi bila ya kuwa na sababu?

Kwa muundo wake ulivyo, na kwa historia ndefu na nzuri iliyokuwa imejijengea, nami ningeungana nawe katika kudai kuwa CCM hawahitaji kufanya rafu ili wabaki kwenye madaraka. Lakini usijifanye kusahau kwamba CCM hiyo ya kihistoria, bado ni hii hii iliyopo sasa.

Viongozi wenu wameichukuwa CCM na kuikoroga, lakini nyinyi mnabaki na historia nzuri tu ya chama kama kumbukumbu yenu ya kudumu.

Ngoja nirudie tena: Katika uchaguzi ulio WAZI, na wa HAKI, Samia hawezi kushinda nafasi hiyo ya Urais (kama ulivyoeleza huko mwanzo, na sasa ukabadilisha kuwa CCM).
CCM kama chama kinaweza kushinda viti vingi; kwa sababu tu ya muundo wake ulivyo, na kwa baadhi ya wananchi kuwa na kumbukumbu nzuri ya kihistoria ya chama hicho; na kwa CHADEMA kukosa wagombea wenye sifa za ushawishi wa kutosha kwa wananchi.
Ndiyo sababu kila mara mnawavuruga vyama vya upinzani visiweze kujiimarisha huko mitaani na kwenye majimbo.
 
Kimsingi hoja yako ina mashiko, haswa katika kubainisha mapungufu yaliyoko. Mapungufu katika taasisi yoyote yapo, CCM ikiwa ni kadhalika. CCM imekuwa na utamaduni wa kujisahihisha kila mara inapopita kwenye machafuko. Azimio la Arusha na Kujivua gamba ni mifano michache. Zaidi ya utamaduni huu, kasoro za CCM mara nyingi zimekuwa na sura ya utendaji na watendaji kuliko kuwa za kimfumo. Hii maana yake ni kwamba zinarekebishika. Haya yanayolalamikiwa sasa, chimbuko lake ni UCHAWA, huu ni msukosuko ambao haisumbui tu CCM, bali nchi yetu yote kwa ujumla wake. Ninaimani nalo litapita.

Mwisho angalau tunakubaliana kwenye mambo matatu: historia iliyotukuka ya CCM, umadhubuti wake kama taasisi imara ya kisiasa na utajiri wa wanachama wanaokiunga mkono kila kona ya nchi yetu. Haya mambo matatu yanaihakikishia CCM mtaji wa ushindi.
 
Mungu anawezaje kuyafungua macho ya mungu mpya?
 
Mene mene tekel upharsin" is a phrase from the Book of Daniel, chapter 5, in the Bible. It refers to the mysterious handwriting that appeared on the wall during a feast given by King Belshazzar. The phrase means: "Mene: God has numbered your kingdom and brought it to an end; Tekel: You have been weighed and found wanting; Upharsin: Your kingdom is divided and given to the Medes and Persians".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…