Mwenza wangu anasumbuliwa na kutoka damu kipindi cha ujauzito

kocha Nabi

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2022
Posts
709
Reaction score
1,881
Habari wakuu,

Tupo tunalea mimba ina week 8 now, but tangu week ya 4 mwenza amekuwa akipata shida ya kutokwa vitone vya damu ukeni.

Inaweza chukua siku mbili isitoke lakini siku ya 3 ikatoka kitone kidogo sana kama mtu aliyegusisha pamba ya masikioni kwenye nguo ya ndani.

Tatizo lilipoanza tulienda hospital ikiwa ni week ya 5 dactari akapima akasema mimba ipo salama ila kuna threateaning factors za kupelekea abortion na kuna dawa alipewa atumie inaitwa salbutamol kama sijakosea.

Lakini shida bado ipo pale pale haipiti siku 2 kitone kinajitokeza na ni kidogo mno.

Msaada wenu wakuu mwenye kufaham lolote.
 
Mpeleke kwa Dr mwingine bingwa wa wanawake mtapewa dawa ya kuzuia hiyo threatening abortion inaitwa duphaston. Mkipewa atumie kikamilifu, pia asifanye kazi za kuinama mara kwa mara au kunyanyua vitu vizito, apate muda mwingi wa kupumzika.

Msifanye sex kwa sasa hadi hali iwe shwari
 
shukrani mkuu ngoja nifatilie kwa daktari mwingine.
 

Zingatia ushauri wa mkuu hapa,kutoka damu hata tone moja sio salama kabisa kwa mjamzito
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…