Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Umewaacha wengi kapa kwa ssbabu wamezoea kutafuniwa kila kituIgweeeeeeeee! Tetesi ni kwamba wa Tanzania tujiandae Kisaikolojia na kama vile wahenga walivyo wahi sema "Ukiona mwenzako ananyolewa basi wewe zako tia maji".
Ndugu za wa Tz hapo nchi jirani pametokea jambo lakushangaza kidogo. Jambo ambalo kama ukiliangalia kwa jicho la tatu huwezi kusita kusema na mimi yanipasa kujianda kama Mtanzania. Kuna mambo yaweza kuwa yakawaida ila Kuna mambo yaweza kuwa sio yakawaida ktk Taifa na hatupaswi kufunga macho nakuimba mapambio wakati mambo sivyo kama yalivyo.
Samahani sitaki kumtaja jina ila kwa mara ya kwanza nimesikia kiongozi mmoja mkubwa mstaafu alikisema tumuombe Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tz. Mimi moyoni nikasema Mh! Nimasikio yangu au naota? Well nikasema Sina cha kushangaa ila najuwa yalishasemwa na wenye macho yakuona mbele ya Taifa hili ila wakakejeliwa na kwabusara zao wakasema endeleeni kiufupi hawa ni miamba isio tikisika wala kutafuta peleka bakuli ikulu kuomba msaada either kwa watoto wao au familia zao. Nembo yao ni Jamuhuri , dam yao ni Jamuhuri chakula chao ni Jamuhuri na malazi yao ni Jamuhuri.
Kuna watu wapo usingizi wa pono ila huko vijijini wameuza mpaka na makopa ya mihogo na mtama Yani hamna kitu. Mtu mmoja kwa tambwe kubwa amelifikisha Taifa kwenye mahali hakuna wakusema neno ila nikilio tu. Unauza chakula cha familia kwa jirani tena kwa bei ndogo alafu unaenda kukinunua kwa Dola mbali zaidi then unakuja kukiuza kwa bei ya chini ili watu wako wasife njaa. Halafu mtu bado ako ofisini anajiona Genius. Serikali ipo Rais yupo, bunge lipo na usalama wapo sawa nisiandike sana.
Mataifa ya jirani wana njaa, hawana ukwasi kwenye serikali zao, na watu hawana nguvu yakununua kiasi Taifa moja hata magari watu wameshindwa kununua jambo limefanya wanunuzi kutekeleza magari bandarini. Sio hilo tu maisha yamepanda kiasi hata mishahara serikali ameshindwa kulipa kwa miezi mitatu na sio hivyo tu serikali imesema ikiona vipi watapunguza watumishi.
Tofauti na nchi yakusadikika data sio Mali ya wananchi wala hakuna jicho la tatu kuangalia ukwasi na Mali ya wana kusadikika kutokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wa wana kusadikika hakuna jicho la tatu ktk chungu hivyo alikwambia anapesa wewe unakubali mwanakusafikia lakini ikumbukwe uchumi sio siasa na kamwe haiwezi kuwa siasa ila siasa nzuri zinaendana na uchumi mzuri japo siasa chafu huwaribu uchumi.
Wanakusadikika msifikirasifikiri kile kimetokea nyumba ya jirani hakitowakuta nidhahiri shahiri kujianda tena kujiandaa sasa sio kesho.
Tetesi zinaonyesha Hilo Taifa lakusadikika ndio linalofwata wala hupaswi kubeza maneno haya. Najuwa wanakusadikika macho yao yapo mei mosi japo uwenda nyota wakusadikika asiwepo kwenye hizo sherehe nakutuma mwakilishi Tetesi zinasema kwamba wanakusadikika wanasubiri kwa ham kuongezewa mishahara ila ukweli nikwamba uwenda naomba msininukuu uwenda Hilo lisiwepo kutokana na sababu siwezi ziandika hapa kutokana bado hazijakuwa wazi ktk Tetesi hizi.
Wanakusadikika wanashauriwa nilazima wajiandae Kisaikolojia kama wenzao nchi ya jirani tena wao kilio Chao kitakuwa cha ndani kwa ndani maana hakuna chombo kitarusha Habari ya ndani yakusadikika kama vile hakuna chombo kinajua Habari ya chungu.
Tetesi zinasema kwamba wanakusadikika wajiandae kwa kuweka vyakula na kupunguza matumizi yasio ya lazima. Wanakusadikika wanashauriwa kusikiliza Vyombo vya Habari na kufungua akaunti kwa wingi jamiiforums maana jogoo atakapo wika mara ya kwanza mpaka ya tatu taarifa hiyo itavuja kwa mara ya kwanza kwenye mtandao wa jamiiforums.
Mwisho wanakusadikika wanashauriwa kuto sadiki kila kitu na akili yakuambiwa wachanganye na za kwao.😭🙏🙏🙏📜✉️📨🤐🤐🤐
Natunza andiko hili