Mwenzenu nimeachwa kweli!

Mwenzenu nimeachwa kweli!

Itahesabika kuwa ni talaka endapo kuwa imehakikishwa kweli hiyo sms imetoka na imeandikwa na mumeo na kama kweli amemaanisha kuwa ni talaka.

Matendo yote yanaswihi kwa nia.Ikiwa amemaanisha kuwa ni talaka basi ni talaka kweli. Unatakiwa ukae 'iddah na anauwezo wa kukurejea muda wowote ndani ya kipindi hicho cha iddah ama ikiwa amekuacha mpaka kipindi cha iddah kupita basi anatakiwa aje tena mfunge mkataba upya wa ndoa.

And Allah knows best
 
Tayari anadai hajamaanisha.
 
Amefanyaje kosa la kiufundi atakuja kujutia muda si mrefu...

Sasa Kama kaniacha nimng'ang'anie Ili isiwe kosa la kiufundi? Mwisho aniue mpate headlines?
Mwanaume kapewa maamuzi ya mwisho na kaamua hivo, au kosa langu ni kuwa ok na maamuzi yake?
 
Tayari anadai hajamaanisha.
Amche ALLAH na aache utani katika masuala ambayo hayana utani. Mtume Muhammad pbuh amesema kuwa kuna mambo matatu huwa umakini wake ni umakini na mzaha wake ni umakini, la kwanza ni "Ndoa, la pili ni Talaka na la tatu ni Kumrejea mke"

~Abu dawood

Talaka huwa haina mzaha , inapotamkwa huwa imetamkwa hata kama umeifanyia mzaha.
 
Ingia mtaani upambane

Uzuri Nina kibarua maisha yatasonga, kuhusu kupambana mwenyewe hainipi shida, kuna kipindi alipata Kazi mkoa mwingine alinipotezea mazima, sikuyumba sikulalamika, akarudi akanikuta.
 
Mwenyewe natamani iwe kweli, Ila tatizo kashaanza kunibembeleza anasema hajamaanisha....hajaniacha.
Ndo Naomba ushauri jamani hiyo si ni red card kabisa? Mwenyewe nataka kusepa mazima, kanichosha
Kama umeshamchoka na unataka kujivua kutoka kwenye ndoa unaweza kuomba khula,(kujivua kutoka katika ndoa) kwa kurejesha mahari aliyokupatia wakati wa kufunga ndoa au mkubaliane kuwa utamlipa kiasi gani iwe ni kikubwa au kidogo ili ujivue kutoka katika ndoa.

Uislam ni mwepesi sana ,haujatia uzito katika masuala ya ndoa. Nenda kwa ofisi ya Kadhi then eleza kuwa unahitaji khul' ili ujivue kutoka kwa mumeo then ataitwa , mtakubaliana either urudishe mahari aliyokupatia au kiasi chochote cha fedha ili akuache huru uendelee na maisha yako na yeye aendelee na maisha yake.

Kwenye Uislam ndoa sio GEREZA.
 
Habari za jioni!

Jamani mwenzenu jana nimezinguana na Baba watoto, katika purukushani nikamwambia niachee nitikise kibiriti....akanijibu subiri, sijakaa vizuri imeingia sms "Mimi Baba kidogoli nimekuacha Mamy K talaka 1, sio mke wangu"

Yani hapa nipo nipo sijui nilie, sijui nicheke, nahisi kisukari si kisukari, covid si covid....!

Wanazuoni njooni mnishauri hiyo si talaka tayari? Hivi kweli mkeo unayempenda akikwambia niache unamwambia hivo, kuna mapenzi hapo?

Nipeni ushauri manake kesho anarudi nyumbani najua ataanza kunibembeleza na kunambia hakuwa anamaanisha, kuna mapenzi hapa?
Sijaelewa hata huenda uliyeandika hujaelewa unachokiandika

Yaani akuache halafu akubembeleze si ndio talaka itakuwa haifanyi kazi!

Na hata akiwa amekuacha unapaswa kuhesabu EDA ukiwa nyumbani kwako na akuhudumie ndio sheria inavyosema..

Naweza kusema masharti ya takaka ni magumu kuliko watu wanavyofikiria.
 
Uzuri Nina kibarua maisha yatasonga, kuhusu kupambana mwenyewe hainipi shida, kuna kipindi alipata Kazi mkoa mwingine alinipotezea mazima, sikuyumba sikulalamika, akarudi akanikuta.
Hii mindset itakugharimu sana mbele ya Safari.,,,hio Fikra ndani yake huwa inakuwa imebeba Kiburi, Dharau, Ujeuri, Ujuaji na Upumbavu mwingi..

Change Or Perish.
 
Back
Top Bottom