Pre GE2025 Mwezi mmoja baada ya uchaguzi, Mbowe yuko kimya lakini CHADEMA wanakanyagana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbowe anahusikaje hapo sasa?? Kwani wanachama wengine kama Mchome hawana akili na haki ya kuhoji?

Hivi Tundu Lissu anaposema "No Reforms, No Elections", bado hamjatambua kuwa yeye ndiye adui namba 1 wa CHADEMA?

Hakika CHADEMA mumeingia choo cha kike, na hamtoki kwenye hicho choo hadi mgawane matofali na mbao
 
Kauli ya No Reforms No Election haikuasisiwa na Lissu, ni Mbowe ndiye muasisi na ikapitishwa na Baraza kuu na hatimaye na Mkutano Mkuu wa Chama, hivyo hiyo si kauli ya Lissu bali ni kauli na msimamo wa Chama.
 
Barua inasema uchaguzi wa wateule hauna uhalali kwa sababu akidi haikutimia. Mchome amesema wazi kuwa hana tatizo na uteuzi bali anataka taratibu zifuatwe. Mbona majibu yake ni mepesi? Anaweza kujibiwa:
1. Akidi ilitimia na majina ya wajumbe halali waliohudhuria ni haya hapa.
2. Alikosea hesabu. Hiyo akidi anayodai haihusiki na uchaguzi huu.
3. Tuliteleza. Tutaita kikao kingine ili takwa hilo litimizwe. Bila shaka wale wale watashinda.

Mchome amewafanyia favour sana maana angeweza kungoja mpaka karibu na uchaguzi na kuliibua.

CDM wasisahau kuwa hukumu kuhusu wakina Halima ilisema kuwa ingawa walikuwa na haki ya kuwafukuza walikosea kwenye taratibu. Wanatakiwa kuwa waangalifu zaidi katika kufanya mambo yao.

Amandla...
 
Hii kaandika kweli Rehema? Mbona anakuwa kama Msigwa? Uchaguzi wameshinda. Wajikite katika kukijenga chama chao waachane na Mbowe. Wajibu tuhuma zilizomo wasonge mbele. Sio kila mtu anaye kuhoji ni adui yako. Kama ni yeye kweli, huku ndio kuponya majeraha ya uchaguzi? Kwanza kumsingizia Aidan halafu sasa Mbowe. Adui yenu mnamjua na sio Mbowe.

Amandla...
 
Nilikuwa nakuona una akili kumbe huna tofauti na Tlaatlaah au Lucas Mwashambwa. Sasa kushinda kwa hila kivp wakati uchaguzi ulikuwa live kabisa
 
wataalamu katika siasa tuliliona hili mapema na tukatahadharisha kabisaa ili isiwe surprise kwamba kwa aina ya kampeni walizofanya chadema hususan uchaguzi wa mwenekiti wa Taifa,

Yeyote atakaeshinda uchaguzi huo ategemee kuhujumiwa na upande utakaoshindwa uchaguzi huo.

Na huo ni mwanzo tu,
bado kukomoana wakati wa uteuzi, na huenda pakawa na kupotezana kabisaa katika zoezi hilo kuelekea uchaguzi mkuu.

Hali hiyo itaendelea kuizonga chadema kwa miaka yote mitano ijayo πŸ’
 
Kauli ya No Reforms No Election haikuasisiwa na Lissu, ni Mbowe ndiye muasisi na ikapitishwa na Baraza kuu na hatimaye na Mkutano Mkuu wa Chama, hivyo hiyo si kauli ya Lissu bali ni kauli na msimamo wa Chama.
Hata kama kauli ni ya Mbowe na mkutano mkuu ukai broadcast, lakini tambua hatukuijua kauli hiyo kabla ya Tundu Lissu hajaiongelea kwenye mkutano wake wa kwanza rasmi na wanahabari.

Kwani yeye hana akili zake kama Mwenyekiti kuanza na kauli yake mpya isiyo na utata?? Mchawi wa CHADEMA ni Tundu Lissu tu
 
Wewe mwenye akili kuliko mtoa mada mbona hujajibu hoja?? Acha woga na matusi
Yaweza kuwa nimeandika matusi bila mimi kujua nikidhani niko sawa. Naomba ndugu uniambie wapi au neno gani ni tusi ili nisije rudia tena hili jambo
 
Utasubiri sana na roho yako ya kichawi
 
Lissu anasimamia azimio la Mkutano mkuu. Hili nalo ni gumu kuelewa?
 
Amendika Rehema kweli, kafungue ile twitter account ambayo nimeambatisha pale kwenye post #1
 
Jipangeni, mlijua siasa ni maneno maneno eeh ?
Wameanza kukwama na kushindwa kuendelea kujenga Chama. Sasa wanatafuta scapegoat na kama kawaida baada ya kumtukana na kumdhalilisha Mwamba Mbowe wanashindwa kuwajibika.Walidhani kuongoza Chama ni kelele za mitandaoni na ngebe za kujipatia umaarufu.Reality has checked in. Deal with it.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…