Mwezi sasa hatuna Waziri wa Ulinzi

Mwezi sasa hatuna Waziri wa Ulinzi

Auto pilot government. Rais hayupo kitini yuko ziara ndefu ya mambo ya utalii. Jana alikuwa jimboni kwa Mh Mbowe pengine ki mkakati zaidi. Makamu wa Rais hajaweza ku prove uwepo wake kwenye hiyo nafasi. Hasikiki. Amekuwa non starter kind of. Waziri mkuu anajiandaa kuwa Rais siku moja. Smart Gwajiboy ameigawa CCM. Anawatisha wenzie ikijulikana kwamba Sukuma gang wenzie wana watch carefully. Kuna wazo ama Waziri wa Ulinzi atoke Zanzibar (kwa kuwa Waziri wa mambo ya Nje ni kutoka Bara). Akitoka bara atoke Sukuma gang tena au kanda nyingine na je akitoka kanda nyingine ataweza kufanya kazi na incumbent CDF? Mambo ni mengi na muda ni mchache. Tuendelee kuiombea nchi yetu.
 
Je, nchi inaendaje? Kwa sasa maana ni mwezi sasa hatuna Waziri wa Ulinzi tangu Kwandikwa Atutoke.

Wataalamu wa mambo mnaweza shea chochote kwenye hili.
Na una uhakika kuwa hatuna mtu anayefanya kazi badala yake? Umesikiliza Bunge linaloendelea? Kama umesikiliza, maswali ya Wizara ya Ulinzi yanajibiwa na nani Bungeni? Tumpeni mama nafasi afanye kazi kwa utaratibu na kwa namna hekima yake inavyomtuma
MASHANJARA
 
Bora atuchagulie Waziri wa Ulinzi kutoka Zanzibar ,tunamkumbuka Salumu Ahamedi Salumu ,yule jamaa vyombo vilimkubali sana sana,kuna watu wanabahatika aisee,ccm wakampiga na chini hakuja juu mpaka leo ,masikini kina Bashiru na Polepole ,hivi wanalijua hili na wengine mnalijua hili ,CCM mwenzako akikupiga na chini basi ni bahati sana kuja juu tunamuona Makonda.
dawa ni Katiba mpya na Tume mpya hata CCM mtakuwa salama.
 
Hana umuhimu ngoja tudemke kwanza na sinema zetu tukimaliza tutarudi sawasawaaaaa?
 
Umebainisha incompetence nyingine ya Rais Samia ambayo tulikuwa hatujaigundua.
 
Ni muda umepita tangu tuondokewe na Waziri wa Ulinzi ndugu Kwandikwa. Ni kwanini imechukua muda mrefu kuteua mrithi wake?
 
Ukiona muda umepita sana ujue mabadiliko yatakuwa na wizara nyingine
 
Muache mama atengeneze filamu kwanza. Ni muhimu zaidi ya uteuzi wa waziri.
Mama anatupeleka Hollywood. Soon atakuwa kama kina Angelina Jolie.

Utani utani mara tunaona mama yupo kwenye Movie ya James Bond kama Queen wa England, ukizingatia kafanya Royal Tour tayari. Sasa huoni hapo ni muhimu kuliko swala lingine lolote ikiwemo uteuzi wa waziri.
Magu alitupeleka uchumi wa kati mama anatupeleka Hollywwod. Mdogo mdogo mpaka Mars tutafika.
 
Mara ya mwisho kuwa na Mkuu wa Majeshi na Waziri wa Ulinzi kutokea Zanzibar ilikuwa lini?
 
Back
Top Bottom