KERO Mwezi ujao mwaka unakamilika toka ahadi ya serikali kujenga barabara ya kibada Mwasonga kwa lami

KERO Mwezi ujao mwaka unakamilika toka ahadi ya serikali kujenga barabara ya kibada Mwasonga kwa lami

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Madaraja ya wapi hayo? Sisi ndio watumiaji wa barabara hii kibada mwasonga mpaka tundwi kila siku tunapita hapa hebu waambie watanzania daraja gani linajengwa mwaka mzima??
Wewe tayari una yako.....basi sie tunaishi kisarawe II ya Lubumbashi tunaona ujenzi unaendelea hio ya kwenu inawezekana kweli hakuna ujenzi kapate chemicola kwa mangi
 
Mi nilimsikia kada wa ccm kwenye ngenga za siasa anasema wameshajenga kwa lami hadi mwasonga juzi tu....hawa watu waongo sana.....hadi leo hiyo barabara wameishia kuichonga nakuweka makalavati tu.....SIASA ZAO MAJITAKA WANATAFUTA ATTENTION YAKUPIGIWA KURA
 
Barabara sahivi imefikia 30% na tar 25 April 2025 Raisi mwinyi alizindua jiwe la msingi la barabara ya lami Kibada-Mwasonga-Tundwi-Kimbiji km41 ambayo makadirio yake ni kukamilika 31 December 2025 kama una kiwanja huko usikimbilie kukiuza kwanza au kama huna unaweza kwenda kununua kiwanja huko. Tazama hizo picha hapo.
 

Attachments

  • IMG-20250503-WA0355.jpg
    IMG-20250503-WA0355.jpg
    161.7 KB · Views: 30
  • Screenshot_20250502_210118_YouTube.jpg
    Screenshot_20250502_210118_YouTube.jpg
    223.4 KB · Views: 31
Barabara sahivi imefikia 30% na tar 25 April 2025 Raisi mwinyi alizindua jiwe la msingi la barabara ya lami Kibada-Mwasonga-Tundwi-Kimbiji km41 ambayo makadirio yake ni kukamilika 31 December 2025 kama una kiwanja huko usikimbilie kukiuza kwanza au kama huna unaweza kwenda kununua kiwanja huko. Tazama hizo picha hapo.
Jamaa ulikuja hapa kutetea kuwa mpaka December barabara hiyo itakuwa imekamilika vipi tunaingia
Barabara sahivi imefikia 30% na tar 25 April 2025 Raisi mwinyi alizindua jiwe la msingi la barabara ya lami Kibada-Mwasonga-Tundwi-Kimbiji km41 ambayo makadirio yake ni kukamilika 31 December 2025 kama una kiwanja huko usikimbilie kukiuza kwanza au kama huna unaweza kwenda kununua kiwanja huko. Tazama hizo picha hapo.
ndugu yetu vipi tunaende mwezi September je kuna kipande chochote cha lami kimewekwa mpaka leo?? Au tusubiri kampeni zianze? Au tusiulize sana 😂😂😂😂
 
Ukienda kusikiliza kwa umakini ile siku ya uzinduzi wa jiwe la msingi, waliweka wazi kuwa mkandarasi aliomba aongezewe mda mpaka mwezi May 2026. Na kiuhalisia mpaka sahivi kuna hatua kubwa sana wameifikia japo sizani kama wataweza kumaliza ndani ya huo mda.

Kitu kikubwa ni kuwa tayari kuna hatua kubwa wanazifanya kadri mda unavozidi. Sahivi sehemu zote zilizokua sumbufu fro Kibada-Mwasonga wameweka makaravati/daraja na wameshasonga mbele zaidi kuitafuta Tundwi. Lile daraja kubwa pale mto Nguva tayari lionaonekana lipo zaidi ya 95% kukamilika na limejengwa kwa viwango vya juu sana kimwonekano, pale hata ije mvua ya namna gari uhakika wa safari upo.

Mimi mpaka nimeamua kuhamia kule ni kwasababu nimeona mabadiliko, na sahivi wanajenga mitaro tena mikubwa tu. Zoezi la kumwaga lami huwa halichukui mda mrefu, kinachochukua mda mwingi ni maandalizi ya ile barabara kuweka layers za udongo na kushindilia kuifanya iwe imara zaidi.

Kiufupi ni kuwa kama mtu hujaenda kule utakua unajenga picha ya ovyo sana, lakini sisi tunaopita kila siku tayari tunaona hatua kubwa zikifanyika na sahivi ndo wanakimbizana na mda, wanafanya kazi j3 mpaka j.mos, ukipita asubuhi saa 1 unakuta vijana wapo site wanakimbiza tu.

Acheni kupotosha umma bhana.
 
Serekali yenywe haina hela TANROADS Kuna hali mbaya sana hata magari tu kuweka mafuta ni kipengele, Wakandarasi tunakwenda mwaka pili Sasa no money
Inasikitisha sana
 
Back
Top Bottom