Mwezi ujao napata milioni 30. Naomba ushauri namna ya kuzitumia

Mwezi ujao napata milioni 30. Naomba ushauri namna ya kuzitumia

Bodaboda moja ni sh ngapi mzee baba???
Boxer ni 3,300,000. Akiwa makini anatoboa. Nina mfano hai wa mtu anajishughulisha na hii kitu kwa ukubwa. Yeye huwa anachukua boda hata 10 kwa pamoja na yuko wealth kinoma. Ila shida ni bandidu hatari.
Kumpeleka boda polisi akizingua jambo jepesi kwake.
Ameni inspire japo mimi nimeishia na boda 4.
Nimemuachia wife apambane nao. Si haba maisha yanaenda. Japo kuzinguana kumo sometimes.
"Ukiwachekea watakuchekea, ukiwakazia watakaza".
 
Nunua bodaboda 10 uwape vijana wakuchumie hela, boda moja kwa siku 12,000 tzs kumi ni 120,000.
Kwa mwezi ni 3,600,000 tzs. Yaani utakua na uwezo wa kuongeza boda mpya kila mwezi mpaka uwezo wako wa kuzi control utakaposhindwa.
Mshikaji wangu aliingia kwenye hii biashara ila haikumpa faida kama hesabu za makaratasi zinavyosema , yeye aliweka Elfu nane kwa siku lakini bado ikawa changamoto kwa baadhi ya madereva , hii biashara kuna maeneo yake sio yote na uoate watu waaminifu na hapo ndio kasheshe
 
Kwenye 30 chukua kwanzia 22 mpka 25 nenda kahama bukoba au moshi sema kwa kilmanjaro inabid ue na akil nying nunua Fusso tiper kaiingize garage cheza nayo ingia mtaani mwaka mmoja unanunua tipa yako nyingne
 
Habari, mwezi ujao naenda kupata milioni 30. Vijana wenzangu naombeni ushauri ili nisije kujuta baadae maana hela sasa hivi sina. Na hiyo hela sidhani kama nitaipata tena kama.

Naombeni ushauri kama ungekuwa wewe ungefanyaje.

Nina mke na watoto 3
Uzi wako umechangia wengi kupata ideas za nini cha kufanya wakipata fedha mbeleni. Pokea maua yako.
 
Habari, mwezi ujao naenda kupata milioni 30. Vijana wenzangu naombeni ushauri ili nisije kujuta baadae maana hela sasa hivi sina. Na hiyo hela sidhani kama nitaipata tena kama.

Naombeni ushauri kama ungekuwa wewe ungefanyaje.

Nina mke na watoto 3
Hiyo itupie aviator ikienda x3 tu, una 90M ndani ya sekunde tu, nankuna wakati inaenda hadi x700 sasa hapo zidisha 700 x 30,000,000 🤣🤣🤣 ........ni vip kama ikiwa kweli!
 
Back
Top Bottom