Mwezi ujao napata milioni 30. Naomba ushauri namna ya kuzitumia

Mwezi ujao napata milioni 30. Naomba ushauri namna ya kuzitumia

Mkuu,Milioni 30 ni 10,000 USD.Ni pesa nzuri. Unapofikira ufanye nini na Pesa Jiulize Umeipataje?Sasa Hivi unajishughulisha na nini?Kipato chako kwa sasa ni kiasi gani?Gharama zako za maisha kwa wastani ni kiasi gani?Malengo yako ya muda mfupi na mrefu ni yapi(Ya kifedha).

Ukishajibu hayo Maswali kwa Ufasaha basi tazama furs mahali ulipo Au Jiulize Uwezo wako wa Kurisk ni mkubwa kiasi gani.Zingatia kwamba Katika Biashara unakuwa unachukua RISK hivyo ni muhimu uzingatie kwamba kuna Kupata au hata Kupoteza.
 
Kwa kuwa bado huna wazo la biashara,ili usipoteze pesa nunua bajaji 3 ziweke barabarani,kila siku utapata 60,000@30=1,800,000 baada ya Mwaka na nusu utapata 30M yako na bajaji ju-hii risk ni ndogo .Kwa muda huo wote utakuwa umisha pata wazo la biashara ya kufanya.
Biashara za jamii forums (pdf) . Baada ya wiki, ukitoa na kujumlisha, baada ya mwaka milioni 20, [emoji23]
 
I'm not here to prove a point to you or anybody else. Sitafuti mshirika, ndio nlianza kwa kusema "Ningekua namfahamu" . Kutomfahamu tayari kunamtoa nje ya ushauri wangu lkn Bado namuonea huruma kwasabb ya biashara kicha ambazo nlisema ziko saturated ( Yaani Kila mtu anafanya) ambazo anashauliwa kufanya, kupoteza mtaji wake ni rahisi kwa asilimia zaidi ya 70. So ndugu yangu usiwe na hofu mm sitafuti mshirika kwa nataka nimtapeli, aongee na matajir ambao Yuko karibu nao labda wasipokua wachoyo watampa connection.
Kaka MKUBWA acha utapeli , hizi janja janja za kizamani
 
Sema hatufamiani hizo biashara zote ziko saturated lkn hata UTT faida ni kdogo, Ningekua nakufahamu ningekuelekeza namna ya kuwekeza hiyo Pesa yako na kupata 1% Kila siku kwanzia jumatatu Hadi ijuma, kwa maana unapata laki tatu Kila cku kwa mwaka mzima, kwa maana hiyo unarudisha mtaji wako ndani ya miezi mitano na unaanza kupata faida Hadi mwaka uishe.
Sitaki mtu anifuate PM kutaka kujua hii ni biashara gani, tunafanya na watu ambao tunafamiana nao.
#No malice to anybody
Kama unafanya na watu mnaofahamiana tu na hutaki kufatwa PM taarifa hapa umeileta ya kazi gani?
 
Tia millioni 20 mpe yanga anashinda mechi yake dhidi ya kaizer chief tarehe 27 Odd 2 million 40 hii hapa On zee pocket 😁😂😂

5 unakula bata binafsi

5unakula bata shirikishi na mpenzi wako (waifu)

2 unawalisha bata watoto

Kwenye ile 20 million ya faida inabaki millioni nane

5 unaenda kuweka heshima ukweni

3 unaweka heshima kwenu

Inabaki 20 million exactly sasa hapo unakua umejiweka sawa exactly kiemoshono, kifiziko bila kusahau kibayolojiko hata maamuzi ya hiyo 30 million yatakua sahihi na baraka za ukweni utakua unazo
Kila unachogusa ni big yess😂😂😂

😂
Najua unajua kwanini sijasema uweke 30 million
😂
Tusije kukuta mtu kajinyonga
Ukapanda cheo kutoka jf expert member mpaka kwenye RIP
Yani we jamaa umesababisha mwenzio nacheka barabarani 🙌🙌🙌😂😂😂
 
Nunua bodaboda 10 uwape vijana wakuchumie hela, boda moja kwa siku 12,000 tzs kumi ni 120,000.
Kwa mwezi ni 3,600,000 tzs. Yaani utakua na uwezo wa kuongeza boda mpya kila mwezi mpaka uwezo wako wa kuzi control utakaposhindwa.
Bodaboda moja ni sh ngapi mzee baba???
 
Unitafute nikuuzie shamba zuri kigamboni mwasonga karibu na stend ...uje na 12m heka 2
 
Kwanza ungesema hiyo milioni 30 umeipata kupitia source gani either biashara,mirathi, au kuna asset umeuza ndo ningejua namna ya kukushauri.
 
Habari, mwezi ujao naenda kupata milioni 30. Vijana wenzangu naombeni ushauri ili nisije kujuta baadae maana hela sasa hivi sina. Na hiyo hela sidhani kama nitaipata tena kama.

Naombeni ushauri kama ungekuwa wewe ungefanyaje.

Nina mke na watoto 3
Usizitumie.
Weka bank
Tafuta kituo cha faragha...recreation...
Pata utuluvu mpaka akili ikukae sawa
 
Back
Top Bottom