Mwezi ujao napata milioni 30. Naomba ushauri namna ya kuzitumia

Hongera, pia nasikitika kwa baadhi ya wadau hapo juu wakikupa ushauri wa kipumbavu. Mtu kaomba ushauri tena kaandika hiyo hela anadhani hato ipata tena endapo ikipotea lakini baadhi ya watu wanamwambia anywee pombe na wanawake, inasikitisha sana.

Ushauri wangu, kama huto fanikiwa kupata ushauri mzuri mpaka una pokea hiyo pesa. Chukua pesa yote weka UTT, kama huna ufahamu kuhusu UTT basi ni wakati sahihi kutafuta ufahamu. Ukiweka huko hiyo 30M kwa mwezi utakuwa unapata gawio la 300k. Wakati huo pesa iko huko jaribu kutafuta ushauri kwa watu makini, usiwe na haraka ata kama huu mwaka utakata ni sawa muhimu upate ushauri sahihi utakao uelewa na kuukubali, kisha unaweza chukua maamuzi.

Ushauri mwingine, chukua 15M weka UTT. Kisha chukua 5M nenda Rukwa ndani ndani kodi shamba heka 10 piga kilimo cha mahindi hiyo pesa inatosha kabisa. Nimekushauri ulime mahindi maana ni kilimo kisicho kuwa na mambo mengi. Hiyo pesa inatosha kuhudumia shamba la hela 10 tena kwa kufuata kanuni zote za kisasa kwa kilimo husika. Chukua 7M piga ufugaji wa kuku wa mayai (layers), tafuta elimu kuhusu ufugaji wa kuku. Anza na vifaranga 600, hatua ya kwanza chukua vifaranga 300 kisha baada ya miezi mitatu weka vifaranga 300. Hiyo pesa inatosha kuwahudumia mpaka wanafikia hatua ya kutaga. Pesa inayo baki 3M mfungulie mkeo genge tafuta location kali kwa mradi husika, hii itasaidia wakati mkisubiri mavuno ya mahindi na kuku kutaga mpate pesa ya kula. Ikikupendeza unaweza kuchukua huo ushauri, ama ukipata ushauri mzuri zaidi ufuate pia. Kila la kheri
Habari mwezi ujao naenda kupata mil 30 vijana wenzangu naombeni ushauri ili nisije kujuta baadae maana hela saiz sina. Na hiyo ela sizani kama nitaipata tena kama hiyo naombeni ushauri kama ungekuwa wewe ungefanyajee.
Nina mke na watoto 3
 
Kumbe hujapata bado....always dont share vitu kabla havijakamilika..shauri zako anyway ukipata rudi upewe mawazo
 
ningeshauri mkaa sema huyu dc nae leo ataki mikaa ipite kwake sijui katumwa nananii bhana mvee iendelee
 
ASITHUBUTU
Anatakaa kifaa mdomo wazii Manchester ajaribuu hizii biashara lazima iwe mchawi ama mshirikina

Kunajamaaa anazozkadhaa mbezbeach ila akizitoa lazima azipeleke bgamoyo zinasagishwa zinakuja kuanza kazi

Laana yake ukibakiza miezi 2 dreva hakikisha na wewe mshirikna zinapata ajali mbaya zingine kwishna
 
Sema hatufamiani hizo biashara zote ziko saturated lkn hata UTT faida ni kdogo, Ningekua nakufahamu ningekuelekeza namna ya kuwekeza hiyo Pesa yako na kupata 1% Kila siku kwanzia jumatatu Hadi ijuma, kwa maana unapata laki tatu Kila cku kwa mwaka mzima, kwa maana hiyo unarudisha mtaji wako ndani ya miezi mitano na unaanza kupata faida Hadi mwaka uishe.
Sitaki mtu anifuate PM kutaka kujua hii ni biashara gani, tunafanya na watu ambao tunafamiana nao.
#No malice to anybody
 
Funguka mkuu!
 
Habari mwezi ujao naenda kupata mil 30 vijana wenzangu naombeni ushauri ili nisije kujuta baadae maana hela saiz sina. Na hiyo ela sizani kama nitaipata tena kama hiyo naombeni ushauri kama ungekuwa wewe ungefanyajee.
Nina mke na watoto 3
Nipatie nikuzungushie kila mwezi milion 2
 
Sema hatufamiani hizo biashara zote ziko saturated lkn hata UTT faida ni kdogo, Ningekua nakufahamu ningekuelekeza namna ya kuwekeza hiyo Pesa yako na kupata 1% Kila siku kwanzia jumatatu Hadi ijuma, kwa maana unapata laki tatu Kila cku kwa mwaka mzima, kwa maana hiyo unarudisha mtaji wako ndani ya miezi mitano na unaanza kupata faida Hadi mwaka uishe.
Sitaki mtu anifuate PM kutaka kujua hii ni biashara gani, tunafanya na watu ambao tunafamiana nao.
#No malice to anybody
hamna kitu hapa biashara kama inalipa haina longo longo watu wanafanya siri chimbo la mzigo sio hivi
 
Habari mwezi ujao naenda kupata mil 30 vijana wenzangu naombeni ushauri ili nisije kujuta baadae maana hela saiz sina. Na hiyo ela sizani kama nitaipata tena kama hiyo naombeni ushauri kama ungekuwa wewe ungefanyajee.
Nina mke na watoto 3
Utaipata kutoka wapi? Mkopo? Unauza kitu? Mafao ya kustaafu/kufukuza kazi/kuachakazi au vipi? Tuanzie hapo!
 
Kama hujajenga basi Jenga nyumba ndogo ishi kwa amani na familia Yako.
Kama umejenga basi fungua car wash nzuri sana ya angalau 10 ml iwe nzuri na standard.
Ml 20 zihifadhi Kisha baada ya miezi miwili baada ya car wash kuanza kazi Anza kuuza hapo vifaa vya pikipiki na bajaji pamoja na oil
Pia unaweza kufanya biashara ya chakula ,saloon za kiume na kike au vipodozi
 
Kama hutaki kumuelekeza mtu ilikuwa na maana ipi kuandika?

Back
Top Bottom