Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Tunakwenda mwaka wa saba au nane, Masheikh wasio na hatia wako Jela.
Waliwekwa ndani na Kikwete, Wakakandamizwa ndani na Magufuli, na Sasa Samia anakaribia Mwezi mmoja madarakani bado serikali yake imewaweka Jela.
Siyo masheikh wa Uamsho tu, kuna mamia kwa mamia ya Masheikh nchi nzima wasio na hatia wamewekwa ndani na utawala uliopita wa Magufuli.
Sasa Silaha ya hawa watu ni moja, Wataendelea Kumlilia Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma kwa dhulma wanazotendewa
Watasimama visimamo vya usiku, Watafanya visomo, Watafanya Kunuti, Watafanya dhikri sana, na Watafunga wakiwa jela.
Ole wao Madhalimu wenye kudhulumu watu hawa wa Mungu, Mungu atalipa kwa kila hadaa, kwa kila uongo, kwa kila dhulma waliyofanyiwa.
Namkumbusha Rais Samia, Rais Hussein Mwinyi kwa Ujumbe wa Mwenyezi Mungu aliompa Nabii Musa amfikishie Firauni kumtaka awaachie huru wana wa Israel.
Mwenyezi Mungu anasema:
"Arsil ma'anaa banii israil walaa tuaddhib humaa".
maana yake : " Waachie huru wana wa Israel na wala usiwaadhibu".
Na mimi nakueleza Rais Samia na Hussein Mwinyi, Waachieni huru watu hawa wa Mungu na wala msiwaadhibu.
Ujumbe huu nimekufikishieni, basi ni juu yenu kuupuuza au kuufanyia kazi, maana hatuombi tena, kama kuomba muwaachie hawa watu kwa miaka minane hamkufanya sasa TUNALIACHA JAMBO HILI MIKONONI MWA YULE MWENYE NGUVU ZOTE.