Mwezi wa Ramadhani umeingia Masheikh wako Jela

Mwezi wa Ramadhani umeingia Masheikh wako Jela

Wawacheni waendelee mashehe hukohuko Jela ,kwani hakuna hata moja litakalofanywa na serikali ya CCM likawa jema kwa wananchi,ni majanga tu.tokea wale mashee wawekwe ndani mnajua serikali zilikuwa zinakwaa majanga,nchi haitulii.

Viongozi walioko madaraka sura zimekunjika,hawana furaha ndani ya moyo ,wamejaa vichko vya kinafiki na wataendelea hivyo hivyo hakuna cha baba wala mama. Kila mtu ana baba yake na mama yake.

Kama hamna akili basi ongezeni mama kwa maana ya mama ni mmoja tu aliekuzaa wengine wa kambo na mnawajua,simba aitwe simba na mbwa aitwe mbwa.
 
Ungejua kwanini hawaachiwi ungenyamaza kimya ndio maana aliyewaweka ndani JK ni Mwislamu, IGP alikuwa Mwislam na Mwanasheria mkuu alikuwa mwislam Jaji Mkuu alikuwa Mwislam


so kuwa mpole wanyooshwe wakitoka watamsumbua saana mama
 
Ungejua kwaini hawaachiwi ungenyamaza ndio maana aliyewaweka ndani ni Mwislamu, IGP alikuwa Mwislam na Mwanasheria mkuu alikuwa mwislam


so kuwa mpole wanyooshwe wakitola watamsumbua saana mama
Kweli kabisa Rais alikuwa JK na Shein, IGP alikuwa Said Mwema, jaji mkuu wote walikuwa waislam.
Hilo ni suala zito la ulinzi na usalama wa kitaifa na kimataifa.

Mama Rais, asitumbukie mtegoni na kuingia kichwa kichwa juu ya hili jambo.

Everyday is Saturday................................😎
 
Mleta mada ungekuwa hata unasoma soma story za The bold ungeelewa ni jinsi gan hawa watu ni hatari kwa usalama wako,kumuhoji mtu aliekula kiapo cha ugaidi inachukua muda mrefu.

Sasa wewe fikilia Kama mtu alihojiwa na CIA miaka mi4 ndo akasema ukweli we unadhan mtu dizain hiyo bongo tutamuhoji miaka mingap ili aseme ukweli,by the way kazi ziendelee kila mtu atatumikia alichokivuna...
 
Kama wana makosa wahukumiwe ili watu wajue wanatumikia adhabu kutokana na kosa kadhaa, lakini si kuwaweka ndani tu bila ya kuendesha kesi yoyote, hivyo si vizuri kwa nchi yenye kuendeshwa na katiba na sheria za nchi. Na kwenye kesi hii pasizungumzwe udini bali haki itendeke kwani sheria zetu si za kidini ni secular laws system.
 
Tunakwenda mwaka wa saba au nane, Masheikh wasio na hatia wako Jela.

Waliwekwa ndani na Kikwete, Wakaandamizwa ndani na Magufuli, na Sasa Samia anakaribia Mwezi mmoja madarakani bado serikali yake imewaweka Jela...
Ina maana huko jela ma shekh ni wao pekee yao ? au ma shekh huwa hawafungwi kama wana makosa ?
Acha upuuzi ww mtoa huu UZI.
 
Wengi wanaochangia humu tayari wameshawahukumu hao masheikh kuwa ni magaidi, kwamba ni watu wabaya, watu hatari

Lakini mpaka sasa mwaka wa nane hakuna ushahidi wa Ugaidi wao, kesi yao inapigwa danadana.

Iko hivi, Endeleeni kuwaweka Jela, Kama walivyowekwa Jela watu wengine wa Mungu in the past!. Na wenye kuunga mkono dhulma hii endeeleeni kushangilia na kusapoti uonevu huu

Ukisoma comment wengine wanasapoti uonevu huu kwa sababu tu wanakomeshwa "Waislamu", kwao hiyo ni burudani kwao maana it seems kwa comment zao wana chuki kali sana vifuani mwao dhidi ya muslims (Wana Islamophobia) .

Ni kweli waliwekwa ndani na utawala wa rais Muislamu ndugu Kikwete, lakini mjue tu mwanasiasa ni mwanasiasa, wengine wako tayari kutenda dhulma bila hata kujali consciousness yao ya ndani, wao wanangalia power tu. Kikwete alikosea, aluwadhulumu hawa Masheikh bila haki, Dhulma hiyo ikaendelezwa na Magufuli dhidi ya hao watu, Na sasa mwezi mmoja mbele dhulma hiyo imeendelezwa na utawala wa Samia.

Ila kitu kimoja nawaambia hawa watawala wakumbuke Aya ya kwenye Qur'an

"Siiru fil ardh, fandhuruu kaifa kaana aakibatul'mujrimiin"
Maana yake "Tembeeni katika ardhi muone mwisho wa madhalimu"

Endeleeni tu kuonea watu wa Mungu tuje tuone Mwisho wenu!

Na nyie wenye kucomment kwa kebehi na dharau na chuki bila empathy wala utu kwa wenzenu kisa tu wao ni "waislamu wacha waumizwe" nanyi endeleeni kufurahia tu huu uonevu kisha tuone nanyi katika life cycle hii mtafika wapi
 
Tunakwenda mwaka wa saba au nane, Masheikh wasio na hatia wako Jela.

Waliwekwa ndani na Kikwete, Wakaandamizwa ndani na Magufuli, na Sasa Samia anakaribia Mwezi mmoja madarakani bado serikali yake imewaweka Jela....
Halafu mbona sikii viongozi wa kikristo kukamatwa au kuwa uko magerezani, inamaana ni watakatifu sana au ni nini zaidi
 
Halafu mbona sikii viongozi wa kikristo kukamatwa au kuwa uko magerezani, inamaana ni watakatifu sana au ni nini zaidi
Watoa comment wamejipa kazi ya kuhukumu
Wanawaita Masheikh ambao ushahidi wa makosa haupo mwaka wa nane sasa kuwa eti ni Magaidi

Maandiko yanasema don't judge, lest you be judged
 
Tena wawachie ,Wasiogope huyu Jiwe hawezi kufufuka na kuwauliza nani kawaruhusu wawaachie,Wasiogope,,Mama Mh Samia,,wewe ni Muislamu,,muhofu ALLAH atakujaza heri nyingi sana.
Tunakwenda mwaka wa saba au nane, Masheikh wasio na hatia wako Jela.

Waliwekwa ndani na Kikwete, Wakaandamizwa ndani na Magufuli, na Sasa Samia anakaribia Mwezi mmoja madarakani bado serikali yake imewaweka Jela....
 
Wengi wanaochangia humu tayari wameshawahukumu hao masheikh kuwa ni magaidi, kwamba ni watu wabaya, watu hatari

Lakini mpaka sasa mwaka wa nane hakuna ushahidi wa Ugaidi wao, kesi yao inapigwa danadana...
Cha ajabu nikuwa tangu wakamatwe, hakuna mtu kamwagiwa tindikali, hakuna mgeni alie dhuliwa, wala mtu kupigwa risasi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunakwenda mwaka wa saba au nane, Masheikh wasio na hatia wako Jela.

Waliwekwa ndani na Kikwete, Wakaandamizwa ndani na Magufuli, na Sasa Samia anakaribia Mwezi mmoja madarakani bado serikali yake imewaweka Jela..
Kwenye hili tuwe wapole, siyo suala la Kisiasa. Hata USA George Bush na baadaye Obama waliwaweka magaidi Guantanamo hadi walipojirishisha.

Naamini hata wewe Missile of the Nation ungekuwa ni Rais wa Tanzania halafu Muislamu, baada ya kusoma ripoti ya Siri usingewaachia.

Jiulize Rais Mohamed Shein ni Muislamu ndiye aliyewashika, akawapasia kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Jakaya Mrisho ambaye ni Muislamu pia na wote wawili wakatoka madarakani bila kuwaachia.

Haya akaja Rais mpenda misifa aliyewaachia akina Nguza na Papi Kocha na wale wezi wa dhahabu Butimba naye akasoma ripoti na akapotezea.

Wale watu chini Sheikh Farid ni hatari sana, dakika 5 wakiwa huru ni rahisi kuifanya Tanzania ikawa kama Allepo au Tikrit.

Tuiache Serikali ijiridhishe ndiyo ichukue hatua stahiki
 
Back
Top Bottom