Mwezi wa Ramadhani umeingia Masheikh wako Jela

Mwezi wa Ramadhani umeingia Masheikh wako Jela

Hizo Dua za Watu waliodhulumiwa Uhuru wao na kufungiwa nyuma ya Kuta ndefu na Nondo ndio zinazoliangamiza hili Taifa mpaka Misiba ya Rais tunaiona zamani kulikuwa hamna kitu kama hii
Karume baba alikufa akiwa nani? Au unazungumzia zamani za kale
 
Siwezi amini haya,,,Kikwete Sheni sijui kama walijua walifanyalo,,maana watu hatari kuna namna ya kuwadhibiti,,,Ila mie Ombi langu kwa Mh Mama SAMIA SULUHU,,,namuomba sana,,,hao watu wamewekwa ndani kipropoganda tu,,riport yao imeandikwa ki-propoganda.Awaonee huruma ALLAH atamjazia kheri nyingi sana,,ukizingatia huu ni mwezi wa ramadhani.
Usiandike kitu usichokijua. HAIWEZEKANI Shein na KIKWETE wote wawe wamedanganywa na Propaganda.
 
Familia za hao Mashekhe zinaishi katika msongo mkubwa wa Mawazo
 
Tunakwenda mwaka wa saba au nane, Masheikh wasio na hatia wako Jela.

Waliwekwa ndani na Kikwete, Wakakandamizwa ndani na Magufuli, na Sasa Samia anakaribia Mwezi mmoja madarakani bado serikali yake imewaweka Jela.

Siyo masheikh wa Uamsho tu, kuna mamia kwa mamia ya Masheikh nchi nzima wasio na hatia wamewekwa ndani na utawala uliopita wa Magufuli.

Sasa Silaha ya hawa watu ni moja, Wataendelea Kumlilia Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma kwa dhulma wanazotendewa
Watasimama visimamo vya usiku, Watafanya visomo, Watafanya Kunuti, Watafanya dhikri sana, na Watafunga wakiwa jela.

Ole wao Madhalimu wenye kudhulumu watu hawa wa Mungu, Mungu atalipa kwa kila hadaa, kwa kila uongo, kwa kila dhulma waliyofanyiwa.

Namkumbusha Rais Samia, Rais Hussein Mwinyi kwa Ujumbe wa Mwenyezi Mungu aliompa Nabii Musa amfikishie Firauni kumtaka awaachie huru wana wa Israel.

Mwenyezi Mungu anasema:

"Arsil ma'anaa banii israil walaa tuaddhib humaa".

maana yake : " Waachie huru wana wa Israel na wala usiwaadhibu".

Na mimi nakueleza Rais Samia na Hussein Mwinyi, Waachieni huru watu hawa wa Mungu na wala msiwaadhibu.

Ujumbe huu nimekufikishieni, basi ni juu yenu kuupuuza au kuufanyia kazi, maana hatuombi tena, kama kuomba muwaachie hawa watu kwa miaka minane hamkufanya sasa TUNALIACHA JAMBO HILI MIKONONI MWA YULE MWENYE NGUVU ZOTE.
Hivi watuhumiwa wengine sio watu mbona hamuwalalamiki kukaa ndani mdaa mrefu kutwa ni kuongelea mashehe tu kwanza hawakukamatwa kama mashehe bali kama watuhumiwa
 
Mnao waoneaga huruma hawa magaidi hivi hamfuatilii kinachoendelea Msumbiji jinsi majitu type hii yanavyo chinja wenzao. Kuweni serious bhana
Hawa wameshikwa fikra zao na udini ndio maana magaidi huwa wanafanya ugaidi kwa mwamvuli wa dini ili kupata ushawishi
 
Unajua kuna baadhi ya watu ujinga ni sehemu ya maisha yao.Mashekh ni magaidi walitaka kuifanya Tanzania kama Somalia halafu kuna mijitu inakuja hapa kubwabwaja eti waachiwe!.

Kwa taarifa yenu mpaka Mwaka huu bado watu wana endelea kukamatwa kuhusiana na ugaidi wa Zanzibar,Arusha na huko kusini.Ukiona unakula ugali wako kwa amani basi elewa kuna watu hawalali usiku na mchana kuhakikisha taifa libakuwa salama.

Hao Mashekh na wengine wote wakioshiriki matendo ya kigaidi hawastahili uhuru kama mwanzisha mada ,yafaa waishi huko magereza maisha yao yote.
Hasahasa huko Twitter Kuna watu wanapongeza Sana hawa mashekh, unabaki unashangaa tu
 
Back
Top Bottom