Kwenye hili tuwe wapole, siyo suala la Kisiasa. Hata USA George Bush na baadaye Obama waliwaweka magaidi Guantanamo hadi walipojirishisha.
Naamini hata wewe
Missile of the Nation ungekuwa ni Rais wa Tanzania halafu Muislamu, baada ya kusoma ripoti ya Siri usingewaachia.
Jiulize Rais Mohamed Shein ni Muislamu ndiye aliyewashika, akawapasia kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Jakaya Mrisho ambaye ni Muislamu pia na wote wawili wakatoka madarakani bila kuwaachia.
Haya akaja Rais mpenda misifa aliyewaachia akina Nguza na Papi Kocha na wale wezi wa dhahabu Butimba naye akasoma ripoti na akapotezea.
Wale watu chini Sheikh Farid ni hatari sana, dakika 5 wakiwa huru ni rahisi kuifanya Tanzania ikawa kama Allepo au Tikrit.
Tuiache Serikali ijiridhishe ndiyo ichukue hatua stahiki