Mwezi wa Ramadhani umeingia Masheikh wako Jela

Mwezi wa Ramadhani umeingia Masheikh wako Jela

Guantanamo Bay wengi walionewa, na Guantanamo bay haikuwa sifa njema kwa Marekani.

Na wala si kigezo chema kujifunza na kufanya matendo ya gross human rights violations kwa sababu yamefanywa na Marekani. Tujifunze mazuri kutoka huko tusijifunze yale ya uovu
Hawa akina Sheikh Farid wa uamsho ndiyo wanachafua dini ya Islam uonekane ni ugaidi wakati si KWELI. Kama wanataka wawe wanava combat za guerillas au kiraia kuliko kuvaa mavazi yenye taswira ya kidini wanapotenda maovu yao. Sympathy ya dini isitumike kuona kuwa wanaonewa
 
Hao watu walihoji muungano tu, na kuhamasisha wazanzibar wauangalie muungano kwa jicho la tatu. Kosa lao ndiyo hilo!.

Hawa wanaodai kuwa hao masheikh ni magaidi ni islamophobes tu ambao wanachuki kali ya kimyakimya with anythibg islamic
Mkuu ninachokumbuka nikwamba walikuwa wanadai uhuru kamili wa masuala ya muungano, na pia walikuwa hawataki kusikia kitu chochote kinachoitwa chadema, ccm, cuf etc,walikuwa wakikuta bendera hizi wanashusha wanapandisha nyeupe ya kwao plus maandamano kadha wa kadha kwa lengo la kuisimamisha dini ya Mungu, kipindi hiki ndio makanisa yalichomwa sana moto pamoja na watu kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana, je unadhan tulikokuwa tunaelekea ni sahihi??
 
Hii hali ingeendelea au ingenyamaziwa ingekuwaje mkuu, sikebei ila nataka tujadili kwa facts with vivid evidences.
tapatalk_1618315615801.jpeg
 
Mkuu ninachokumbuka nikwamba walikuwa wanadai uhuru kamili wa masuala ya muungano, na pia walikuwa hawataki kusikia kitu chochote kinachoitwa chadema, ccm, cuf etc,walikuwa wakikuta bendera hizi wanashusha wanapandisha nyeupe ya kwao plus maandamano kadha wa kadha kwa lengo la kuisimamisha dini ya Mungu, kipindi hiki ndio makanisa yalichomwa sana moto pamoja na watu kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana, je unadhan tulikokuwa tunaelekea ni sahihi??
Huyo jamaa ni jinga kabisa, kwa makusudi anapindisha ukweli wa walichofanga uamsho kule zenj.
Huko jela ni sehemu sahihi kwao
 
Tunakwenda mwaka wa saba au nane, Masheikh wasio na hatia wako Jela.

Waliwekwa ndani na Kikwete, Wakakandamizwa ndani na Magufuli, na Sasa Samia anakaribia Mwezi mmoja madarakani bado serikali yake imewaweka Jela.

Siyo masheikh wa Uamsho tu, kuna mamia kwa mamia ya Masheikh nchi nzima wasio na hatia wamewekwa ndani na utawala uliopita wa Magufuli.

Sasa Silaha ya hawa watu ni moja, Wataendelea Kumlilia Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma kwa dhulma wanazotendewa
Watasimama visimamo vya usiku, Watafanya visomo, Watafanya Kunuti, Watafanya dhikri sana, na Watafunga wakiwa jela.

Ole wao Madhalimu wenye kudhulumu watu hawa wa Mungu, Mungu atalipa kwa kila hadaa, kwa kila uongo, kwa kila dhulma waliyofanyiwa.

Namkumbusha Rais Samia, Rais Hussein Mwinyi kwa Ujumbe wa Mwenyezi Mungu aliompa Nabii Musa amfikishie Firauni kumtaka awaachie huru wana wa Israel.

Mwenyezi Mungu anasema:

"Arsil ma'anaa banii israil walaa tuaddhib humaa".

maana yake : " Waachie huru wana wa Israel na wala usiwaadhibu".

Na mimi nakueleza Rais Samia na Hussein Mwinyi, Waachieni huru watu hawa wa Mungu na wala msiwaadhibu.

Ujumbe huu nimekufikishieni, basi ni juu yenu kuupuuza au kuufanyia kazi, maana hatuombi tena, kama kuomba muwaachie hawa watu kwa miaka minane hamkufanya sasa TUNALIACHA JAMBO HILI MIKONONI MWA YULE MWENYE NGUVU ZOTE.
Unataka kutuamnisha kwamba nchi nzima masheikh ni hao tu wa uamsho wengine sio masheikh? Au na wewe ndio wale mnaoshinda Mozambiq kazi yenu kukata vichwa watu eti mnampigania Allah?
 
Those guys waliuchallenge Muungano kwa challenge kubwa.
Ndiyo maana unaona badala ya wao kushitakiwa Zanzibar(kama kweli walitenda makosa huko zenji) walitekwa na kukimbizwa bara ili washitakiwe huku!
Kiufupi kwa mujibu wa sheria zetu hata kitendo cha kuwaleta bara badala ya kuwashitaki hukohuko Zanzibar ni kinyume cha sheria
Acha uongo wewe, hao masheikh si ndio kundi la akina Sheikh Ilunga, ambaye mafundisho yake mpaka leo ndio yanasumbua vijana kwa wazee wanauawa kuanzia mombasa mpaka Msumbiji wote magaidi wanatumia mafundisho yao, sio watu kabisa hawana hata chembe ya huruma, hivi hii dini shughuli ya kuchinjana ingeingia Afrika miaka 50 iliyopita wewe na wazazi wako ungekua hai? Maana sidhani kama uliupata uislam kamili na wenzako hawa hawa wangekuchinja wewe au baba yako
 
Mkuu ninachokumbuka nikwamba walikuwa wanadai uhuru kamili wa masuala ya muungano, na pia walikuwa hawataki kusikia kitu chochote kinachoitwa chadema, ccm, cuf etc,walikuwa wakikuta bendera hizi wanashusha wanapandisha nyeupe ya kwao plus maandamano kadha wa kadha kwa lengo la kuisimamisha dini ya Mungu, kipindi hiki ndio makanisa yalichomwa sana moto pamoja na watu kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana, je unadhan tulikokuwa tunaelekea ni sahihi??
Matendo ya kuchoma makanisa na kuuawa padri huko Zanzibar waliletwa wachunguzi wa kimataifa kuchunguza nadhani ni Scotland yard, Kama ushahidi wa wao kuhusika na vitendo hivyo upo,
kwa nini kesi yao inapigwa kalenda kwa hoja za upelekezi bado haujakamilika!

8 years hakuna ushahidi!
 
HAta hiyo ya kushawishi tu; kwenye sheria hao vingozi wa dini ni raia kama sisi so kwanini useme eti sheikh Abubakari ashawishi fulani na fulani wawekwe ndani?
Kwahiyo Abubakari hana ushawishi kwa serikali kwa nafasi aliyonayo?
 
Comments humu ndani zinaonyesha kuwa kuna silent Islamophobia ya kutisha ndani ya hii nchi (chuki kali ya kimyakimya dhidi ya muslims) .

Watu wanahukumu wenzao bila ushahidi, yaani wanaenjoy watu kuteswa, kuumizwa na kubambikiziwa kesi bila haki.

Hao Masheikh hakuna ushahidi uliofikishwa mahakamani kuonyesha wanahusika na ugaidi, lakini watu wameng'ang'ania kuwa ni magaidi magaidi au kwa sababu ni waislamu kwa hiyo lebo ya ugaidi inawakaa vizuri eh?

Nyie watu acheni kutetea uonevu kwa sababu ya chuki za kimyakimya za kidini
Hakuna mwenye chuki na uislamu mkuu, ndio maana wewe ni muislamu na hauko jela

Hao mashekh wako jela kwasababu ya matendo yao, uislamu wao si sababu.
 
Hakuna mwenye chuki na uislamu mkuu, ndio maana wewe ni muislamu na hauko jela

Hao mashekh wako jela kwasababu ya matendo yao, uislamu wao si sababu.
Matendo mabaya huletwa ushahidi, sasa ushahidi haupo mwaka wa nane sasa. Huoni kuwa kuna something wrong?
 
Unataka kutuamnisha kwamba nchi nzima masheikh ni hao tu wa uamsho wengine sio masheikh? Au na wewe ndio wale mnaoshinda Mozambiq kazi yenu kukata vichwa watu eti mnampigania Allah?
Kuna Masheikh wengi sana Jela kiuonevu zaidi ya hao
 
Matendo mabaya huletwa ushahidi, sasa ushahidi haupo mwaka wa nane sasa. Huoni kuwa kuna something wrong?
Cha kushangaza, mwendazake aliwaacha mashehe wa watu waendelee kusota sero bila ushahidi wa madai dhidi yao, lakini akawaachia huru kina babu Seya ambao mahakama ilithibitisha pasi na shaka kuwa walikuwa walawiti wa watoto

Afu kuna mijitu inamwita mtetezi wa wanyonge...
 
Matendo mabaya huletwa ushahidi, sasa ushahidi haupo mwaka wa nane sasa. Huoni kuwa kuna something wrong?
Kabla hawajakamatwa tulishuhudia mlolongo wa matukio mengi sana hapo Zanzibar, kuuwawa kwa mapadre, kumwagiwa tindikali nk nk

Lakini baada ya kukamatwa, hatujawahi kusikia tukio lenye viashilia vile tena

Kwa mazingira hayo kwanini tusiamini wao ndo walikua masterplanners wa matukio yale?
 
ila cha motto wamekiona sijui kama watarudia tena ‘uchochezi’ wao, walikuwa wameanza kuota mapembe!
 
Hoja yako haina mashiko!

Zanzibar aliuawa Padri mmoja, na aliuawa mwaka 2013 wakati Masheikh wametiwa ndani mwaka 2012

Sasa Sijui Hao Masheikh walitoka ndani wakafanya tukio kisha wakajirudisha?
 
ila cha motto wamekiona sijui kama watarudia tena ‘uchochezi’ wao, walikuwa wameanza kuota mapembe!
Kwa hoja hizi za Cha Moto wamekiona ndicho hichohicho walichokiona akina Lissu, Ben Saanane, Azory Gwanda etc

Hao Masheikh walitaka Zanzibar huru!, Walitaka Zanzibar isiyokaliwa na Tanganyika.

Kama hilo ni kosa basi washitakiwe kwa kosa hilo(kama lipo kwenye sheria), Kama ni Uhaini basi washitakiwe kwa Uhaini lakini siyo chengachenga za kuwabambikiza makosa yasiyokuwepo huku ushahidi haupo!
 
hao sahau kabisa.......sio leo au keshokutwa......tusiache kuwaombea ni wa-TZ wenzetu
 
Back
Top Bottom