Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Waziri wa Fedha, Mwigulu amejigamba Mbungeni kuwa "Anayeonge ndiye Waziri Fedha, mikirudi Majimboni waambieni Wajumbe wenu hakuna awamu tumetoa pesa kama awamu hii ya Sita
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
==
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema hakuna awamu ambayo imetoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo kama awamu ya sasa inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Akichangia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Halima Mdee, Waziri Nchemba amesema anachokisema anakijua kwa sababu amekuwa kwenye Wizara ya Fedha tangu akiwa naibu waziri.
Amesema miradi inayotekelezwa katika majimbo ya wabunge ni uthibitisho wa fedha nyingi zinazoelekezwa kwenye maendeleo badala ya kubaki benki, kitu ambacho hata wao wanajua hakijawahi kuwepo.
Akitoa mfano, ameeleza kuwa mradi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere umetumia zaidi ya shilingi trilioni 6.5, kiasi ambacho ni sawa na bajeti ya maendeleo ya baadhi ya nchi.
Hata hivyo, Dkt. Mwigulu amekiri kuwa kuna maeneo ambayo bajeti haijatekelezwa kwa asilimia 100, akieleza kuwa sababu ni uchepushaji wa fedha kushughulikia majanga ya kibinadamu, kama maporomoko ya udongo yaliyotokea Hanang.