Mwigulu: Awamu ya 5 kuna Kiongozi mkosoaji alishambuliwa ilionekane ni Serikali

Mwigulu: Awamu ya 5 kuna Kiongozi mkosoaji alishambuliwa ilionekane ni Serikali

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesayasema hayo Mei 23, 2026 wakati akizungumza na wananchi wa mkoa wa Iringa, katika viwanja vya kichangani.

Dkt. Mwigulu yupo mkoani Iringa kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Mbinu za kawaida hizi,
"Brame the victim" Hatua ya pili watu wakiishaanza kuamini, unatuma polisi wamkamate victim kwa makosa
 
Mwigulu unasema tuwe macho tusikubali kugawanywa na watu wenye nia ovu. Hupni kwamba wewe ndiye unaewagawa watu kwa uongo wako??

Kumbuka kutakuwepo na kundi litakalokuunga mkono na kundi lingine litasimamia ukweli hivyo kukupinga. Uongo unakusaidia nn? Uliwahi kutamka Bungeni kuwa una ushahidi wa duniani na mbinguni kuthibitisha Lwakatare alikuwa gaidi. Kumbe uongo mtupu.

Wakati mwingine ukiwa unatengeneza uongo wako jaribu kuzisoma nyuso za watazamaji wako. Utagundua kama wanakukubali au wanakupotezea. Lkn kama huna uwezo huo, utaendelea kuongea mwisho wakuone hamnazo. Iko siku utatuambia kuwa wewe sio Mnyiramba bali Mmasai wa Ilboru.
 
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesayasema hayo Mei 23, 2026 wakati akizungumza na wananchi wa mkoa wa Iringa, katika viwanja vya kichangani.

Dkt. Mwigulu yupo mkoani Iringa kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Hiki anachokisema, hata mimi niliwahi kulisema hapa Shambulio la Lissu: Wajue wasiojulikana watakaojulikana na 'Wasiojulikana' ambao kamwe, hawatajulikana nilisema
Wanabodi,

Tangu kutokea kwa shambulizi kwa Mhe.Tundu Lissu, ambalo mpaka sasa linaelezwa kufanywa na watu wasiojulikana, kumeibuka shauku kubwa ya watu kutaka kuwabaini hawa watu wanaoitwa ni watu wasiojulikana, ni kina nani?, wanatumwa na nani? na lengo lao ni nini?, kunakopelekea kujengwa kwa dhana mbalimbali kuhusiana na wasiojulikana hawa, hadi kufikia kuwanyooshea vidole baadhi ya watu, wakiwemo wale 'jamaa zetu' kuwa ndio watu wasiojulilana!.

Ukimya wa Jeshi letu la polisi kuhusu matukio haya, japo ushahidi wa wazi upo lakini hakuna any update ya uchunguzi, na utulivu wa Comred Mwingulu Nchemba, kuonyeshea, he knows something ameamua bora ajinyamazie tuu kimya kusubiria hatima yake, huku ameisha amua liwalo na liwe kwenye hatima yake!, of which time will tell!

3. Divide and Rule za Mabeberu
Lakini kama the motive behind wasiojulikana hawa ni hawa mabeberu wezi wa rasilimali zetu na lengo lao ni kutufarakanisha sisi na serikali yetu kwa devide and rule, wagawanye uwatawale, ili kutuhamisha kwenye hoja za rasilimali zetu, ili tusahau makinikia, Tanzanite, Dhahabu, Almasi na Gesi, then, sisi as sisi, hatuna uwezo huo wa kuwabaini bila msaada wa Scotland Yard, ila, kwa vile tayari, tumeisha wastukia nia yao ovu, hatuta farakana, tutasimama firm as one, and under th e united front. Kama lengo ni ili tufarakane, tuichukie serikali yetu kuwa ni ya kidikiteta, na kuanza kufanya vurugu, tukifarakana, tutakuwa tumewapa walichokitaka, tusikubali kufarakana, kwa kufakaranishwa na wafakaranishaji hawa, lets stand together as one, tupendane, tuheshimiane, tuvumiliane, tustahimiliane, tubishane bila kupigana, tukubaliane kwenye maslahi ya taifa na ikishindikana tukashindwa kukubaliana, then tukubaliane kutokubaliana lakini mwisho wa siku, wasiojulikana wajulikane lakini 'wasiojulikana', sijui.
Paskali
Leo Mhe. Mwigulu, amekisema kile mimi nilichokisema anakijua, lakini amenyamaza kimya.
Kauli hii ya Waziri Mkuu, ni uthibitisho kuwa Tanzania tuna inteligensia nzuri sana ya kuhisi tuu, lakini hatuna uwezo wa kuchunguza na kuwabaini hawa wanaocheza michezo hii, ambayo mwisho wa siku, vina tuchafua!.

Kama ni kweli tunajua chochote kuhusu michezo hii, kwanini tumenyamaza kimya na hatukuwahi kusema kitu mpaka leo huku taasisi zetu nyeti zikichafuliwa?!, TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Kauli hii, ingetolewa na kiongozi wa upande fulani, kesho yake angeitwa mahali kutoa maelezo kuthibitisha, lakini akisema wa upande huu, ni sawa tuu!.

P,
 
Vilaza wana taabu sana humu duniani. Watanzania sio wajinga, wanakuchora tu ukimwaga upupu. Majibu wanayo tayari hata akikana sasa sio wao.
 
Huyu mwanamtandao anasemaje?Anaogopa hata kutaja jina la Lissu
 
Makaburi ya CCM kupigwa viboko

SAMIA NAYE KUINGIA KATIKA VITABU VYA HISTORIA KAMA DIKTETA MWANAMKE ALIYEKUWA MADARAKANI KWA MUDA MFUPI SANA

06 Januari 2025

Kumbukumbu ya Udikteta wa mwendazake Francisco Franco waipasua Uhispania miaka 50 baada ya kifo​

1779563054932.jpeg

FILE - Miaka hamsini baada ya kifo chake, legasi ya Franco inaendelea kuigawanya Uhispania [Faili poto: Javier Bernardo / Serikali ya Mkoa wa Melilla]


Kundi la Upinzani wa kihafidhina nchini Hispania utasusia kuhudhuria kumbukumbu rasmi za kuadhimisha miaka 50 ya kifo cha dikteta wa mrengo wa kulia mwendazake jenerali Francisco Franco, na hatua hii kuweka wazi mgawanyiko wa kudumu wa legasi yake katika taifa la Hispania.


Jenerali Francisco Franco aliipindua jamhuri ya kidemokrasia ya Uhispania katika vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoua mamia ya maelfu na kutawala kwa mkono wa chuma kwa miaka 36 mfululizo kuanzia mwaka 1939 hadi kifo chake mwaka wa 1975.

Waziri Mkuu wa Kisoshalisti Pedro Sanchez ametangaza karibu matukio 100 muhimu ya kukumbuka mnamo 2025 "kuonyesha mabadiliko makubwa yaliyopatikana" katika nusu karne tangu nchi hiyo ya Ulaya ianzishe mabadiliko yake ya kidemokrasia.

Makumbusho hayo yatahusisha pia sanaa katika jumba la Makumbusho la Malkia (Reina) Sofia huko Madrid - nyumbani uliopo mchoro wa "Guernica" wa mchoraji maarufu Pablo Picasso, mojawapo ya kazi maarufu zaidi inayomuangazia mwendazake dikteta Franco - imeandaliwa kama sherehe ya kwanza siku ya Jumatano.

Waziri mkuu Pedro Sanchez ataongoza maadhimisho ya kumbukumbu hizo lakini si Mfalme Felipe VI wa Hispania wala kiongozi wa chama kikuu cha kihafidhina cha Popular Party (PP), Alberto Nunez Feijoo, atakayehudhuria.

Alberto Feijoo anaamini kuwa mpango huo ni mbinu nyemelezi hadaa ya serikali ya wachache ya mrengo wa kushoto ili kuvuruga utata unaoangaziwa sasa kuhusu matatizo yanayoikabili serikali yake hususan changamoto za kisiasa na kisheria.

Uchunguzi wa ufisadi unaendelea dhidi ya mke wa waziri mkuj Pedro Sanchez na washirika wake wa kisiasa, huku Wanasoshalisti wakilazimika kujadiliana kwa uchungu na safu ya vyama pinzani na vyenye kujitenga ili kupitisha sheria bungeni.


Maadhimisho yaliyopangwa nchini kote ikiwemo katika shule, vyuo vikuu, makumbusho na mitaa ni kazi ya serikali ambayo "katika hali yake ya kukata tamaa mara kwa mara inaangalia yaliyopita kujiokoa ", Feijoo alisema.


Wasoshalisti wamejibu kwa kuashiria chimbuko la chama cha PP, kilichozaliwa mwaka 1989 kama mrithi wa Muungano wa Popular, ulioanzishwa mwaka 1976 na waziri wa zamani wa Franco.


Jamaa wa Waathirika wa utawala wa mwendazake dikteta Franco wakatishwa tamaa
Kundi la Mrengo wa kulia wa Vox , muungano wa tatu kwa ukubwa bungeni, pia kitapuuza mpango huo wa maadhimisho ya aliyekuwa dikteta Franco .


Mmoja wa wabunge wake hivi karibuni alisema bungeni kwamba utawala wa mwendazake dikteta Fransisco Franco "haukuwa kipindi cha giza, kama serikali hii ya sasa inavyoelezea, badala yake ni hatua ya ujenzi, maendeleo na maridhiano"
1779567860466.jpeg

Familia zikiwa zimeshika picha za wapendwa wao waliopotea, kuuawa na kufungwa wakati wa utawala wa Dikteta wa Uhispania mwendazake Francisco Franco alipopindua jamhuri ya kidemokrasia katika vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoua mamia ya maelfu [Picha ya faili: Pierre-Philippe Marcou / AFP]

Kwa upande mwingine wa wigo wa kisiasa, Podemos wa mrengo mkali wa kushoto ameziita kumbukumbu hizo kama kiini-macho mazingaombwe "facade" ili kuficha fidia ndogo kwa waathiriwa wa udikteta.


Pedro Sanchez alipitisha sheria ya "kumbukumbu ya kidemokrasia" mnamo 2022 inayolenga kufufua kumbukumbu zao, pamoja na kuunda rejista ya waathiriwa na kuondolewa kwa alama za Wafaransa.

Lakini sheria haijajaribu au kuwahukumu maafisa wowote wa zamani wa Franco wanaotuhumiwa kwa uhalifu na ambao wanasalia hai huku wakinufaika na msamaha ulioidhinishwa wakati wa mpito, na kuwakatisha tamaa manusura.


Kumbukumbu ya mgawanyiko ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya 1936-1939 na jenerali Franco inatokana na kuangamia kwa serikali, kulingana na Joan Maria Thomas, profesa wa historia ya kisasa katika Chuo Kikuu cha Rovira i Virgili.

Franco akiwa na umri wa miaka 82 na mgonjwa alifariki dunia kwa amani hospitalini, tofauti na anguko la kustaajabisha la Ujerumani ya Nazi 1945 na Italia ya kifashisti Mussolini wakati wa Vita vya Pili vya Ulimwengu au Mapinduzi ya Carnation ambayo yalipindua udikteta wa mrengo wa kulia wa Ureno mnamo 1974.

Uchaguzi wa kidemokrasia ulifuatiwa mwaka wa 1977 na Wahispania wapya walioidhinisha katiba mpya katika kura ya maoni mwaka uliofuata, ambayo sasa inaadhimishwa kama Sikukuu ya Kitaifa kila mnamo Desemba 6.

Hatua 'Chanya' imepigwa
Nchini Uhispania, "kulikuwa na makubaliano makubwa yasiyo rasmi ... " ya kuacha kufukua makaburi kuangalia dhuluma za siku za nyuma chini ya utawala wa mwendazake dikteta Franco, Thomas aliiambia AFP.

Kukumbuka kifo cha dikteta jenerali Fransisco Franco kilikuwa "chanya" kwa sababu Uhispania ya leo "haizingatii umuhimu wa kurejesha mfumo wa kidemokrasia mwaka 1977 na kuweza kuuunganisha", alisema.

Lakini "hatuwezi kuepuka... au kupuuza kumbukumbu ya sehemu ya nchi yetu ambayo ilikuwa inamuunga mkono Franco, ambayo ilikuwa sehemu kubwa," aliongeza.


Wafuasi wa Kikatoliki wa kifashisti na wahafidhina walikuwa miongoni mwa wafuasi wake wakubwa waaminifu, na wakati mmoja walimheshimu dikteta jenerali Franco kwa wingi na kutembelea Bonde la Mashujaa Waliofariki, kaburi kubwa karibu na Madrid ambalo lilihifadhi kaburi la nwendazake jenerali Franscisco Franco .

Serikali ya awali ya Pedro Sanchez ilichukua hatua ya kihistoria ya kuondoa mabaki ya mwili wa dikteta Francisco Franco mnamo 2019 na kulibadilisha jina la bonde hilo, linaloonekana kama kumbukumbu ya ushindi kwa sababu yake.


Katika uchunguzi wa mwaka wa 2018 wa mchambuzi Sigma Dos wa gazeti la El Mundo la kila siku la kihafidhina, mpango huo wa kuondoa mabaki ya mwili wa dikteta Franscisco Franco kutoka makaburi ya mashujaa wa kitaifa ya Bonde la Waliofariki ulipata kuungwa mkono zaidi kidogo tu kuliko ulivyopingwa.
Chanzo: AFP
 
Miye naona matukio yanayofanywa na CCM mtandao yamemshinda ameamua kuropoka kimjiacho.
 
Back
Top Bottom