Mwigulu: Cement bei juu kwa sababu ya vita ya Ukraine na Urusi

Suzy Elias

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,067
Reaction score
6,200

"...gharama za cement zimeendelea kupanda kila mara na hilo la vita ya Ukraine na Urusi ndilo limeongeza changamoto ya kupanda kwa bei..."

"...nimewataka wadau waone namna bora ya kupunguza gharama kupanda mara kwa mara kwa maslahi ya wananchi wetu."

Amesema Mwigulu.

Nb: Tanga cement na Dangote cement si mhamishie viwanda vyenu Tanzania ili bei ya cement ipungue?!
 
Kwani sasa hivi mfuko wa Cement unaenda sh.ngapi...?
 
westbrookwtf.png
 
Hawa jamaa...elimu makaratasi sio kumukichwa. Sasa hivi wanapga hela kwa kwenda mbele kisingizio eti Ukraine....Elimu yao kupambana na hii hali, Imekua kukimbilia World Bank madigrii yao makaratasi. Raslimali tulizonazo hawazioni macho wanayo,mbongo wanazo .ila Fikra hawana!!Nchi yangu Tanzania mamaaweee!!
 
Nikishasema humu tunaongozwa na viongozi wajinga na asilimia 90% ya watumishi wa umma ni incompitent ukilinganisha na wa nchi nyingine huko.

Walisima vizuri na wenye maonp wapo uraiani wanahenyeka, yale maboga ndo yamepewa nyadhifa kubwa.

Hebu kumbuka tu zile division four za 28 zilizokuwa zunaenda nursing na Clinical officers, ualimu, polisi na kazi nyeti nyinginezo, zimetuzalishia watumishi wangapi mambumbumbu ambao wapo kwenye system mpaka sasa?

Hao ndo wakina Mwigulu.
 
... ni kama walikuwa wanaombea vita ya Ukraine itokee ili utetezi upatikane! Bei ya cement na vifaa vya ujenzi ilianza kupaa hata kabla ya vita.
 
"...gharama za cement zimeendelea kupanda kila mara na hilo la vita ya Ukraine na Urusi ndilo limeongeza changamoto ya kupanda kwa bei..."

"...nimewataka wadau waone namna bora ya kupunguza gharama kupanda mara kwa mara kwa maslahi ya wananchi wetu."

Amesema Mwigulu.

Nb: Tanga cement na Dangote cement si mhamishie viwanda vyenu Tanzania ili bei ya cement ipungue?!
Sijawahi kuona waziri mzigo kama Mwigulu. Sijui Mama alimuokota wapi huyu kilaza jamani!!!
 
"...gharama za cement zimeendelea kupanda kila mara na hilo la vita ya Ukraine na Urusi ndilo limeongeza changamoto ya kupanda kwa bei..."

"...nimewataka wadau waone namna bora ya kupunguza gharama kupanda mara kwa mara kwa maslahi ya wananchi wetu."

Amesema Mwigulu.

Nb: Tanga cement na Dangote cement si mhamishie viwanda vyenu Tanzania ili bei ya cement ipungue?!
Ni kweli kasema hayo!??! Au mnamlisha maneno bwana fedha. Nijuavyo cement na nondo zimeanza kupanda bei kitambo sana. Lakini pia ingridients zinazotumika kuzalisha cement kwa sehemu kubwa zinapatikana hapa hapa Tanzania!!! Au kuna mambo mi sijui?!?
 
"...gharama za cement zimeendelea kupanda kila mara na hilo la vita ya Ukraine na Urusi ndilo limeongeza changamoto ya kupanda kwa bei..."

"...nimewataka wadau waone namna bora ya kupunguza gharama kupanda mara kwa mara kwa maslahi ya wananchi wetu."

Amesema Mwigulu.

Nb: Tanga cement na Dangote cement si mhamishie viwanda vyenu Tanzania ili bei ya cement ipungue?!
Mwigulu uwe na aibu. Hapa nilipo bei iko juu vilevile Tangu sept 2021. Hii Vita ya Ukraine na Rusia ilianza mwaka Jana kimya kimya bila Sisi kutangaziwa?

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
 
Mtu anaye ongea kwa kuweka mikono mfukoni CYO POA kbsa
 
Dah asee Tz tumekosa nini kwa Mungu mbona anatupa viongozi mizigo namna hii, Hao ndio huwa wanàhalalisha nchi za kiafrika kuitwa shit hole.
 
ni kweli kasema hayo!??! au mnamlisha maneno bwana fedha. nijuavyo cement na nondo zimeanza kupanda bei kitambo sana. lakini pia ingridients zinazotumika kuzalisha cement kwa sehemu kubwa zinapatikana hapa hapa TZ!!! au kuna mambo mi sijui?!?
Amesema na Taarifa ya Benny Mwaipaja inafafanua zaidi:

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ametoa rai kwa kampuni zinazozalisha saruji hapa nchini kuangalia gharama zao za uzalishaji ili kuleta nafuu kwa wananchi pamoja na Serikali inayohitaji saruji kwa wingi katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati ya ujenzi.

Dkt. Nchemba ametoa rai hiyo Jijini Dodoma, alipokutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Kampuni ya Afrisam ambayo ni mmoja wa wanahisa wakubwa wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga.

Aliishukuru kampuni hiyo kwa kufanikisha upatikanaji wa saruji kwa wakati katika utekelezaji wa mradi wa shilingi trilioni 1.3, Fedha za Uviko 19 na kuwaomba wazalishaji hao kufanya hivyo wakati huu ambapo bei ya vitu vinapanda kutokana na vita vinavyoendelea baina ya Urusi na Ukraine.

Alikumbushia jinsi ambavyo Wizara ya kisekta yaani Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, ilivyokaa na wawekezaji hao wakati wa kujenga madarasa na kuwaomba wasipandishe bei kwa sababu ya uhitaji mkubwa wa bidhaa hiyo uliokuwa umesababishwa na mahitaji ya ujenzi wa madarasa na walikubaliana kufanya hivyo bila kuongeza gharama zaidi.

Dkt. Nchemba alikumbushia pia hivi majuzi pale bei za vifaa vya ujenzi vilipopanda gharama, waliitikia tena wito wa Serikali wa kuwaomba waendelee kuangalia bei ya saruji na kusimamia gharama za uzalishaji.

“Rai yetu, haya mambo ya bei kuongezeka yanaendelea hasa baada ya kuja hili jambo jipya la vita vya Urusi na Ukraine, tuendelee kukabiliana na majanga ya namna hii huku tukiwajali wananchi masikini, sisi huku kwenye sekta ya uzalishaji tukichoka kubeba mzigo, wananchi wetu ambao ni watumiaji wa mwisho watachoka zaidi” alisisitiza Dkt. Nchemba.

Kuhusu masuala ya uwekezaji wao hapa nchini, ambayo ndiyo agenda iliyowapeleka kuzungumza naye, Dkt. Nchemba aliwahakikishia wawekezaji hao kwamba itawalinda na kuwajengea mazingira mazuri ya kufanyabiashara zao kwa kuwa ndio msisitizo mkubwa uliotolewa na Mkuu wa Nchi, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Dkt. Nchemba alieleza kuwa ili kuwezesha uwekezaji mkubwa uendelee kuja Tanzania, ni pamoja na kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji kwa ajili ya kuzalisha ajira na pia vyanzo vipya vya kodi ambavyo vitawapunguzia mzigo na kuwapatia fedha wananchi kwa ajili ya kufanya shughuli za maendeleo.

Kwa upande wake Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya AfriSam, Bw. Erick Diack, alisema kuwa kampuni yake ipo nchini tangu mwaka 1996 na imewekeza zaidi ya dola za Marekani milioni 190.2 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 55.7 kati ya mwaka 2009 hadi mwaka 2016.

Alisema kuwa Kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha tani milioni 1.2 kwa mwaka na katika kipindi kifupi kijacho wanakusudia kuongeza uwekezaji na ufanisi kwa kufunga mitambo mingine yenye uwezo mkubwa wa kuzalisha.
 
ooo ok, vita kaitaja kiujumla lakini sio specific kwenye cement. wajameni mbona bia hazipandi bei na ndio waathirika direct wa vita hii maana wakati mwingine hulazimika kuagiza shayiri nje ya nchi na nyingi inatoka hukohuko kwenye mchapano. Why?????!!!!???
 
Anatuonaje sisi huyu?
Mwigulu Nchemba, Makonda, Ole Sabaya, na Mwendazake, Wana hulka ya Udictator, na kwa hiyo mtazamo wao kwa Watu winginne ni kuwatwisha mizigo bila kuwajali.
 
Back
Top Bottom