Mfikirishi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 8,939
- 10,403
Uchumi wa wizi...Hivi Mwigulu kasoma uchumi gani?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uchumi wa wizi...Hivi Mwigulu kasoma uchumi gani?
Huyu ni waziri mbovu kabisa kuwahi kutokea
"...gharama za cement zimeendelea kupanda kila mara na hilo la vita ya Ukraine na Urusi ndilo limeongeza changamoto ya kupanda kwa bei..."
"...nimewataka wadau waone namna bora ya kupunguza gharama kupanda mara kwa mara kwa maslahi ya wananchi wetu."
Amesema Mwigulu.
Nb: Tanga cement na Dangote cement si mhamishie viwanda vyenu Tanzania ili bei ya cement ipungue?!
Bora hata dikteta... hao si watu. Ni majangili au maharamia.Mwigulu Nchemba, Makonda, Ole Sabaya, na Mwendazake, Wana hulka ya Udictator, na kwa hiyo mtazamo wao kwa Watu winginne ni kuwatwisha mizigo bila kuwajali.
Hivi Mwigulu kasoma uchumi gani?
Kati ya hao wenye Maoni walioko mtaani ni pamoja na wewe au? 😆😆😆,Mtanipasua kwa kichekoNikishasema humu tunaongozwa na viongozi wajinga na asilimia 90% ya watumishi wa umma ni incompitent ukilinganisha na wa nchi nyingine huko.
Walisima vizuri na wenye maonp wapo uraiani wanahenyeka, yale maboga ndo yamepewa nyadhifa kubwa.
Hebu kumbuka tu zile division four za 28 zilizokuwa zunaenda nursing na Clinical officers, ualimu, polisi na kazi nyeti nyinginezo, zimetuzalishia watumishi wangapi mambumbumbu ambao wapo kwenye system mpaka sasa?
Hao ndo wakina Mwigulu.
Yana nyonya wananchi haswaBora hata dikteta... hao si watu. Ni majangili au maharamia.
Mwigulu hajawahi kuwa na nia njema na yeyote na chochote!Yana nyonya wananchi haswa
Bia licha ya kuwa na inelastic demand lakini ina substitute na wazalishaji ni wengi kuliko cement..ooo ok, vita kaitaja kiujumla lakini sio specific kwenye cement. wajameni mbona bia hazipandi bei na ndio waathirika direct wa vita hii maana wakati mwingine hulazimika kuagiza shayiri nje ya nchi na nyingi inatoka hukohuko kwenye mchapano. Why?????!!!!???
Yeye kuna V8 haizimwi hata kwa dak 5 muda wote ipo silenceMwigulu hajawahi kuwa na nia njema na yeyote na chochote!
Bei tunajua imepanda... ila kila kitu kuisingizia Urusi na Ukraine ni upuuzi. Bila kutuambia nchi inafanya kujikwamua ni dalili za kushindwa uongozi!
Wapunguze matumizi yao ya anasa...
Inasafirishwa na uongo yenyewe?Bia licha ya kuwa na inelastic demand lakini ina substitute na wazalishaji ni wengi kuliko cement..
By the way malighafi na gharama za usafirishaji zimeongeza bei ya saruji..
Tumia common sense,kwa nini kitumbua kisipandeSasa hivi hata vitumbua vikipanda tutaambiwa vita vya URUSI
Hahaha. Inachekesha lakini wakati huo huo inatia hasira. Unawaomba wazalishaji wapunguze gharama!?
"...gharama za cement zimeendelea kupanda kila mara na hilo la vita ya Ukraine na Urusi ndilo limeongeza changamoto ya kupanda kwa bei..."
"...nimewataka wadau waone namna bora ya kupunguza gharama kupanda mara kwa mara kwa maslahi ya wananchi wetu."
Amesema Mwigulu.
Nb: Tanga cement na Dangote cement si mhamishie viwanda vyenu Tanzania ili bei ya cement ipungue?!
Umeuaa!Kasoma uchumi wa kuchumia tumbo.
Hivi kweli unapunguza bei ya cement kwa kutoa rai kwa makampuni husika? Watamsikiliza kweli? Inahitajika strategic revisions za monetary na fiscal policies. Mbolea, cement, nondo, mafuta ya kula vilipanda tangu mwaka Jana. Tunaambiwa Ukraine. Inatia hasiraAmesema na Taarifa ya Benny Mwaipaja inafafanua zaidi:
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ametoa rai kwa kampuni zinazozalisha saruji hapa nchini kuangalia gharama zao za uzalishaji ili kuleta nafuu kwa wananchi pamoja na Serikali inayohitaji saruji kwa wingi katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati ya ujenzi.
Dkt. Nchemba ametoa rai hiyo Jijini Dodoma, alipokutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Kampuni ya Afrisam ambayo ni mmoja wa wanahisa wakubwa wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga.
Aliishukuru kampuni hiyo kwa kufanikisha upatikanaji wa saruji kwa wakati katika utekelezaji wa mradi wa shilingi trilioni 1.3, Fedha za Uviko 19 na kuwaomba wazalishaji hao kufanya hivyo wakati huu ambapo bei ya vitu vinapanda kutokana na vita vinavyoendelea baina ya Urusi na Ukraine.
Alikumbushia jinsi ambavyo Wizara ya kisekta yaani Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, ilivyokaa na wawekezaji hao wakati wa kujenga madarasa na kuwaomba wasipandishe bei kwa sababu ya uhitaji mkubwa wa bidhaa hiyo uliokuwa umesababishwa na mahitaji ya ujenzi wa madarasa na walikubaliana kufanya hivyo bila kuongeza gharama zaidi.
Dkt. Nchemba alikumbushia pia hivi majuzi pale bei za vifaa vya ujenzi vilipopanda gharama, waliitikia tena wito wa Serikali wa kuwaomba waendelee kuangalia bei ya saruji na kusimamia gharama za uzalishaji.
“Rai yetu, haya mambo ya bei kuongezeka yanaendelea hasa baada ya kuja hili jambo jipya la vita vya Urusi na Ukraine, tuendelee kukabiliana na majanga ya namna hii huku tukiwajali wananchi masikini, sisi huku kwenye sekta ya uzalishaji tukichoka kubeba mzigo, wananchi wetu ambao ni watumiaji wa mwisho watachoka zaidi” alisisitiza Dkt. Nchemba.
Kuhusu masuala ya uwekezaji wao hapa nchini, ambayo ndiyo agenda iliyowapeleka kuzungumza naye, Dkt. Nchemba aliwahakikishia wawekezaji hao kwamba itawalinda na kuwajengea mazingira mazuri ya kufanyabiashara zao kwa kuwa ndio msisitizo mkubwa uliotolewa na Mkuu wa Nchi, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Dkt. Nchemba alieleza kuwa ili kuwezesha uwekezaji mkubwa uendelee kuja Tanzania, ni pamoja na kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji kwa ajili ya kuzalisha ajira na pia vyanzo vipya vya kodi ambavyo vitawapunguzia mzigo na kuwapatia fedha wananchi kwa ajili ya kufanya shughuli za maendeleo.
Kwa upande wake Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya AfriSam, Bw. Erick Diack, alisema kuwa kampuni yake ipo nchini tangu mwaka 1996 na imewekeza zaidi ya dola za Marekani milioni 190.2 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 55.7 kati ya mwaka 2009 hadi mwaka 2016.
Alisema kuwa Kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha tani milioni 1.2 kwa mwaka na katika kipindi kifupi kijacho wanakusudia kuongeza uwekezaji na ufanisi kwa kufunga mitambo mingine yenye uwezo mkubwa wa kuzalisha.
Ushamba huu alikua nao Saada Mkuya.Yeye kuna V8 haizimwi hata kwa dak 5 muda wote ipo silence
Kwa hiyo kwani sababu za kupanda hazikuwepo?Cement ilipanda kabla ya Vita kuanza.
Huixin 16000Kwani sasa hivi mfuko wa Cement unaenda sh.ngapi...?
Kwani Ukr haijachangia? Tuwekee hapa hizo strategic za monetary na fiscal policies 😆😆..Hivi kweli unapunguza bei ya cement kwa kutoa rai kwa makampuni husika? Watamsikiliza kweli? Inahitajika strategic revisions za monetary na fiscal policies. Mbolea, cement, nondo, mafuta ya kula vilipanda tangu mwaka Jana. Tunaambiwa Ukraine. Inatia hasira