Mwigulu: Elimu ya msingi ya lazima kuwa miaka 10

Dah, wastaafu wengine hapa mtaani nawaonea huruma kweli kweli.
Unajua kuna tofauti kubwa sana kati ya mfanyakazi mstaaf na mkuluma na kiumri wako sawa... Mkuluma anakua na furaha na amani (maisha yake yanaendelea kama kila siku, mstaaf anakaa akijua ameishiwa nguvu na umri umekwenda no maana haitajiki kazini, hivo anasubiri kufa. Na ndomaana wakistaafu wengi wao hawamalizi miaka mitano wanakufa kweli.
 
Hapa kuna mkanganyiko.
Mwanangu (std III) aliniambia kwamba elimu s/m mwisho std VI kisha watajiunga sekondari.

Mwigulu anatangaza s/m(lazima) ni miaka 10?! Je, hii inajumuisha miaka 6 ya s/m + miaka 4 ya o'level ndo ifike kumi?
Je, hii inamaanisha kwamba elimu ya o'level imejumuishwa kuwa elimu ya msingi?
Ndiyo maana yake.
Akimakiza elimu ya msingi darasa la 6 atapangiwa kidato cha kwanza shule ya sekondari awe amefaulu au amefeli.
Lazima asome hadi kidato cha 4.
Hakuna mambo ya zamani akifeli darasa la 7 anaenda kujifunza ufundi mtaani au VETA.
VETA hadi akimaliza kidato cha 4.
 
Unajua kuna tofauti kubwa sana kati ya mfanyakazi mstaaf na mkuluma na kiumri wako sawa... Mkuluma anakua na furaha na amani (maisha yake yanaendelea kama kila siku, mstaaf anakaa akijua ameishiwa nguvu na umri umekwenda no maana haitajiki kazini, hivo anasubiri kufa. Na ndomaana wakistaafu wengi wao hawamalizi miaka mitano wanakufa kweli.
Comfort zone inawamaliza.
 
Ndiyo maana yake.
Akimakiza elimu ya msingi darasa la 6 atapangiwa kidato cha kwanza shule ya sekondari awe amefaulu au amefeli.
Lazima asome hadi kidato cha 4.
Hakuna mambo ya zamani akifeli darasa la 7 anaenda kujifunza ufundi mtaani au VETA.
VETA hadi akimaliza kidato cha 4.
Hiyo kwamba "awe amefaulu au hajafaulu" nakataa.

Hapa kati lazima kuwe na mchujo ndiyo maana mitihani ya mchujo ya taifa imeongezwa kuanzia darasa la pili, la nne, la sita necta kubwa ambayo wahitimu bila shaka watapewa leaving certificate. Then sekondari mchujo upo form two.
Baada ya hapo watafanya mtihani wa kidato cha nne ambao ndo wa kupewa cheti cha taaluma kuhitimu elimu inayo tambulika.

Bila shaka kwa hapo kidogo itaeleweka vizuri.
 
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba akihitimisha bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu amesema kuwa elimu ya msingi sasa kuwa miaka 10

---
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba ametangaza kuanza kwa utekelezaji wa mfumo mpya wa elimu utakaofanya elimu ya msingi kuwa ya lazima kwa kipindi cha miaka kumi, akisema ni sehemu ya mageuzi makubwa yaliyofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akihitimisha hotuba yake ya bajeti bungeni, Dkt. Nchemba amesema mageuzi hayo ni ya kihistoria kwani mara ya mwisho mabadiliko makubwa ya mfumo wa elimu yalifanyika mwaka 1967, wakati elimu ya lazima ilipopanuliwa kutoka darasa la nne hadi la saba.

Amesema mabadiliko hayo hayaishii kuongeza muda wa masomo pekee, bali yanaambatana na maboresho ya kina yaliyokuwa yakihitajika kwa muda mrefu, ikiwemo kuboreshwa kwa mitaala na miundombinu ya elimu.

"Mheshimiwa Rais ameonyesha ujasiri mkubwa wa kufanya maamuzi haya bila kujali gharama ili kuhakikisha watoto wa Kitanzania wanapata elimu bora," amesema Dkt. Nchemba.

Ameeleza kuwa maandalizi ya utekelezaji wa mpango huo yamefanyika kwa kiwango kikubwa, huku hatua zilizobaki zikiendelea kukamilishwa ili kuhakikisha utekelezaji wake unakuwa wa mafanikio.

Katika kuimarisha elimu ya ufundi, amesema serikali imeongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya shule kutoka takribani tano zilizokuwepo awali hadi zaidi ya 300, zikiwemo shule za awali na za ufundi, ambapo nyingi zina mwelekeo wa masomo ya kihandisi.

Aidha, amesema ujenzi wa madarasa 79,000 umeondoa changamoto ya mfumo wa "second selection" uliokuwa ukiwanyima baadhi ya wanafunzi fursa ya kuendelea na masomo.
Mlipofikiria elimu ya msingi kuwa miaka 10 mlijaribu kufikiria nyongeza ya miaka ya kazini kustaafu?
 
Hiyo kwamba "awe amefaulu au hajafaulu" nakataa.

Hapa kati lazima kuwe na mchujo ndiyo maana mitihani ya mchujo ya taifa imeongezwa kuanzia darasa la pili, la nne, la sita necta kubwa ambayo wahitimu bila shaka watapewa leaving certificate. Then sekondari mchujo upo form two.
Baada ya hapo watafanya mtihani wa kidato cha nne ambao ndo wa kupewa cheti cha taaluma kuhitimu elimu inayo tambulika.

Bila shaka kwa hapo kidogo itaeleweka vizuri.
Darasa la 4, 6, na kidato cha 2 hiyo yote itakuwa Assessment Exams, Ila kidato Cha 4 na 6 hiyo ndiyo itakuwa mitihani ya mchujo wa wanaoendelea elimu ya juu zaidi ya madaraja hayo.
Hayo mengine ni mtazamo au maoni yako tu. Siyo haki halisi kwa mujibu wa mtaala mpya.
 
P/s miaka 6
S/s miaka 4
Jumla hiyo 10 waliyosema.
Watoto watamaliza elimu ya msingi darasa la 6. Darasa la 7 limefutwa.
Mtoto lazima asome hadi kidato Cha 4 iwe amefaulu au hajafaulu.
ahsante hapo umetuweka sawa maana ilikuwa ni mkanganyiko.. Mda lazma uheshimiwe
 
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba akihitimisha bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu amesema kuwa elimu ya msingi sasa kuwa miaka 10

---
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba ametangaza kuanza kwa utekelezaji wa mfumo mpya wa elimu utakaofanya elimu ya msingi kuwa ya lazima kwa kipindi cha miaka kumi, akisema ni sehemu ya mageuzi makubwa yaliyofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akihitimisha hotuba yake ya bajeti bungeni, Dkt. Nchemba amesema mageuzi hayo ni ya kihistoria kwani mara ya mwisho mabadiliko makubwa ya mfumo wa elimu yalifanyika mwaka 1967, wakati elimu ya lazima ilipopanuliwa kutoka darasa la nne hadi la saba.

Amesema mabadiliko hayo hayaishii kuongeza muda wa masomo pekee, bali yanaambatana na maboresho ya kina yaliyokuwa yakihitajika kwa muda mrefu, ikiwemo kuboreshwa kwa mitaala na miundombinu ya elimu.

"Mheshimiwa Rais ameonyesha ujasiri mkubwa wa kufanya maamuzi haya bila kujali gharama ili kuhakikisha watoto wa Kitanzania wanapata elimu bora," amesema Dkt. Nchemba.

Ameeleza kuwa maandalizi ya utekelezaji wa mpango huo yamefanyika kwa kiwango kikubwa, huku hatua zilizobaki zikiendelea kukamilishwa ili kuhakikisha utekelezaji wake unakuwa wa mafanikio.

Katika kuimarisha elimu ya ufundi, amesema serikali imeongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya shule kutoka takribani tano zilizokuwepo awali hadi zaidi ya 300, zikiwemo shule za awali na za ufundi, ambapo nyingi zina mwelekeo wa masomo ya kihandisi.

Aidha, amesema ujenzi wa madarasa 79,000 umeondoa changamoto ya mfumo wa "second selection" uliokuwa ukiwanyima baadhi ya wanafunzi fursa ya kuendelea na masomo.
Hivi huu mfumo wa elim wanasema watoto wa WM, W, CEO, au ni mfumo wa mama anaandaa chakula kwa baba asichokila yy? Maana si kwa hii big result now
 
Umeanza munaanzazahuu, wanafunzi ambao wako lasaba na lasita mwaka huu wanafanya mtihani pamoja. sasa sijui mwakani wanaendaje sekondari, na watasoma shule gani sijui

Na hao watakaofika lakumi sijui watasomea madarasa ya wapi kwa hiyo miaka minne ya juu iloongezeka.

Na shule za sekondari zitakua nakazi gani kwenye hiyo miaka minne wanayosubiri intake ya form one wa kwanza kutoka darasa la kumi.

Hivi unajua hivi vitu ukienda kumwambia mtu ambae hafuatilii mitandao na vyombo vya habari atasema unamuongopea. Maana najiona kama naandika pumba saana hadi naona aibu. Lakini ndo waheshimiwa wameamua hivi. INAFIKIRISHA sana
Mkuu mfumo tunaanza 2027 mwaka huu wameponea kwenye tundu la sindano.. huko mbele Elimu yetu ambayo wansosoma si watt wa viongozi waandamizi tusipoiwahi tutaikuta imefika antakitiki
 
Back
Top Bottom