Mwigulu, it's enough. You MUST resign!
Matajili walirudishiwa hela zilizokuwa zimelipishwa kabisa na mahakama na Ile bargaining ya dpp kumbe walijua namna za kuzifidia lol.
 
Unaacha kukusanya MABILLIONI kwa matajiri unakuja kukusanya BUKU BUKU uswahilini kwa wanyonge🤔

Serikali inaona mbali kamanda 🤣🤣 wakizichanga buku buku kwa vichwa milioni 5 kote nchini wana hela ndefu

Kwa mfano ukichukua 1000×5,000,000=Bilioni tano, nimetolea mfano kwa siku moja 🤣

Tunacheka utafikiri mazuri
 
Nchi hii walipa kodi wakubwa na wa uhakika ni watu laki 5 tu kati ya watu mil 60.

Hao matajiri unaotaka wakatwe kodi zaidi ndo wanaoendesha nchi literally na ndo watoa ajira wakubwa. Wanakamuliwa hadi cent ya mwisho.

Hatua zozote za kuendelea kuwakamua walipa kodi wakubwa kutaporomosha uchumi zaidi badala ya kusaidia.

Nchi inahitaji vyanzo vipya vya mapato na vyanzo vinavyogusa kila mtu katika ukusanyaji tena bila shurti sio matajiri tu. Sisemi makato ya miamala ya sasa ni sawa, nadhani inabidi yapitiwe upya, ila sio kila kitu kusukumia matajiri huku wengine hawalipi au wanalipa kiduchu.

Ni aibu wizara ya fedha na taasisi zake hawaji na vyanzo vipya zaidi ya pombe, mafuta na miamala miaka nenda rudi.
 
Mimi siamini kama mwigulun chemba anamsaidia mama Suluhu Samia kwa haya maboko anayoanzisha yanaudhi Sana wananchi nyuma ya pazia Kuna jambo.

Natesti mitamboView attachment 1855273
Nakuomba tena Mama yangu ufikirie tena hivi vimeo unavyochomekewa, na uwe makini navyo. Mafuta ndio "trigger" ya mfumuko wa bei wa bidhaa mbalimbali za muhimu. Na kwenye miamala ya tigopesa/mpesa ndio wengi wa kipato cha kati na chini hufanya miamala yetu, sababu hatuna hela za kuweza kukaa benki.
 
Unaacha kukusanya MABILLIONI kwa matajiri unakuja kukusanya BUKU BUKU uswahilini kwa wanyonge[emoji848]
Nakuomba tena Mama yangu ufikirie tena hivi vimeo unavyochomekewa, na uwe makini navyo. Mafuta ndio "trigger" ya mfumuko wa bei wa bidhaa mbalimbali za muhimu. Na kwenye miamala ya tigopesa/mpesa ndio wengi wa kipato cha kati na chini hufanya miamala yetu, sababu hatuna hela za kuweza kukaa benki.
 
Unaacha kukusanya MABILLIONI kwa matajiri unakuja kukusanya BUKU BUKU uswahilini kwa wanyonge🤔
JPM alikuwa anakusanya kwa vigogo, wapuuzi akina Tundu Lissu wakamsakama, sasa ngoja mama azisake kwenu wapigadebe.
 
Matajiri ni RAIA na wanalipa KODI pia......

Matajiri wameajiri watanzania wengi ambao kuishi kwao ,kulisha familia na kulea watoto hutegemea hao matajiri......

Wewe hutegemewi na watu wasiozidi 20 halafu ujifananishe na hao matajiri waajiri wa Watanzania?!!!

Tuache pang'ang'a tulipe KODI....

Mh.SSH ni rais wa maskini na matajiri pia......

#KaziIendelee
Wakati wanafanya maamuzi wanapaswa kuangalia sehemu Kuna uafadhali kwamba mhusika hata pata maumivu sana.

Matajiri Wana uafadhali kidogo wa kulipa kuliko maskini.

Kumminya mtu wa chini kwa makodi mengi na makubwa Kwa wakati mmoja huko ni kutengeneza civil unrest.
 
Back
Top Bottom