Izato
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 5,441
- 11,669
Ama kwa hakika madaraka hulevya. Inafedhehesha sana pale mtu aliyepewa nafasi ya uongozi wa juu serikalini anapojitoa ufahamu kuhusu uwepo wa kero ya utekaji iliyotamalaki kwa kiwango cha juu katika utawala wa Samia Suluhu.
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema hayo Mei 23, 2026 wakati akizungumza na wananchi katika Viwanja vya Kichangani kwenye ziara yake ya kikazi ya siku mbili.
"Tunagombanishwa mno. Watu wanapoteza muda hata wa kutafakari kila jambo, kwamba hili limetokeaje.
Unakaa hivi, unasikia sister katekwa. Unakaa hivi, si padri katekwa. Unakaa hivi, nimeona mwingine jana tena... nimeona pale... nimeona mtandaoni pale eti katekwa. Mnaangalia mtu kaumizwa, anapingu.
Hii ni ajenda maalum. Hii ni michezo. Hii ni michezo.
Na hii michezo haijaanza jana. Hii ni michezo haijaanza jana kwa Tanzania, tuamke! Hizi ni ajenda za watu wenye akili wanaolitafuta taifa letu. Ni ajenda za watu wenye akili, hii sio mpuzi mpuzi tu hivi."
Kwa makusudi kabisa anasema kwa dharau na kebehi, eti sister katekwa! Eti padri katekwa! Anakebehi madai ya TEC pale inapokemea tatizo hili.Anafanya unafiki hui ili kutaka kumfurahisha bosi wake mwenye chuki binafsi na misimamo ya TEC.
Mwigulu anajifanya hatambui chochote kile kuhusu matukio ya watu kutekwa au kupotea bila kujulikana, ambayo yamekuwa yakizungumziwa na kuripotiwa na ripoti mbalimbali.
Watekaji wameelezewa na baadhi ya viongozi wa kidini kama kikundi maalumu chenye kuhusiana moja kwa moja na maafisa serikali hasa kutoka TISS na jeshi la polisi.
Mwigulu anakwepa kwa makusudi kuutambua ukweli juu kadhia hii kupitia Tume ya Haki na Amani ambayo imeeleza wasiwasi wao kuwa utekaji huu unaathiri moja kwa moja haki ya msingi ya uhai ya wakosoaji wakuu wa serikali. Kinyume kabisa na matakwa ya Katiba kuhusu haki ya uhai na uhuru wa mtu wa kutoa maoni yake.
Mwigulu kwa kushupaza shingo na kutokana na kiburi cha uzima anaropoka hadharani na kupingana na msimamo wa serikali kwamba inachukua hatua dhidi ya uhalifu huu wa utekaji.
Kwa kuwa kero hii imekuwa moja ya hoja kubwa za kisiasa na kijamii, na kwa kuwa waathirika wengi ni makada wa CDM, basi ili kukwepa kuwajibika anaona ni vyema akatoa majibu rahisi rahisi akihusisha kero hii na propaganda na michezo ya maigizo.
Mwigulu! Mwigulu! Mwigulu! You have been used, misused, and abused. Now expect to be utterly confused.
Always do remember that, karma is a bitch.