Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President!-Nimeguswa!

Mwigulu anahubiri mambo ya misamaha mikubwa ya kodi na kodi za wajasiriamali wakati hata sasa hivi yupo wizara ya Fedha lkn hajafanya chochote,huyu mnafiki hana lolote tapeli huyu Mwigulu
 
tatizo ndani ya ccm hayo mambo ya ukawa hawawezi kuyakubali kamwe. mwigulu kazungumza mambo ya ukawa tupu.
Ni Mwigulu huyuhuyu huwa anapinga na kuponda Sera za UKAWA hasa CHADEMA kufa na kupona halafu leo tumuamini? Heri umuamini Malaya anayeuza mwili sio m....aya wa siasa.
 
Mwigulu hana lolote, anacheza na psychology ya watu, ndo maana alianza kuuelezea umasikini, akijua watu wengi wamepitia maisha yale, hivyo watasympathize nae, na amewapata. Wanasiasa wajanja sana! Lakin tukiangalia kwani viongozi wote waliopita na waliopo nani hajapitia maisha yale? Mtu kama mkapa aliekulia kusini kwenye umasikini wa kutisha mbona hakuja na style ya kuuelezea umasikini wake kama mwigulu? Utakuja kuona ni strategy. Lowassa mwenyewe nae kakulia familia ya kimasikini na kifugaji kama mwigulu, nae alie kama mwigulu? Umasikini wa umasaini na life style yao ni mbaya zaidi ya kina mwigulu. Hivyo strategy yake kwangu haina mashiko. Tatizo mtu yoyote wa ccm hawezi kubadili system iliyoko ndani ya CCM, nyerere mwenyewe alishindwa, sidhani kama huyu aje na maajabu yoyote. Watanzania kila ikifika uchaguzi wanaaminishwa na ccm kuwa kuna mtu amekuja kuleta mabadiliko! Lakini wanasahau ni uzao uleule wa nyoka. Kazi tulionayo ni kuibadili system, ccm inabidi iondoke, haijalishi anakuja nani na uongo upi...
 
Tuache ujinga na unafiki hapa, Mwigulu hafai na hana uwezo wowote wa kuwa mgombea Urais wa CCM, Kwa sababu alikuwa akilalamika, kukosoa tu mfumo wa sasa wa serikali na CCM na wakati huo huo akisahau kuwa yeye pia ni kiongozi wa juu wa serikali na CCM.

Yote kwa yote ameshindwa kujitetea kabisa kuhusu kashfa zinazomkabili mbele ya watanzania kama
1/Bomu la Arusha
2/Ushahidi wa kutengeneza kuhusu Ugaidi wa CHADEMA
3/Ushiriki wa kihuni katika bunge la katiba
4/Ahadi ya kuwakamata wasiolipa kodi katika wizi wa ESCROW
5/Kushindwa kutatua mgogoro wa wafanyabiashara kuhusu mashine za kukusanya kodi.
6/Kushindwa kuishauri serikali kuhusu kushuka vibaya kwa thamani ya shilingi.
7/Kushindwa kupambana na mafisadi bungeni, katika serikali na ndani ya CCM.
 

Kuchanganyana tuu
 
Pasco Sio wewe tu hadi sasa kati ya watangaza nia mwigulu yuko juu ngoja tuendelee kuona tatizo mfumo Wa ccm unaharibu viongozi wazuri ambao huwa tunawaamini ndio hapo sasa ninapoichukia ccm na yeyote aliye ndani ya ccm. Nimeweka ushabiki pembeni

Unamfahamu vizuri huyo jamaa kama jimbo lake limemshinda nchi ataiweza?
 
Jana kaongea kama mjumbe wa UKAWA,tatizo lake wakiyasema kina Mnyika wanaonekana wasaliti,hata kuunga mkono hoja ya upinzani inakuwa dhambi kwao,sasa jana ameyarudia yote!!
 
MWALIMU Nyerere daima nitakukumbuka.Ule msemo wa Watanzania tunahitaji mabadiliko umeshatimia,tumeyakosa CCM tutayapata sehemu nyingine nayo ni UKAWA tu.Tuliona nafasi adimu wanazozipata hawataki kuzitumia.Hivyi suala la RICHMOND mpango wa VUA GAMBA ugetekelezwa nani angewasema vibaya CCM? likaja suala la EPA nayo ilikuwa nafasi adimu ya kuonyesha mnavyochukia rushwa mlivyolimaliza walioiba mabilioni hasa jamaa wa kiasia kesi zao zikaishia kwa JK sisi vibaka tulioiba kuku mwaka huo baado tumo gerezani.Likaja suala la TEGETA ESCROW hadi Ikulu ikahusishwa Mpigaji wetu CHENGE na kundi lake wakaibuka tena,Mwigulu akasema waliotupiga hata kodi hawajalipa hadi leo.MABADILIKO YA KWELI HAYATATOKA CCM yatatoka UKAWA,kubaki IKULU CCM labda mbinu chafu za Katiba Pandikizi zitumike na za JIRANI YENU NKURUZINZA
 
Kaiza safari kwa kuwajibu maasimu wake, hajaonesha njia za kupita, binafsi nampongeza Wasira
 
That's it. You nailed it
 

Kuna msemo wa kielimu unasema "UMAHIRI WAKO ONYESHA KWENYE MAANDISHI"
Mkuu....umeandikaa....umechambua....
 
Jamaa kaipiga madongo serikali kisawasawa! Yaani utafikiri yeye siyo waziri wa serikali na pia ndo katoka kujiuzuru unaibu katibu mkuu wa ccm!
 
Kama wakitokea watafiti wengine tena kuja kupima IQ za watanzania, atapata shock result maana atashangaa kutokuona hata hizo IQ zenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…