expirience man
JF-Expert Member
- Nov 16, 2013
- 214
- 104
Mwigulu ni opportunistic populist tu.
We ulitaka aseme nini ama afanye nini usimuone opportunistic kaka. Acha huo uzombi jamaa kafanya poa sana zaidi ya wote waliotangaza nia mpaka sasa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwigulu ni opportunistic populist tu.
Mkuu, Nafikiri swali ni je unaweza kuthibitisha kwa ushahidi usio na shaka kuhusu hayo machache. Kisha tunaweza kujadili hayo mengi.
Hii ni fursa yetu wapiga kura kuwajua hawa watu vyema
Jibu swali wewe
Imetulia hii Mpwa. Umekaa na kufanya yako kwa hekima na busara kubwa, hongera sana. Baadhi ya Watanzania ni wakurukupukaji kupita kiasi sijui kwanini huwa hawapendi kutafakari kwa kina kabla ya kukurupuka na kuandika yale ambayo hayastahili kuandikwa.
Tutaendelea kufanya makosa ya kuwapa mdaraka wasiostahili mpaka lini!? Kwanini hatutaki kujifunza kupitia makosa yetu ya miaka ya nyuma ili kuinusuru nchi yetu ambayo ilitakiwa iwe na maendeleo makubwa sana lakini inayumba miaka nenda miaka rudi kutokana na viongozi wasio na sifa hata moja ya kuliongoza Taifa letu, wezi, wanafiki, majangili, wauza unga, wapokea rushwa, waongo, wahuni n.k. Dah! inauma sana kuwasoma baadhi ya watu humu kwa jinsi wanavyokurupuka kila siku iendayo kwa Mungu.
Ata kwa Lipumba ujaona jipya,maana nae KatangazaBado sijajisikia hata msisimko kwa wote waliotangaza nia mpaka sasa .ile waooooooo waooooo waoooo na misisimko ya ngozi kwa kusikiliza hotuba bado sijapata .japo kiduchu mwigulu alitaka kunisisismua lakini kila nikimuangalia sura yake na maongezi yake ni tofauti.mpaka sasa tarehe 31 hatujapata msalary wa mwezi wa tano.sikui kama ataweza kuongoza nchi wakati a
Kawizara kadogo ka fedha kamemshinda.
Lowassa watu hawampendi yeye, wanapenda fedha zake, kuwa mkweli Pasco.
Kibaya zaidi mkutano wa Jana Arusha umemvua nguo kabisa Lowassa kwa wale waliokuwa katikati.Mimi binafsi hata leo hii huyu bwana Lowassa asafishwe Richmond, simpi kura yangu kwa kuwa ni visionless, tired and outdated.
Hata akiwa most genuine tatizo mfumo wa ccm inawenyewe subirini mwicho wa mchakamchaka
Mimi sikuweza kusikiliza hotuba ya Mwigulu kwa muda mfupi lakini niseme kwa dakika hizo kama tano hivi alinivutia mno....anajieleza kwa ufasaha na anamiliki jukwaa. I was very very very disappointed na Comrade Lowassa jana. Jamani kuna nini kumuhusu Lowassa?! Yaani alishindwa kabisa kulimiliki jjukwaa. Speech yake ilikuwa imeandaliwa na anasoma utadhani mkuu wa mkoa au wilaya anasoma hotuba mbele ya Rais. Wasaidizi wake walishindwa hata kuandaa jukwaa na vipaza sauti. Kila muda walikuwa wanagonga gonga vipaza sauti...Lowassa aliomba wimbo gani ule wa Komba lakini haukutokea...Sijui nani yule alikuja na helikopta....aliyepaswa kuja na helikopta ni Lowassa na sio mwingine. Yaani wasaidizi wake hata protocol hawajui. Lowassa ameshafika jukwaani mwingine anaingia na helikopta what is that????? yaani wasaidizi wake wanapita pita jukwaani mara kibonde mara yule aliyevaa kofia kama ya kinana. hawakujiaandaa It is a disaster kwa Lowassa It is possible wanamhujumu. Kwanini Lowassa asiwe na tmu nzuri? Yaani akiingia kwenye mdahalo......
Itakuwa Pasco alitegemea atapewa kazi ya kigawa vibahasha kwa Lowassa akapigwa chini.
Inabidi ajaribu bahati yake kwa Mwigulu.
Tukirudi kwenye mada, ni mapema sana ku judge, ngoja na wengine wote wanaojinadi watakapoisha.
Wanabodi,
Tuweke ushabiki pembeni, kati ya watangaza nia watatu kati ya jana na leo, Mwigulu Lameck Nchemba is the most bonafide genuine mgombea so far, ukimuangalia huku unamsikiliza, utaiona his genuinity kutoka moyoni mwake ku practice what he preach na kiukweli nadhani kwa kati ya hawa watangaza nia so far, naamini Mwigulu can make the best president this nation has ever had tangu mwalimu Nyerere!.
Jee wewe mwenzangu ulibahatika kumsikia, unamuonaje?!.
NB Ku make the best president ni jambo moja, mgombea anayependwa zaidi so far ni Edward Lowassa, na mgombea the most experieced so fat ni Stephen Wasira, nikichukulia mchakato wa 2005 wakati JK alipochaguliwa, kama reference, assuming hawa watatu ndio wameingia tatu bora, Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wakipewa choice ya kuchagua between "the most loved", "the most experienced" and the "the best president", watachagua mtu anayependwa na watu, mtu atakayechagulika kwa urais na kuwatupa the rest, na hivi ndivyo JK alivyochaguliwa ile 2005 kwa sababu kwenye the finalist watatu, kulikuwa na "the most experienced" Dr. Salim, "The best Brain", Prof. Mwandosya, na "the good looking" Jakaya Kikwete, akapitishwa kwa hoja kuwa ndiye anayependwa na watu, as if mapenzi ya watu ndio uongozi wa nchi!.
JF has a role to play kuwaelimisha wananchi wetu waweze kufanya informed decisions kwenye choice of president, ili ifike mahali chaguo la mgombea wa CCM sio lazima ndio automatikally awe rais, wakituletea ule ujinga ujinga kama wa 2005, tunapiga tuu chini only if huko kungine kuna the better alternative!.
Ushauri wangu wa kwanza kwa wana JF, Mwingulu Nchemba is the man to keep watching seriously!.
NB. Kwa walionidhania mimi niko kambi fulani, uzi huu ni uthibitisho kuwa Pasco wa jf, hana chama, hana kambi, hana mtu, ila kuna watu anawakubali akiwemo yule 'jamaa yetu', hivyo sitarajii kuulizwa kama nimehama kambi kwa sababu sijawahi kuwepo kambi yoyote!.
Kiukweli mimi Pasco wa jf, nimeguswa na Mwigulu Nchemba!.
Vipi wewe?.
Pasco
Mwigulu tatizo ni huo upande aliopo..
"kutokana na umuhimu wa hii hutoba naomba niisome" EL, May 30, 2015 Arusha.
Yule mzee wa jana maskini hata ubongo haumruhusu kukariri tena, akaamua kutusomea maandishi tu teh teh teh