Wanabodi,
Tuweke ushabiki pembeni, kati ya watangaza nia watatu kati ya jana na leo, Mwigulu Lameck Nchemba is the most bonafide genuine mgombea so far, ukimuangalia huku unamsikiliza, utaiona his genuinity kutoka moyoni mwake ku practice what he preach na kiukweli nadhani kwa kati ya hawa watangaza nia so far, naamini Mwigulu can make the best president this nation has ever had tangu mwalimu Nyerere!.
Jee wewe mwenzangu ulibahatika kumsikia, unamuonaje?!.
NB Ku make the best president ni jambo moja, mgombea anayependwa zaidi so far ni Edward Lowassa, na mgombea the most experieced so fat ni Stephen Wasira, nikichukulia mchakato wa 2005 wakati JK alipochaguliwa, kama reference, assuming hawa watatu ndio wameingia tatu bora, Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wakipewa choice ya kuchagua between "the most loved", "the most experienced" and the "the best president", watachagua mtu anayependwa na watu, mtu atakayechagulika kwa urais na kuwatupa the rest, na hivi ndivyo JK alivyochaguliwa ile 2005 kwa sababu kwenye the finalist watatu, kulikuwa na "the most experienced" Dr. Salim, "The best Brain", Prof. Mwandosya, na "the good looking" Jakaya Kikwete, akapitishwa kwa hoja kuwa ndiye anayependwa na watu, as if mapenzi ya watu ndio uongozi wa nchi!.
JF has a role to play kuwaelimisha wananchi wetu waweze kufanya informed decisions kwenye choice of president, ili ifike mahali chaguo la mgombea wa CCM sio lazima ndio automatikally awe rais, wakituletea ule ujinga ujinga kama wa 2005, tunapiga tuu chini only if huko kungine kuna the better alternative!.
Ushauri wangu wa kwanza kwa wana JF, Mwingulu Nchemba is the man to keep watching seriously!.
NB. Kwa walionidhania mimi niko kambi fulani, uzi huu ni uthibitisho kuwa Pasco wa jf, hana chama, hana kambi, hana mtu, ila kuna watu anawakubali akiwemo yule 'jamaa yetu', hivyo sitarajii kuulizwa kama nimehama kambi kwa sababu sijawahi kuwepo kambi yoyote!.
Kiukweli mimi Pasco wa jf, nimeguswa na Mwigulu Nchemba!.
Vipi wewe?.
Pasco