mimi nadhani Mwigulu hakujua kama atakuja kumbea urais hadi alipojiona ni maarufu ghafla,
1. angejua asingekuwa anaropoka au kutoa kauli chafu tena kana kwamba sio msomi.
mfano ccm ni ng'ombe wananchi ni ndama. mkikataa kutujagua udiwani mtakufa maana tutagoma kuwanyonyesha. Ni kazi ya srikali kumuudumia kila mwananchi bila kujali dini wala itikadi. ulitereza hapo mkuu.
2. Kama raia mwema kudai kuwa anaushahidi wa ugaidi huku akishindwa kuupeleka polisi, tena hata polisi kumuhoji ni udhaifu na kutafuta umaarufu mwepesi wa kisiasa.
3. kama Mwanasiasa mzarendo hakupaswa kuongea yale ambayo huwa anayapinga kisa kutetea ccm hashindwi kutetea mafisadi akiwa rais. Kigeugeu.
4. Herikopta ya msukuma ndio aliitumia kujitafutia umaarufu kule moro, wakati huohuo huyo jamaa ni mfuasi mkubwa wa EL. inanipa picha kuwa kuna uwezekano hawa lao ni moja.
5. Bingwa wa siasa chafu, Kutembea na Mtu aliyemwagiwa tindikali ili kuwatisha wananchi ubaya wa wapinzani wakati alipaswa kuwaeleza nini SERA zake na atatekeleza vipi.
6. Kama ukiwa na elimu ya Masters ulishindwa kubuni njia ya kisomi ya kujipatia Kipato (labda kama ulisoma elimu mbaya) ukaenda kubeba zege, nilitegemea labda ufanye kazi ya kuandika proporsals, projects, au hata kutafuta nafasi ya kufundisha ktk mamia ya shule hapo jijini,. utawezaje kubuni miradi au mawazo ya kuondoa umasikini kwa graduates hususani kipindi ambacho hata kupata internship ni kazi.(msoni ni yule anayetumia elimu yake kujikwamua kimaisha kwa mtazamo wangu mimi ambaye sijaenda shule)
7. Siku moja ukiwa umejaa jazba bungeni ulitamani kupata japo nafasi ya urais ili uwashughulikie wapinzani na watu waliokuwa na mawazo tofauti na yako. Hadi ukasiema usingekuwa waziri ungeongea maneno mabaya zaidi(jinsi nilivyokuelewa). Sasa ilinitisha kidogo kwa jaribu dogo tu lilikutoa kwenye mstari, je ukikabidhiwa nchi?? You need time to convince people that you are new Mwigulu.
Maoni yangu: Mwigulu wa leo sio kama wa miaka iliyopita. Unaonekana unakuja kama mkombozi lakni inabidi upate muda tujiridhishe vizuri kama kweli umebadilika au unatumia sifa mbaya ya USAHAULIFU wa wachache kutimiza malengo yako kisiasa.
yote kwa yoe, Nakupongeza kwa kutangaza lakini fanya marekebisho, kama unafaa siku ikifika utakuwa.