PostGE2025 Mwigulu: Mnataka tuseme idadi ya waliokufa kwani tunafanya sherehe ya vifo?

PostGE2025 Mwigulu: Mnataka tuseme idadi ya waliokufa kwani tunafanya sherehe ya vifo?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Na kuna kima bado ziliendelea kutega masikio na kunakili uharo wa huyo savimbi?!

Mwigulu anawajua baadhi ya polisi wauwaji waliohusika MO29. Task force ya wauwaji ndani ya polisi na TISS anawafahamu na aliwatumia sana kipindi akiwa waziri wa mambo ya ndani.
 
Yaani zinatajwa kila kitu ila hakuna kutaja idadi, ilitajwa idadi ya waliokufa kwwnye mv bukoba, ajali train kule Dodoma idadi ilitajwa, japokuwa na yenyewe namba zilipikwa, leo kutaja idadi ya waliokufa kwwnye maandamano ndio inamaanisha watu wanasherekea mauaji yaliyotokea?🤣🤣 Mwigulu, Watanzania sio wajinga sana.... eti nimekuwa imshono sana, na wewe ndugu wa Mc Pilipili wanakuzoom tu.... nachoka mimi mkwe wa Mwandambo!

====

Mwigulu amesema:

Tunaongelea maisha ya watu, ytunaongelea watu kupoteza wapendwa wao, haya si majengo, nchi ya aina gani ya kucelebrate maisha ya watu? Inabidi tuweke miiko, mtu amepotelewa na mpendwa wako wewe unapost?

Kwanini tunataka kushereka watu kupotea, nilidhani tukubali jambo kutokea, lakinintuko bize tunataka tuanze kuhesabu kama watoto wamezaliwa, mnataka tuanze kuhesabu kama mafanikio, mnataka tuhesabu kama magari, maisha ya watu?

Na wengine wanataja tu, hawako hatya hapa wanasema ni idadi hii, sehemu nyingine miili inawekwa kwenye plate number za magari ambako si za nchi hii, kuna sehemu mpaka taasisi ikaomba radhi kuwa picha iliyopostiwa si ya nchi hii.

Tunakubali kuwa kuna vifo vimetokea lakini tuheshimu familia walizopotezwa wapendwa wao, tuwape breki familia na haya. Ningetamani kuweka staha sana kwenye mambo yanayohusisha maisha ya watu. Kwasababu tume imeundwa tutoe nafasi ili tupaje mambo kwa uhakika.

Wanaofanya hili kama sherehe kuna jambo wanataka.
Kutotaja Namba waliofariki ni kuto thamini Uhai wa hao waliofariki kuulinganisha na vitu au Mali alizozitaja
 
Waziri mkuu yuko Sahihi kutaja idadi ya waliokufa ni sawa na kusherekea vifo
Mv bukoba ilitajwa waliokufa ni 800 ajali ya treni miaka ile ilitajwa waliokufa ni 200+

Kwann leo mnapatwa na kigugumizi kutaja maelfu ya watu mliowaua??!!.

Hili mnalo na ndio mwanzo wa anguko lenu, wananchi wa leo wengi wanajitambua wanawachora tu!!.
 
Mbona idadi ya waliofariki kwa Covid walitoa, malaria wanatoa? Waliokufa kwa ajali za barabara wanataja? Hua wanasherehekea nini?
Watanzania sio wajinga, wauaji wajiandae kwenda ICC
Vifo vya Covid ilikuwa wanatoa update kabisa kila baada ya mda na idadi ya wagonjwa. Basi kulikuwa na sherehe kila baada ya mda flani..kwa tafsiri yake
 
IMG-20251128-WA0000.jpg
 
Back
Top Bottom