Mwigulu na Watoto Wake (Joshua na Isack) Jukwaani, Je ni mkakati wa kulinda Legacy ya Kisiasa?

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Habari wakuu,

Jana nimeona watoto wa Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba wakivutia mjadala mkubwa mtandaoni baada ya baba yao kuwapa nafasi ya kuzungumza jukwaani. Miongoni mwao, Isack tayari anafahamika kwa kuwa ameonekana mara kadhaa kwenye majukwaa ya kisiasa.

Tangu tukio hilo, kumekuwa na maoni mbalimbali mitandaoni. Wapo wanaoamini kuwa hatua hiyo ni sehemu ya kuwaandaa vijana hao kuingia rasmi kwenye siasa, huku wengine wakiona ni jambo la kawaida kwa mzazi kuwapa nafasi watoto wake kujitokeza hadharani.

Kwa mtazamo wangu, huenda Mwigulu ameanza kufikiria namna ya kuendeleza ushawishi na urithi wake wa kisiasa katika eneo la Wanyiramba. Sababu ni kwamba, kwa nafasi yake ya sasa na mwenendo wa siasa za CCM, si rahisi kuona akiwa miongoni mwa viongozi wa juu wa chama kwa muda mrefu sana ujao.

Nakumbuka aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, aliwahi kueleza kuwa kwa utamaduni wa chama hicho, viongozi waliowahi kuwa Makamu wa Rais au Waziri Mkuu au Spika wa Bunge mara nyingi hawajawahi kufanikiwa kupata uteuzi wa mwisho wa kugombea urais kupitia chama. Ukiangalia historia ya CCM, hoja hiyo inaonekana kuwa na uzito wake.

Zaidi soma Humphrey Polepole: Kama ulishakuwa Spika, Waziri Mkuu, au Makamu wa Rais hutakiwi kugombea urais

Kutokana na mazingira hayo, najiuliza kama Mwigulu ameanza mapema kuandaa kizazi kitakachoendeleza ushawishi wake wa kisiasa baada ya yeye kupunguza shughuli za kisiasa za kitaifa.

Swali la msingi ni hili: Je, watoto wa viongozi wakuu wana nafasi kubwa zaidi ya kutoboa kisiasa kutokana na majina ya wazazi wao, au mwisho wa siku ni uwezo wao binafsi ndio unaoamua hatima yao?

Karibuni kwa mjadala.

Pia soma > Ndoto za Mwigulu Nchemba kuwa Rais wa JMT zimezimwa rasmi leo kama ilivyotarajiwa
 
Watawala hawa wa sasa hivi wataachia msala mzito watoto na wajukuu wao kwani Damu za Watanganyika zaidi ya 10,000 zilizomwagwa ili wao wawe madarakani lazima zitalipiwa kisasi. Wangekuwa na akili wangewaepusha watoto wao na kujihusisha na siasa kwani ni kama wanawaandalia kitanzi.
 
Habari wakuu,

Jana nimeona watoto wa Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba wakivutia mjadala mkubwa mtandaoni baada ya baba yao kuwapa nafasi ya kuzungumza jukwaani. Miongoni mwao, Isack tayari anafahamika kwa kuwa ameonekana mara kadhaa kwenye majukwaa ya kisiasa.

Tangu tukio hilo, kumekuwa na maoni mbalimbali mitandaoni. Wapo wanaoamini kuwa hatua hiyo ni sehemu ya kuwaandaa vijana hao kuingia rasmi kwenye siasa, huku wengine wakiona ni jambo la kawaida kwa mzazi kuwapa nafasi watoto wake kujitokeza hadharani.

Kwa mtazamo wangu, huenda Mwigulu ameanza kufikiria namna ya kuendeleza ushawishi na urithi wake wa kisiasa katika eneo la Wanyiramba. Sababu ni kwamba, kwa nafasi yake ya sasa na mwenendo wa siasa za CCM, si rahisi kuona akiwa miongoni mwa viongozi wa juu wa chama kwa muda mrefu sana ujao.

Nakumbuka aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, aliwahi kueleza kuwa kwa utamaduni wa chama hicho, viongozi waliowahi kuwa Makamu wa Rais au Waziri Mkuu mara nyingi hawajawahi kufanikiwa kupata uteuzi wa mwisho wa kugombea urais kupitia chama. Ukiangalia historia ya CCM, hoja hiyo inaonekana kuwa na uzito wake.

Kutokana na mazingira hayo, najiuliza kama Mwigulu ameanza mapema kuandaa kizazi kitakachoendeleza ushawishi wake wa kisiasa baada ya yeye kupunguza shughuli za kisiasa za kitaifa.

Swali la msingi ni hili: Je, watoto wa viongozi wakuu wana nafasi kubwa zaidi ya kutoboa kisiasa kutokana na majina ya wazazi wao, au mwisho wa siku ni uwezo wao binafsi ndio unaoamua hatima yao?

Karibuni kwa mjadala.
Gentleman,
Rais Donald Trump ana mpa fursa na nafasi mwanae Trump Jr.kadiri anavyoona inafaa, Elon Musk yuko bega kwa bega na mwanae kwenye maeneo ya biashara na siasa za Marekani hadi siku moja alikua ikulu na kidogo aharibu mambo.

Lakini,
hivi rais wa Korea Kaskazini asingekua anampa mwanae ambae ni Rais hivi sasa fursa na nafasi za mazoezi kinadharia na kivitendo katika platforms mbalimbali za kisiasa, angekua na confidence ya kukubali kuiongoza Korea Kaskazini kweli?

Unakumbuka mjadala kuhusu nani aiongize DRC, baada ya kuuawa kwa Laurent D. Kabila, babake na Joseph Kabila rais mstaafu wa DRC, anaesapoti M23 na anaechezea kibano cha vikwazo vya Marekani?

Kabila Jr,
angekua anapata sapoti ya babake tangu utotoni, wala kusingekua na mjadala dhidi ya uwezo wake kuiongoza DRC.

Mamba hazai Kenge my friends, ladies and gentlemen.
Mwanasiasa anazaa wanasiasa wengi kadiri anavyojaaliwa.

Tuwalee watoto wetu na tuwakuze kadiri tupendavyo wawe. Lakini tusaport ndoto na matamanio ya watoto wetu kadiri wanavyotamani wawe.🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Acha makasiriko kijana...

Yohana 5:19

"Basi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Mwana hawezi kufanya neno lolote peke yake, ila yale tu anayoyaona Baba akifanya; kwa kuwa kila lile Baba analofanya, Mwana hulifanya vivyo hivyo."
 
Acha na Trump, Tanzania atufikii hata robo ya Demokrasia ya Marekani. Turudi hapa Tanzania, niambie kiongozi wa ngazi ya juu ambaye alikuwa anatoa platform kwa wanae kama afanyavyo Mwigulu?

Hayo mambo atakuwa anaiga kwa Samia.
 
Ezekieli 18:20

Mwana hatachukua uovu wa baba yake, wala baba hatachukua uovu wa mwanawe...
 
Habari wakuu,

View attachment 3607555

Jana nimeona watoto wa Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba wakivutia mjadala mkubwa mtandaoni baada ya baba yao kuwapa nafasi ya kuzungumza jukwaani. Miongoni mwao, Isack tayari anafahamika kwa kuwa ameonekana mara kadhaa kwenye majukwaa ya kisiasa.

Tangu tukio hilo, kumekuwa na maoni mbalimbali mitandaoni. Wapo wanaoamini kuwa hatua hiyo ni sehemu ya kuwaandaa vijana hao kuingia rasmi kwenye siasa, huku wengine wakiona ni jambo la kawaida kwa mzazi kuwapa nafasi watoto wake kujitokeza hadharani.

Kwa mtazamo wangu, huenda Mwigulu ameanza kufikiria namna ya kuendeleza ushawishi na urithi wake wa kisiasa katika eneo la Wanyiramba. Sababu ni kwamba, kwa nafasi yake ya sasa na mwenendo wa siasa za CCM, si rahisi kuona akiwa miongoni mwa viongozi wa juu wa chama kwa muda mrefu sana ujao.

Nakumbuka aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, aliwahi kueleza kuwa kwa utamaduni wa chama hicho, viongozi waliowahi kuwa Makamu wa Rais au Waziri Mkuu au Spika wa Bunge mara nyingi hawajawahi kufanikiwa kupata uteuzi wa mwisho wa kugombea urais kupitia chama. Ukiangalia historia ya CCM, hoja hiyo inaonekana kuwa na uzito wake.

Zaidi soma Humphrey Polepole: Kama ulishakuwa Spika, Waziri Mkuu, au Makamu wa Rais hutakiwi kugombea urais

Kutokana na mazingira hayo, najiuliza kama Mwigulu ameanza mapema kuandaa kizazi kitakachoendeleza ushawishi wake wa kisiasa baada ya yeye kupunguza shughuli za kisiasa za kitaifa.

Swali la msingi ni hili: Je, watoto wa viongozi wakuu wana nafasi kubwa zaidi ya kutoboa kisiasa kutokana na majina ya wazazi wao, au mwisho wa siku ni uwezo wao binafsi ndio unaoamua hatima yao?

Karibuni kwa mjadala.

Pia soma > Ndoto za Mwigulu Nchemba kuwa Rais wa JMT zimezimwa rasmi leo kama ilivyotarajiwa
Aliyemshauri kufanya hivyo amewakosea sana hao watoto!
 
Acha na Trump, Tanzania atufikii hata robo ya Demokrasia ya Marekani. Turudi hapa Tanzania, niambie kiongozi wa ngazi ya juu ambaye alikuwa anatoa platform kwa wanae kama afanyavyo Mwigulu?

Hayo mambo atakuwa anaiga kwa Samia.
my first born floriana ni miongoni mwa wanasiasa chipkizi wanaokuja juu kuanzia chini, achilia mbali Kikwete kwa Ridhiwani au Mwigulu kwa kijana wake.

Binti yangu I'm sure, atakua among powerful figures in this country ukiachilia mbali florian ambae nae ana moto wa kisiasa mno but nampushi zaidi awe daktari 🐒
 
CCM kimegeuka chama cha kisultan
 
Kuwaandaa siyo kosa lakini wao wanawaandaa hadi na namna ya kuwaibia waganganyika maliasili zao.
 
Ezekieli 18:20

Mwana hatachukua uovu wa baba yake, wala baba hatachukua uovu wa mwanawe...

Methali 22:6​

“Mfundishe mtoto njia impasayo; naye hataiacha hata atakapokuwa mzee.”

Kumbukumbu la Torati 24:16
“Wazazi wasiuawe kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasiuawe kwa ajili ya wazazi wao; kila mtu atauawa kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe.”
 
Leo tena hapa kiomboi, watoto wanastruggle sana kugain confidence mbele za hadhira

Habari wakuu,

Jana nimeona watoto wa Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba wakivutia mjadala mkubwa mtandaoni baada ya baba yao kuwapa nafasi ya kuzungumza jukwaani. Miongoni mwao, Isack tayari anafahamika kwa kuwa ameonekana mara kadhaa kwenye majukwaa ya kisiasa.

Tangu tukio hilo, kumekuwa na maoni mbalimbali mitandaoni. Wapo wanaoamini kuwa hatua hiyo ni sehemu ya kuwaandaa vijana hao kuingia rasmi kwenye siasa, huku wengine wakiona ni jambo la kawaida kwa mzazi kuwapa nafasi watoto wake kujitokeza hadharani.

Kwa mtazamo wangu, huenda Mwigulu ameanza kufikiria namna ya kuendeleza ushawishi na urithi wake wa kisiasa katika eneo la Wanyiramba. Sababu ni kwamba, kwa nafasi yake ya sasa na mwenendo wa siasa za CCM, si rahisi kuona akiwa miongoni mwa viongozi wa juu wa chama kwa muda mrefu sana ujao.

Nakumbuka aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, aliwahi kueleza kuwa kwa utamaduni wa chama hicho, viongozi waliowahi kuwa Makamu wa Rais au Waziri Mkuu au Spika wa Bunge mara nyingi hawajawahi kufanikiwa kupata uteuzi wa mwisho wa kugombea urais kupitia chama. Ukiangalia historia ya CCM, hoja hiyo inaonekana kuwa na uzito wake.

Zaidi soma Humphrey Polepole: Kama ulishakuwa Spika, Waziri Mkuu, au Makamu wa Rais hutakiwi kugombea urais

Kutokana na mazingira hayo, najiuliza kama Mwigulu ameanza mapema kuandaa kizazi kitakachoendeleza ushawishi wake wa kisiasa baada ya yeye kupunguza shughuli za kisiasa za kitaifa.

Swali la msingi ni hili: Je, watoto wa viongozi wakuu wana nafasi kubwa zaidi ya kutoboa kisiasa kutokana na majina ya wazazi wao, au mwisho wa siku ni uwezo wao binafsi ndio unaoamua hatima yao?

Karibuni kwa mjadala.

Pia soma > Ndoto za Mwigulu Nchemba kuwa Rais wa JMT zimezimwa rasmi leo kama ilivyotarajiwa
Kuna post hapa iliwahi kuandikwa about this, viongoz wanaweka watoto wao kwenye positions wakati chawa wataendelea kusifu na kuabudu for the rest of their life, na watoto wao huenda kuwa wakabakia chawa
 
Back
Top Bottom