Mwigulu Nchemba acha kudanganya wananchi, mikopo hulipwa na watanzania wanapolipa kodi. Usipotoshe umma

Mwigulu Nchemba acha kudanganya wananchi, mikopo hulipwa na watanzania wanapolipa kodi. Usipotoshe umma

Katika kosa ambalo wa tz tutafanya nikumpa huyo jamaa cheo kikubwa. Ni mtu hatari mno.
 
Msomi wa uchumi anatuongopea kweupe kuwa mikopo utalipwa na serikali.

Serikali ina hela kutoka .. what sources.. au anatuona sie ni kama job
 
Kwa nini viongozi wa serikali hupenda kuona watu kama wajinga na hawana akili?

Mlipopitisha tozo za serikali kwenye miamala ya simu ulitamka kwa dharau na kejeli kuwa asiyetaka kulipa tozo ahamie Burundi, bila kujali hata namna tozo zinavyoumiza wananchi.

Leo hii unatamka bila hata aibu kuwa mikopo ya serikali italipwa na serikali bila kumgongea mlango mwananchi yoyote nyumbani kwake. Hii inaingia akilini?

Mikopo hulipwa na wananchi wanapolipa kodi za kila namna iwe direct tax or indirect tax. Kw hiyo kwa kadiri mnavyokopa hovyo ndivyo mnavyoongeza mizigo ya kodi kwa wananchi. Sasa kwa nini utamke kuwa wananchi hawalipi madeni ya taifa lao? Hii ni dharau kubwa sana.

Acheni kuwaona wananchi wajinga kisa tu mpo madarakani.
Mikopo hulipwa na wananchi wanapolipa kodi za kila namna iwe direct tax or indirect tax. Kw hiyo kwa kadiri mnavyokopa hovyo ndivyo mnavyoongeza mizigo ya kodi kwa wananchi. Sasa kwa nini utamke kuwa wananchi hawalipi madeni ya taifa lao? Hii ni dharau kubwa sana.
 
ZERO KABISA.
tunaolipa na kuumia ni sisi wananchi ndo maana ukitoa hela Kuna makato ya miamala na UPUMBAVU MWINGINE UNAITWA TOZO YA SERIKALI.
Na kodi nyingine tunazokamuliwa .
Serikali inatoa wapi hela?
 
Back
Top Bottom