Waliotajwa na mwana-CCM Kindakindaki wote ni wana-CCM, tena waliowahi kuhudumia ngazi za juu kabisa serikalini!
Kama ndivyo, hatimae mwana-CCM Kindakindaki unatuthibitishia kwamba CCM na Viongozi wanaotokana na CCM ni kansa kubwa kwa taifa!
Mosi, inaonekana kwamba CCM na Viongozi wanaotokana na CCM ni watu walioptopewa na ujinga vichwani manake ikiwa mtu unaogopa kurogwa kupitia nguo, huo ni ujinga kuliko hata ujinga wenyewe!
Pili, inaonekana kwamba CCM na Viongozi wanaotokana na CCM hawaziamini biashara za Kutanzania kwa sababu ikiwa wanaamini wanaweza kurogwa kupitia nguo walizopeleka dry cleaners, ina maana hawaamini HATA PUNJE ya weledi wa KAMPUNI ZOTE za dry cleaners za TZ
Tatu, kama nguo tu wanapeleka nje ya nchi kwa kuogopwa kurogwa kupitia nguo; je walikuwa wanakula mchele wetu wa Mbeya hawa?! Walikuwa wanatumia nyanya zetu za Lushoto hawa? Walikuwa wanatumia maji yetu ya Uhai, Kilimanjaro, and the like hawa?!
Ni ujinga wa wana-CCM na Viongozi wanaotokana na CCM au ni kutaka kuwakoga wananchi maskini wanaowapatia huo uongozi?!