Lyambalyetu
JF-Expert Member
- Apr 6, 2021
- 278
- 255
Tangu ateuliwe Uwaziri wa Fedha, Dkt Mwigulu Lameck Madelu Nchemba, amekuwa very humble. Amesha-adopt utaratibu na upole wa Mhe. Samia Suluhu Hassan. Juzi alionana na Ndugu yangu ndani ya viunga vya bungeni - kwa kweli Dkt. Mwigula ameshabadilika.
Kabadilika faster - tena faster haswa. Kwa sasa hakukimbii anakusikiliza na kukupa ahadi nzuri. Hana tena kuhoji hoji - anaonesha ule utaratibu wa kifedha - yaani hata ngozi yake na hata mikono yake sasa inaonesha ni Waziri wa Fedha kweli kweli. Dkt Mwigulu kafika kwenye nafasi yake sasa. Anaonekana kuicheza vema nafasi yake - atafika mbali.
Kwa sasa haoneshi tena makeke ya kuutaka URais - yeye anachapa kazi tu. Jimboni anatoa maelekezo na yanatekelezwa. Anafanya siasa za kuwabakiza wapiga kura - hili litaonekana zaidi wakati akiwasilisha bajeti yake. Huku jimboni kwake tayari kuna viashiria vya uhakika kuwa kipindi hichi atakimaliza kwa mafanikio zaidi kuliko vipindi vyake vyote vilivyopita. Hamna mbunge ambaye amewahi kuacha alama Jimbo la Iramba tangu kuanza kwake - uliza Nalingigwa, Nkurlu, Kiula, Shango na hata Kilimba hamna walichoacha cha kukumbukwa nacho Iramba. Kama kipo hebu mtu aniambie hapa.
Dkt. Mwigulu Nchemba anaelekea kuacha legacy kwa miaka 15 atakayoongoza. Hata hivyo ninamtahadharisha kuwa mapaka sasa naye ubunge wake unaelekea kulingana na wa Nalaila Kiula - huyu naye aliongoza miaka 15 lakini hakuacha alama yeyote. Kwa kweli mpaka sasa Dkt. Mwigulu hana kitu cha kujivunia, miradi ya Serikali ni hiyo hiyo hata asingekuwepo yeye ingekuwepo tu. Nina uhakika kwa miaka 15 kama hatakuwa na jipya Dkt. Mwigulu atatemwa na WanaIramba. Yangu macho! Tena macho makubwa kweli kweli!