Mwigulu Nchemba, hata kama Magufuli hayupo hai ulipaswa kumheshimu

Mwigulu Nchemba, hata kama Magufuli hayupo hai ulipaswa kumheshimu

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Nimemsikiliza Mhe. Mwigulu Nchemba akimwagia sifa za umairi Jakaya Mrisho Kikwete, nimeshangazwa sana na kitendo hiki kwa sababu zifuatazo;

Mwiguli alikuwa anawasilisha hotuba ya bajeti ambayo kimsingi haina hoja mahususi inayolazimisha kumtaja JK, Magu Wala Mkapa. Ni Nini kimemsukuma kuweka paragraph hii kwenye hotuba yake? Anamsuta Nani?

Hata Kama JK alikuwa kiongozi, Magufulu pia alikuwa kiongozi. Unapotoa sifa za kiongozi ambazo hazishabiani na kiongozi asiyekuwepo Duniani huku huko nyuma hukuwahi kutoa sifa Kama hizo kwake nikuutangazia umma kwamba huna na ujawahi kuwa na heshima kwake Bali ulikuwa unatafuta madaraka.

Lakini pia kumtaja Jakaya Kikwete kwa kumuunganisha na Mama Samia kunaleta picha kwamba bila JK uamini Kama Rais aliyepo anaweza kuongoza nchi. Naweza nisiwe sahihi lakini mitandao yote inaandika kwamba JK ndiye anayeongoza nchi kwa Sasa, Waziri wa fedha na timu yako kitendo chakuibgiza sifa za JK nikumdhalilisha Rais kwa kuonyesha umma kwamba wanayosema wanaharakati na watu wengine ni sahihi.

Lakini pia napata mashaka na uwezo binafsi wa mtu huyu katika nafasi hii nyeti, Wizara ya fedha ni nyeti. Aina ya bajeti aliyowasilisha inahitaji elimu kubwa kwa umma iweze kuonekana kwamba ina malengo chanya na kuepusha upotoshaji wakimantiki unaoweza kufanywa na watu wasio serikalini. Kuwasilisha bajeti Kama hii huku ukiweka sifa za JK kumeligawa Taifa na chama pia.

Watu wengi wameondoka kuijadili bajeti wamejadili udhalimu na unafiki wakimfumo unaofanywa na wanasiasa kuwasaidia kuendelea kuteuliwa. Madhara yake ni kwamba upotoshaji utakuwa mwingi nakupunguza imani ya wananchi kwa serikali.

Utavuna ulichopanda, na naamini au natabiri hii itakuwa bajeti yako ya mwisho Kama Waziri wa fedha. Soon utajionea labda kama hawataona damage yako kwa macho ya Tanzania mpya
 
Kuhusu kumsifia JK sijui kafanya hivyo kwenye mazingira yapi kama yalimlazimu kufanya hivyo.

Lakini kwa tabia za kujipendekeza za hao jamaa sitashangaa kama amefanya hivyo kwa lengo maalum akijua fika JK kwa sasa ndie remote ya ikulu yetu, na yeye Mwigulu hastahili kuwepo kwenye hiyo wizara hasa baada ya ile kashfa ya kupotea bilioni tatu kwenye wizara yake.
 
Back
Top Bottom