Mwigulu Nchemba, hata kama Magufuli hayupo hai ulipaswa kumheshimu

Tulishauri humu kuwa Mama yetu aache ku recycle hawa Wabunge ambao mostly ni incompetent, Sio huyo tu kuna kundi kubwa la Minister linahisi ugali wao utamwaga soon ivo the only way ni kusaka Cheap popularity ili ata wakienguliwa Nafasi zao basi wawe wamevuna mtaji wa kisiasa wa kutosha wa kuja kuwaweka Madaraka baadae angalia alichokifanya waziri wa nishati ila pia tujue kuwa Mwigulu amesababisha damage ambayo haiwezi kuvumilika amekuja kuprove right kwa activists walioko Jamhuri ya Twitter
 
Una akili sana
 
mh, ila yanayomkuta JK kikwete nina hakika hata Nyerere hakuwahi kuyakabili......jamaa anaandamwa sana aisee;

wakati wa utawala wake chadema walihakikisha hafanikiwi kwa lolote, kiubishi ubishi sana akapenya!

anaandamwa kuwa eti alimsaliti lowassa.....yet, hakuna mwenye kuujua undani hadi sasa.

wakati wa utawala wa mwendazake, aliandamwa mno kwa kukosolewa kuwa hakufanya chochote wakati wa utawala wake na hata kunyamazishwa 'kibabe' mbele ya kamera pale aliojaribu kutoa maoni, hilo lilifanywa na mwendazake mwenyewe na 'washikadau' wake.

sasa hivi (wakati huu wa awamu hii ya sita), anaandamwa kwa kila hatua anayoichukua mama.....kwamba eti ndiye anayeongoza nchi sasa. kama hilo halitoshi, anaambiwa kuwa anahusika na kuondoka kwa mwendazake. kivipi? hakuna mwenye jibu.

Mungu ni mkubwa, na mapito haya pia yatapita......pole sana JK Kikwete, tunapokuona na tabasamu lako pamoja na yote haya, hakika wewe ni jasiri sana!!
 
Kikwete ni Smart na Hazina kwa Taifa hili Mungu ampe maisha marefu
 
Mkuu like genge la kutaka itawala nchi hii lililoanzishwa Mwaka 1995 bado lipo na sasa limegaij momentum😆😅
 
Nchi yetu inashida sana hasa kwenye mifumo, ona sasa mtu badala ya kukonsetreti kwenye budget anawaza cheo chake kwanza
 
Ni jitu la ajabu sana. Liliua ndugu zetu Arusha olesiti. Halafu cha kushangaza lili steji ajali
Hii dhambi haita mwacha, aendelee kujichekesha na kujikomba.
Hii ngoma inamsubiri.
 
Utavuna ulichopanda, na naamini au natabiri hii itakuwa bajeti yako ya mwisho Kama Waziri wa fedha. Soon utajionea labda kama hawataona damage yako kwa macho ya Tanzania mpya

Wazungu wanasema "WAKORA WAIYTU" ... !!!

Bity umenena vema sana leo nafumba macho kuombea utabiri wako utimie katika maono uliyoyaona ... ili siku moja nifukue hili kaburi huku niki usifu UFALME wa MUNGU dhidi ya watu wanafiki, wazandiki na watu wabaya wanaopaka mafuta kwa mgongo wa chupa watu wasio utu aina ya MWIGULU NCHEMBA
 
Mkuu ndio ujue unafiki wa viongozi wetu
Mkuu ndio ujue unafiki wa viongozi wetu, wao wanajali matumbo yao, pamoja na kuwa Mwigulu anafahamika kuwa ni timu mzoga ni aibu kwake kuonyesha unafaiki mbele ya umma, nadhani sasa watu wanajionyesha tabia zao zilivyo ni watu wa kujikomba kwa viongozi waliopo,wakishaondoka tutakuja kuwasikia wakisema ah raisi fulani alikuwa dhaifu ah yule alikuwa vile, kuna wakati nasikia kichefuchefu ukiwasikia wanasiasa wetu,yeye badadala ya kusoma bajeti anawasifia waliompa ugali ,watu wanajua kujikomba. Kifupi wanasiasa hawaaminiki huyu Mwigulu si ndie kila siku alijifanya mtetetzi wa mwendazake kwa kuwajibu na kutupa vijembe kwa kina Zitto? hii inatia hadi kichefuchefu.
 
Kwanza ni muhimu tujue Aina ya viongozi tulio nao, Mwigulu ni Opportunist, nakumbuka alivyo ondolewa uwaziri wa Mambo ya ndani alianza kumsifia sana mzee hadi akapewa tena uwaziri wa katiba na Sheria! Ni dhahiri kwamba sasa hivi mshauri mkuu wa Mh. Rais ni Jk hivyo kumsifia kwake sio kwa upendo wa dhati, ila ni kulinda cheo chake alichopewa ili aendelee kudumu nacho
 
Kinachonishangaza
Kinachonishangaza ni kuwa hadi sasa bado ni waziri, pamoja na mapungufu yake mwendazake saa hizi Mwigulu angekuwa anachoma mahindi, sijui jamaa ana kizizi gani kila wizara anaharibu halafu anapelekwa kwingine nako anaharibu lakini bado anakuwa yupo tu, au ile tai anayovaa ndio kinga yake?
 
Ukiona hivyo ujue ni jasiri na kiongozi shupavu. Yupo kasimama akipokea kashfa ila ndie icon pekee ya raisi wastaafu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…