hivi ni kweli huyu Mwigulu ana PHD?soma maandishi yake hapa chini tafadhali
UNPATRIOTIC! Mng'ang'ana hawajatangaza corona ipo, Kwani corona ni kama mwewe au mwizi unaweza kuifukuza kwa mayowe!? Eti hawajatoa takwimu, Hivi tukifanya sensa kila asubuhi nani anaumwa na kutaja kama mafungulio ya wafungwa ndio wanapona? Tukitaja waliopoteza Maisha hata wa magonjwa mengine tuseme ni corona ili idadi iwe kubwa ndio corona itatuonea huruma iondoke? Tukiwatisha sana watu wakawa na hofu sana ndio corona itakimbia? Mataifa waliokuwa busy na lockdown, corona imekimbia? Waliokuwa busy na kutangaza vifo na orodha, corona imekimbia? Waliokuwa, wamefanikiwa kitu gani mpaka tuone tuliomtanguliza Mungu tumekosea! ETI HATUMWONI RAIS, MMEKWENDA OFISINI KWAKE MKAMKOSA? MLIKIWA NA APPOINTMENT NAYE
Kiongozi wa Nchi sio Parishworker Kanisani wala sio Mzee wa Kanisa kwamba alipangiwa zamu na hakuonekana!, Kiongozi wa Nchi Sio Mtangazaji wa TV kwamba alikuwa na kipindi Ila hakuonekana! Kiongozi wa Nchi sio kiongozi wa jogging clubs kwamba anatakiwa kuwa tu mtaani kila siku na kurusha selfie. TUACHE UPUUZI UPUUZI HATA KAMA HATUNA JAMBO LA KUFANYA. Umeichafua sana nchi umeshindwa, mmetamani tukwame mmeshindwa,Sasa mnaombea mabaya nchi yetu na Kiongozi wa Nchi yetu. SHERIA YEYOTE INAPOVUNJWA, HAKUNA CHA MIPAKA, WALA HAKUNA CHA MUDA KUPITA. KWA WANAOROPOKA ZINGATIENI KIFUNGU CHA 89 cha Penal code na 16 cha Cyber Crime, SERIKALI IPO KAZINI