Ukiwa na matumaini makubwa ya kuwa raia namba moja nchini, ulianza kampeni mapema kwa kuandika mabango kwa mamia katika maeneo yote muhimu na pia katika structures nyingi zilizo barabarani nchi nzima!
Kwa kuwa umegonga mwamba katika matumaini yako tafadhali tumia mbinu zile zile ulizotumia kuyaandika mabango hayo kuyafuta kwani sasa yamekuwa uchafu!
hv ni nani kwanza alekua anaandka. . au n yeye mwenyewe anaingia nyt anachora af anasepa?
msamvu stend morogoro alichafua kweli ila sasa wameanza kufuta.
Naamini yakiachwa kuna siku akipata akili atayachukia na yeye
Wana bodi kwenye kinyang'anyiro cha kampeini za kuusaka urais kupitia ccm mwaka huu ndugu Mwigulu Nchemba anaonekana alikuwa na mbinu kali ya kuandika mabango kwenye miamba, madaraja, miti mkikubwa nk sasa uchaguzi umeisha atumie njia ile ile kufuta maneno yanayosema Mwigulu Nchemba ni rais 2015 vinginevyo atakuwa ana mkana dr magufuli.
Anapunguza gharama za 2025, mwaka huo ataondoa namba 1 kwenye 2015 na kuweka namba 2 ili isomomeke 2025. Ni mchumi yule. Si unajua masuala time-value for money.~~~>>Kwenye daraja la Lembeni huku Kilimanjaro amechafua.
~~~~>>>Njia Panda hapa Kilimanjaro pia amechafua
Njoo utufutie huu Uchafu Wako....