Mwigulu Nchemba: Tumepokea maoni ya tozo, tunashughulikia

Mwigulu Nchemba: Tumepokea maoni ya tozo, tunashughulikia

Mwigulu Nchemba, wafafanulie watanzania tofauti ya tozo na kodi. ( Makamu wa Rais aliyekuwa Waziri wa fedha asaidie kufa fauna).

Kuna uweze kano mkubwa wizara ya fedha ikachangia mpasuko mkubwa Kati ya serikali na wananchi hasa kuelekea 2025.
Hz habari za kuelekea 2025 zinatuchelewesha ww sema kinaweza kunuka muda wowote 2025 mbali sana mateso ni makubwa,aliyeshiba hamjui mwenye njaa.
 
Weka Hela cash ya matumizi ya mda flan.Zingne zitunze Kwa crypto inform of stable coins kwenye wallet flan au exchange unaimn.Sisi tusio katika mifumo rasmi wengne tuna bank system zetu sahzi.Tozo zinanigusa mara chache sana.Blockchain and crypto is the future
 
Waziri wa fedha Mhe. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imesikia kilio na malalamiko ya wananchi wake kuhusu vipengele kadhaa vinavyohusiana na tozo.

Mfano wa mapendekezo hayo ni uwepo wa makato mara mbili kwenye miamala ya simu wakati wa kutuma na kutoa. Kupitia mkutano wake na waandishi wa habari amesisitiza kuwa muda si mrefu hatua stahiki zitachukuliwa.

Kuhusu tozo za benki, serikali itakaa na watoa huduma hiyo ili kujadiliana tena kwa mara nyingine.

Kuhusu kodi ya pango, waziri amebainisha kuwa mpangaji siyo mdaiwa bali yule mwenye nyumba hivyo haitawahusu wao. Hata hivyo ili kuondoa mgogoro kati ya wapangaji na mwenye nyumba, serikali itazingatia maoni ya watu waliopendekeza kuwaondoa wapangaji kwenye kadhia hii ili serikali idai moja kwa moja kwa wamiliki wa nyumba.

Waziri amekiri kuwa lengo la kodi hii (ya pango) ni zuri lakini kulikuwa na upungufu kwenye mkakati wa ukusanyaji wake hivyo wao kama serikali watajitathimini kuona wanafanyaje.
Way back then (2021), ilikuwa ni ngumu sana kumshauri Mwigulu Lameck Nchemba, jambo lolote juu ya sera za uchumi kwa kuwa ndio alikuwa ametoka kumaliza PhD.
At that time Mwigulu alikuwa akijiona kuwa 'he was on top of the World'. (Oh Yes! He was on top of the World, but he was underneath the real World~ a World of realities).
Kama serikali, tulikuwa tunahitaji ku raise around 1.5T ili kukabiliana na matumizi ya ziada ya serikali kwa hiyo mezani kwa Mwigulu zilikuwapo proposal nyingi.
Mie kwa upande wangu nilipendekeza tuongeze VAT kwa asilimia 2.
Lakini wewe kama undergraduate ungeweza kumueleza nini Mwigulu ambaye alikuwa ametoka kuhitimu PhD ya uchumi?
Basi, tukaamua kwenda na proposal za mchumi mwandamizi; Mwigulu Lameck Nchemba ambazo zilizalisha 'tozo kila mahali'!
So, kwa lolote linaloendelea kuhusu tozo, asilaumiwe Samia, wasilaumiwe wachumi wa serikali, wala wanasiasa wengine bali, Mwigulu na PhD yake abebe msalaba wake mwenyewe!
Apart from term papers and group assignments, Mwigulu's economic policies had never been tried anywhere in real World, so when he put them into experiment, in real World, they quickly blew on his face. So here we go again...
 
Yaani mtasababisha maisha yazidi kuwa magumu kwa wapangaji kwani walio wengi ni maskini. Ukimtoza mwenye nyumba automatically itamuathiri mpangaji. Mfano kama mpangaji analipa Kodi 30000 kwa mwezi bila tozo, mkimwekea makato ya tozo Nate ataongeza Kodi. Hivyo moja kwa moja atakaye athirika ni mpangaji. Serikali inapaswa kufanya research kabla ya kuja na mambo mapya
 
Huyu jamaa ni kila tafsiri ya neno kilaza. Hata sijui hiyo Phd aliipataje pataje. Ni mvivu wa kufikiria mpaka imekuwa kama ugonjwa.

Samia kama una chembe ya huruma iliyobaki ndani ya nafsi yako juu ya Watanzania naomba tuondolee huyu kiumbe. Kama ana ulazima wa kuwa waziri basi japo mpeleke wizara nyingine yeyote lakini sio hii ya fedha, imemuelemea. HAIWEZI.

Kuweni na Akili basi Watizedi.hivi unadhani kuwa Waziri wa fedha anaweza kufanya lolote bila endorment ya Samia . ? Yaani kesi ya Mbuzi aliyekufa unampelekea Muuza Supu ,

Simply TOZO kaleta Samia, Samia na system yake ni rotten system and she is incompetent to the position. Wakati Ngosha anakufa lita ya mafuta ilikuwa ni 1700. Leo Lita ni 3380 !

Watizedi acheni ujinga kulaumu waziri. The Top Dog pale magogoni ndiyo shida. 90% ya watizedi hatumtaki SAMIA ; unless wale ambao wananufaika nae.
Now unatoa elf 20 hupati hata lita 5 , wakati enzi za JPM , elfu 20 ni lita almost 12 .
Ni mambo ya Hovyo !
 
Mi mwenyewe nawasubiria waje wanipekue.
Ila Tozo na ile "23% thing" Mwigulu kamwingiza Maza chaka

Hapa ndio mnapokosea. Anamuingiza vip mama Chaka as if all decision zinatoka kwa Mwigulu. Hilo suala la TOZO linaanzia kwa Rais ambaye ndio Target .... hao wa chini ni kutekeleza maagizo . Nasema tena suala la TOZO the president must be held responsible in a very serious note .
 
jamaa ana akili sana anajua wabongo tunalalamika bila kufanya chochote!! na Bimkubwa hawezi kumtoa maana matozo yake yanaijaza sirikali mapesa, swali la kujiuliza hayo mapesa yanaenda wapi barabara za vumbi ziimejaa kwenye majiji SGR inasuasua, Nyerere Dam hapaeleweki, umeme tangu Mwendazake aondoke mgao umerudi! hii serikali inaboa kinoma!
ila labda after 2 years tutampigia makofi miundombinu ikiisha!

Barabara za mwendokasi mbagala ni mwaka wapili hazijakamilika ; huku tozo zinaliwa, keko mataa ile njia ni majanga... Magomeni yote kupitia kigogo na karume kila siku kunajengwa pale na hapakamiliki na tozo zinakatwa.

Hii nchi ina watu wq hovyo halafu kuna very dirty system ya ulaji wa wachache.

Ili tutoke hapa tulipo, ni lazima VIONGOZI wawe na nidham na raia na mali zao, na hii nidham haiwezi kutokea mpaka TUUANE wenyewe kwa wenyewe kwanza. Nadhani huko ndio CCM inatupeleka na nisuala la Muda, nchi nyingi zilizoendelea waliuana Kwanza wenyewe kwa wenyewe ndio wakaheshimiana. Hapa TZ hatuheshimiane viongozi wanafanya maamuzi bila ya kujali impact .
 
Mchumi gani hajui double tax mpk uraini kuchemke ndiyo anakumbuka. Yeye na Babu Tale hawana tofauti.
 
MAKARANI WA SENSA KATIKA ZOEZI LA SENSA ZA MAKAZI KUNA MAKOSA WAMEFANYA WAMEHESABU MPAKA STOO ZA MKAA ,VYUMBA VYA WALINZI N.K,SEREKALI KUPITIA WENYEVITI NA MAKATIBU WA SEREKALI ZA MITAA HAWANABUDI KUPITA UPYA KUHAKIKI HILI.
 
Hapa ndio mnapokosea. Anamuingiza vip mama Chaka as if all decision zinatoka kwa Mwigulu. Hilo suala la TOZO linaanzia kwa Rais ambaye ndio Target .... hao wa chini ni kutekeleza maagizo . Nasema tena suala la TOZO the president must be held responsible in a very serious note .
The immediate victim is this "phd ya Uchumi" thing,Maza tutakutana naye 2025 akili zikitukaa sawa.
Tozo ituzindue
 
Back
Top Bottom