Mwigulu Nchemba: Tumepokea maoni ya tozo, tunashughulikia

Mwigulu Nchemba: Tumepokea maoni ya tozo, tunashughulikia

Waziri wa fedha Mhe. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imesikia kilio na malalamiko ya wananchi wake kuhusu vipengele kadhaa vinavyohusiana na tozo.

Mfano wa mapendekezo hayo ni uwepo wa makato mara mbili kwenye miamala ya simu wakati wa kutuma na kutoa. Kupitia mkutano wake na waandishi wa habari amesisitiza kuwa muda si mrefu hatua stahiki zitachukuliwa.

Kuhusu tozo za benki, serikali itakaa na watoa huduma hiyo ili kujadiliana tena kwa mara nyingine.

Kuhusu kodi ya pango, waziri amebainisha kuwa mpangaji siyo mdaiwa bali yule mwenye nyumba hivyo haitawahusu wao. Hata hivyo ili kuondoa mgogoro kati ya wapangaji na mwenye nyumba, serikali itazingatia maoni ya watu waliopendekeza kuwaondoa wapangaji kwenye kadhia hii ili serikali idai moja kwa moja kwa wamiliki wa nyumba.

Waziri amekiri kuwa lengo la kodi hii (ya pango) ni zuri lakini kulikuwa na upungufu kwenye mkakati wa ukusanyaji wake hivyo wao kama serikali watajitathimini kuona wanafanyaje.
Atuambue Nani muagizaji mkuu wa YU Tong 60 na zimelupuwa kiasi gani pamoja na Kodi hadi uingie barabarani.
Sivyo Rais amuru zigawiwe kwenye mashule!.
 
Amesema anaangalia Kutoza tozo Kwa wenye mifugo wengi.
Aisee wakifanya hivyo wataweka watanzania wengi sana ktk hali mbaya sana, wanasema kilimo na ufugaji ni mkombozi Kwa Mtanzania Sasa hapo hapo wanataka kumkamua, ukienda kununua mahitaji yako Kwa ajili ya mifugo yako wanakukamua na mifugo inakamuliwa Yaani Acha tuu
 
Huyu jamaa ni tapeli, tozo na kodi si kitu kimoja kila siku wanasingizia madarasa na hospital. Wakati pato la taifa linapotea kupitia wizi wa taasisi na matumizi yasiyofaa.

Mwananchi kwepa kodi ukishikwa bahati mbaya
Na ukienda huko shuleni elimu mbovu,madawati hakuna na kwenye afya hakuna unafuu.
Unapimwa ila dawa unaambiwa hakuna au wakati mwingine unaambiwa kipimo hiki hakipatikani hapa.
NHIF Mfuko unapumulia machine ,sasa wameboresha wapi tuone? Au zile hela za Corona ndio zimekuwa sehemu ya kujifichia? Ki ukweli mimi siwaelewi hawa wanasiasa
 
Tozo kwa huduma za benki ni uonevu mkubwa , maana benki wana makato yao na wewe unataka hicho hicho nilichokihifadhi ilihali unajua kabisa aliyehifadhi ni mfanyakazi ambaye umeshamkata kodi au mfanyabiashara ambaye unamkata kodi kwenye pato lake analopata kwenye biashara. Unakuja mbele ya halaiki unasema una shahada ya uzamivu kwenye uchumi ilihali vitu vidogo vinavyoimarisha uchumi hauvielewi au sijui ubinafsi kwa kuwa unaweza kulisha familia yako milo mitatu na kuwapeleka wanao shule ya Feza.Mwigulu, Simbachawene , Bashungwa mtuachie nchi yetu, hatuwahitaji maana hamna mawazo yoyote ya ujenzi wa uchumi wa nchi yetu.Mnaita vyombo vya habari kutueleza vitu ambavyo kijana wangu wa shule ya Upili hawezi kuvielezea kwa aibu kwa kuwa pumba.
 
Hayo madarasa na hosipitali vilivyojengwa kwa tozo vikowapi??

Mbona hii wilaya niliyopo hakuna hata choo cha mfano kilichojengwa kwa tozo??
 
Hayo madarasa na hosipitali vilivyojengwa kwa tozo vikowapi??

Mbona hii wilaya niliyopo hakuna hata choo cha mfano kilichojengwa kwa tozo??
Watutajie kwa majina, mimi sijaona ujenzi mpya au mwendelezo wowote significant kwa karibu mwaka sasa.

Mwigulu and Co. lazima waelewe hatukatai kulipa kodi/tozo tunachokataa ni double taxation sijui triple!

Na hatufahamu criteria gani zimetumika kupanga tozo, serikali inakata kiasi fulani mfano katika miamala ya kibenki kwasababu imewekeza nini hapo.
 
Kaka pembe tulia tuu
Katika kila jambo liwe zuri au baya tafuta fursa
Raha zinaweza kukufanya kuwa imara na shida pia zinaweza kukuimarisha
Usichoweza kukibadilisha kitumie kukubadilisha
Kwa iyo wewe kwakuwa ni shemeji yako unafuraia
 
Sio mimi nikuonyeshe ila tujadili nini kifanyike
Kuna wakati unaweza kujikuta analazimika kuiweka pesa yako kwenye mizunguko ili tuu isiingie bank
Wewe ni "Msen..............eee
 
Serikali imekosa ubunifu hata kdg

Wewe Kama Mwananchi mwenye ubunifu kichwani wa vyanzo vya mapato toa hapa kwenye mitandao kusaidiana na serikali hacha kupiga Kelele na kukosoa nyuma ya keyboard matendo sifuri
 
Atuambue Nani muagizaji mkuu wa YU Tong 60 na zimelupuwa kiasi gani pamoja na Kodi hadi uingie barabarani.
Sivyo Rais amuru zigawiwe kwenye mashule!.
Mungu fundi, ngoja ziingie zikutane na wachawi wazifanyie ya dunia. Mali ya dhuluma huisha kidhuluma dhuluma pia
 
Waziri wa fedha Mhe. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imesikia kilio na malalamiko ya wananchi wake kuhusu vipengele kadhaa vinavyohusiana na tozo.

Mfano wa mapendekezo hayo ni uwepo wa makato mara mbili kwenye miamala ya simu wakati wa kutuma na kutoa. Kupitia mkutano wake na waandishi wa habari amesisitiza kuwa muda si mrefu hatua stahiki zitachukuliwa.

Kuhusu tozo za benki, serikali itakaa na watoa huduma hiyo ili kujadiliana tena kwa mara nyingine.

Kuhusu kodi ya pango, waziri amebainisha kuwa mpangaji siyo mdaiwa bali yule mwenye nyumba hivyo haitawahusu wao. Hata hivyo ili kuondoa mgogoro kati ya wapangaji na mwenye nyumba, serikali itazingatia maoni ya watu waliopendekeza kuwaondoa wapangaji kwenye kadhia hii ili serikali idai moja kwa moja kwa wamiliki wa nyumba.

Waziri amekiri kuwa lengo la kodi hii (ya pango) ni zuri lakini kulikuwa na upungufu kwenye mkakati wa ukusanyaji wake hivyo wao kama serikali watajitathimini kuona wanafanyaje.
Nimeshauri mara nyingi sana kwa Mwigulu kwamba task force irejeshwe na Polisi wapewe mamlaka ya kukagua manunuzi ya bidhaa zote walisonunua watu Ili kubaini wasio na risiti..

Watu hawataki Kulipa Kodi Wala tozo ila huduma wanataka kwa kisingizio cha ugumu wa maisha..

Nchi haiwezi kwenda kwa kubelezana kiasi hiki..

Futa tozo ila tight kwenye risiti na wasiokuwa na risiti chukua bidhaa piga mnada.
 
Incompetence,Incompetence,Incompetence

tunapoteza muda sana kufikiria kuna siku incompetent people wanaweza kutuletea mabadiriko, Ukisikiliza issue mbili za leo kuanzia kwenye tozo na kule kwenye Afya kwa wale NHIF inatosha kusema we have bunches of incompetent people in system trying to apply theories in fuckin real business which need the real people to husstle and come up with solutions.
 
Mwigulu ni mchumi sio kilaza😅😅😅😅
jamaa ana akili sana anajua wabongo tunalalamika bila kufanya chochote!! na Bimkubwa hawezi kumtoa maana matozo yake yanaijaza sirikali mapesa, swali la kujiuliza hayo mapesa yanaenda wapi barabara za vumbi ziimejaa kwenye majiji SGR inasuasua, Nyerere Dam hapaeleweki, umeme tangu Mwendazake aondoke mgao umerudi! hii serikali inaboa kinoma!
ila labda after 2 years tutampigia makofi miundombinu ikiisha!
 
Nimeshauri mara nyingi sana kwa Mwigulu kwamba task force irejeshwe na Polisi wapewe mamlaka ya kukagua manunuzi ya bidhaa zote walisonunua watu Ili kubaini wasio na risiti..

Watu hawataki Kulipa Kodi Wala tozo ila huduma wanataka kwa kisingizio cha ugumu wa maisha..

Nchi haiwezi kwenda kwa kubelezana kiasi hiki..

Futa tozo ila tight kwenye risiti na wasiokuwa na risiti chukua bidhaa piga mnada.

WATAKUPINGA

ILA NA WEWE WATAKUJA KUKUKUMBUKA
 
jamaa ana akili sana anajua wabongo tunalalamika bila kufanya chochote!! na Bimkubwa hawezi kumtoa maana matozo yake yanaijaza sirikali mapesa, swali la kujiuliza hayo mapesa yanaenda wapi barabara za vumbi ziimejaa kwenye majiji SGR inasuasua, Nyerere Dam hapaeleweki, umeme tangu Mwendazake aondoke mgao umerudi! hii serikali inaboa kinoma!
ila labda after 2 years tutampigia makofi miundombinu ikiisha!

😃😃😃😃
 
Back
Top Bottom