Mwigulu Nchemba: Tumepokea maoni ya tozo, tunashughulikia

Waziri wa fedha Mhe. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imesikia kilio na malalamiko ya wanachi wake kuhusu vipengele kadhaa vinavyohusiana na tozo.

Mfano wa mapendekezo hayo ni uwepo wa makato mara mbili kwenye miamala ya simu wakati wa kutuma na kutoa. Kupitia mkutano wake na waandishi wa habari amesisitiza kuwa muda si mrefu hatua stahiki zitachukuliwa.

Kuhusu tozo za benki, serikali itakaa na watoa huduma hiyo ili kujadiliana tena kwa mara nyingine.

Kuhusu kodi ya pango, waziri amebainisha kuwa mpangaji siyo mdaiwa bali yule mwenye nyumba hivyo haitawahusu wao. Hata hivyo ili kuondoa mgogoro kati ya wapangaji na mwenye nyumba, serikali itazingatia maoni ya watu waliopendekeza kuwaondoa wapangaji kwenye kadhia hii ili serikali idai moja kwa moja kwa wamiliki wa nyumba.

Waziri amekiri kuwa lengo la kodi hii (ya pango) ni zuri lakini kulikuwa na upungufu kwenye mkakati wa ukusanyaji wake hivyo wao kama serikali watajitathimini kuona wanafanyaje.
Nadhani alipaswa kusitisha kwanza wakati tunasubiria hizo hatua.
 
suala la kodi sio suala la Waziri wa Fedha…ni suala la Serikali na Nchi kwa Jumla

wee hujaskia mtu wa TRC katuma sms kwny group la Wasap kupinga tozo akaenda kupekuliwa kabatini na chini ya kitanda utadhan kuna ma sms mengine yamejificha huko ?
Wizara ya Fedha haina Waziri!
Mh Rais tuvushe hapo
 
suala la kodi sio suala la Waziri wa Fedha…ni suala la Serikali na Nchi kwa Jumla

wee hujaskia mtu wa TRC katuma sms kwny group la Wasap kupinga tozo akaenda kupekuliwa kabatini na chini ya kitanda utadhan kuna ma sms mengine yamejificha huko ?
Yaani tuna nchi ya kijinga sn
 
suala la kodi sio suala la Waziri wa Fedha…ni suala la Serikali na Nchi kwa Jumla

wee hujaskia mtu wa TRC katuma sms kwny group la Wasap kupinga tozo akaenda kupekuliwa kabatini na chini ya kitanda utadhan kuna ma sms mengine yamejificha huko ?
Mi mwenyewe nawasubiria waje wanipekue.
Ila Tozo na ile "23% thing" Mwigulu kamwingiza Maza chaka
 
Kuna kademu kule twita kanamnanga an huyo njemba![emoji38][emoji2957][emoji41][emoji317]
 
Waziri wa fedha Mhe. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imesikia kilio na malalamiko ya wananchi wake kuhusu vipengele kadhaa vinavyohusiana na tozo.

Mfano wa mapendekezo hayo ni uwepo wa makato mara mbili kwenye miamala ya simu wakati wa kutuma na kutoa. Kupitia mkutano wake na waandishi wa habari amesisitiza kuwa muda si mrefu hatua stahiki zitachukuliwa.

Kuhusu tozo za benki, serikali itakaa na watoa huduma hiyo ili kujadiliana tena kwa mara nyingine.

Kuhusu kodi ya pango, waziri amebainisha kuwa mpangaji siyo mdaiwa bali yule mwenye nyumba hivyo haitawahusu wao. Hata hivyo ili kuondoa mgogoro kati ya wapangaji na mwenye nyumba, serikali itazingatia maoni ya watu waliopendekeza kuwaondoa wapangaji kwenye kadhia hii ili serikali idai moja kwa moja kwa wamiliki wa nyumba.

Waziri amekiri kuwa lengo la kodi hii (ya pango) ni zuri lakini kulikuwa na upungufu kwenye mkakati wa ukusanyaji wake hivyo wao kama serikali watajitathimini kuona wanafanyaje.
Hadi Mbowe aseme ndo asikie???

Amenusa kufukuzwa huyo, mkeka mpya waja!!!
 
Back
Top Bottom