Waziri wa fedha Mhe. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imesikia kilio na malalamiko ya wananchi wake kuhusu vipengele kadhaa vinavyohusiana na tozo.
Mfano wa mapendekezo hayo ni uwepo wa makato mara mbili kwenye miamala ya simu wakati wa kutuma na kutoa. Kupitia mkutano wake na waandishi wa habari amesisitiza kuwa muda si mrefu hatua stahiki zitachukuliwa.
Kuhusu tozo za benki, serikali itakaa na watoa huduma hiyo ili kujadiliana tena kwa mara nyingine.
Kuhusu kodi ya pango, waziri amebainisha kuwa mpangaji siyo mdaiwa bali yule mwenye nyumba hivyo haitawahusu wao. Hata hivyo ili kuondoa mgogoro kati ya wapangaji na mwenye nyumba, serikali itazingatia maoni ya watu waliopendekeza kuwaondoa wapangaji kwenye kadhia hii ili serikali idai moja kwa moja kwa wamiliki wa nyumba.
Waziri amekiri kuwa lengo la kodi hii (ya pango) ni zuri lakini kulikuwa na upungufu kwenye mkakati wa ukusanyaji wake hivyo wao kama serikali watajitathimini kuona wanafanyaje.
Way back then (2021), ilikuwa ni ngumu sana kumshauri Mwigulu Lameck Nchemba, jambo lolote juu ya sera za uchumi kwa kuwa ndio alikuwa ametoka kumaliza PhD.
At that time Mwigulu alikuwa akijiona kuwa 'he was on top of the World'. (Oh Yes! He was on top of the World, but he was underneath the real World~ a World of realities).
Kama serikali, tulikuwa tunahitaji ku raise around 1.5T ili kukabiliana na matumizi ya ziada ya serikali kwa hiyo mezani kwa Mwigulu zilikuwapo proposal nyingi.
Mie kwa upande wangu nilipendekeza tuongeze VAT kwa asilimia 2.
Lakini wewe kama undergraduate ungeweza kumueleza nini Mwigulu ambaye alikuwa ametoka kuhitimu PhD ya uchumi?
Basi, tukaamua kwenda na proposal za mchumi mwandamizi; Mwigulu Lameck Nchemba ambazo zilizalisha 'tozo kila mahali'!
So, kwa lolote linaloendelea kuhusu tozo, asilaumiwe Samia, wasilaumiwe wachumi wa serikali, wala wanasiasa wengine bali, Mwigulu na PhD yake abebe msalaba wake mwenyewe!
Apart from term papers and group assignments, Mwigulu's economic policies had never been tried anywhere in real World, so when he put them into experiment, in real World, they quickly blew on his face. So here we go again...